mwananthropolojia
JF-Expert Member
- Oct 6, 2012
- 956
- 638
Mpendwa una mawazo ya ajabu kweli.
1. Ni wazi ya kwamba Ukristo una uhusiano wa karibu sana na Uyahudi. Sehemu kubwa ya Biblia yangu nimerithi kutoka Wayahudi, Yesu yangu alikuwa Myahudi, nimejifunza amnri 10 kufuatana na mapokeo ya Kiyahudi na mengi mengine.
2. Je umeongea na Wayahudi wangapi? - wapi unapata picha ya kwamba wanamwona Yesu mahali pale unapotaja kwa maneno ya ajabu? Si kweli na sidhani wewe una uwezo wa kupima. Wayahudi ninayojua mimi wako pande tatu: wengine hawajali habari za Yesu kabisa; wengine wanamwona alikuwa mmoja kati ya wazushi wengi katika historia ya Uyahudi (ambao bado wanawaona kama Wayahudi!) na wengine tena wanamheshimu kama mwalimu wa maana fulani katika historia ya kiyahudi lakini wakristo hawakumweleewa na kupinda ujumbe wake.
3. Halafu unajipinga kulingana na maelezo yako ya juu. Huko juu ulijaribu kutofautisha kati ya Uzayuni na Uyahudi na kutueleza ni mambo mawili tofauti - hapa unajumlisha yote pamoja. Vipi sasa????
ni kweli ukristo umetokana na uyahudi na yesu ni myahudi lakin wao hawamkubali yesu kama kristo wanamchukulia kama gaidi asiyeitakia mema dini yao na anachomwa moto saiz kwajil ya kukufuru kwa kujiita masiya,hata mafundisho yake yesu kwao hawayakubali wanaendelea kufuata torati waliyopewa na musa na talmud
haitaji kuongea na myahudi kujua msimamo wao wakati magazet,mitandao, vitabu vyao mbalimbali na utaratibu wao wa kusali kama dini hakuna sehemu wanamtambua yesu kama nabii wala masiya na hata ufufuko wa yesu wanachukulia ni utapeli mkubwa
kuna tofauti kubwa ya uyahudi na ukristo ndugu huku unakatazwa kula baadhi ya chakula kama nguruwe nk kwani ni najis na unavunja sheria wakati wakristo wanakula sasa wewe kweli unaielewa dini yako?madhani ww unajichanganya zaidi practically kimatendo na kimafundisho kama unakula kitimoto halaf unajifunza kwenye agano la kale kitabu cha wayahud