Iran Hiding Flight MH370 Boeing--Israeli Security Expert


ndiyo hapo sasa....
 
Hii ni Zionist propaganda za kutimiza majukumu yao ya kuitafutia Marekani na Ulaya mafuta huko Iran. ... Hii sio ndege ya kwanza kupotea kutoka angani.


he...kumbe! mi sikujua kuna ndege zingine zilishawahi kupotea kwa mtindo huu. labda niombe kujuzwa sasa: kumbe ni ndege gani ilishawahi kupotea kwa zaidi ya siku 10 isijulikane imeenda wapi? Ilikuwa ya taifa gani? na hilo lilitokea lini?
 
Na vipi kama hiyo military base ipo kisiwani ambapo hakuna anayeishi zaidi ya kuwepo na militär installations?

Out of 100 hundred sheep, there is at least One black sheep.

Just as an interesting aspect and another detail for understanding the complexity of modern aviation, if you have never seen the radar maps of current flights it is astonishing to see how many planes are in the air around the world at any given time:

Flightradar24.com - Live flight tracker!
 

Una uhakika Israel inategemea silaha toka marekani????? Nakushauri usome vizuri kuhusu silaha za Israel na marekani ndo utajua utofauti pamoja na technology zao...anzia kwenye vifaru kwanza. Isitoshe uliza au fuatilia wataalam wa kivita wa marekani pamoja na wanasayansi kama wa kule NASA na wataalam wa maswala ya ulinzi, madaktari na maprofesa waliobobea pamoja na ma lecturer wa vyuo wengi wao ni kina nani au wana asili ya wapi ndo utachoka zaidi kama siyo kabisa! Achana na hilo taifa teule!
 
Ndege itapatikana na abiria woote wapo salama. T.B joshua aanze kuandaa uongo wa kudanganya wafuasi wake
 

Wewe ni mpuuzi tu ukiwa unaongea porojo bila kuwa na uhakika bali imani na hisia zao zinavyokutuma:

(1) Utashangaa sana utakapogundua kuwa maprofesa wengi maarufu katika engineering kwenye vyuo vingi vya Marekani ama ni Wahindi, au Wachina au Wairani; siyo waisrael.

(2) Silaha nyingi sana kubwa kubwa huko zinatoka Marekani; juzi juzi walijengewa missile defence system iliyoitwa iron dome ili kukabiliana na makombora ya hamas. Ndege zote za kivita za jeshi la Israel ama ni za kimarekani au ni za kifaransa. Hawana kiwanda cha ndege hata kimoja, hata kiwanda cha gari hawana ingawa wanategeneza body za magari zinazohimili milipuko (armoured vehicle body). Viwanda vyao vikubwa vya kijeshi ni vya mizinga tu, hiyo ni kweli lakini vita haipiganwi kwa mizinga tu, wanahitaji vifauru na magari ya kivita kutoka Marekani.

(3) Karibu nchi zote kubwa kubwa zinategeneza bunduki zao wenyewe, hiyo ikiwa ni pamoja na Israel, Misri na hata Iran; kwa hiyo sidhani unahesabu bunduki kama silaha kwa vile hakuna ushindani mkubwa sana katika utengezaji wa bunduki leo hii.
 

Acha ku argue mambo kwa kutumia hisia za udini. Hakuna Israel bila Marekani wewe.

Hiyo NASA, kabla ya hapo ilikuwa inaitwa NACA ilikuwepo kabla hata hiyo Israel haijawa taifa rasmi.

Duniani hapa kuna super power moja tu: The United States of America.

Period, end of story.
 

Ni kweli kabisa hakuna Israel bila marekani.
Lakini hao NACA/NASA hawakuwahi kuwa na mafanikio kabla ya Wernher Von Braun kuingia pale. Huyu jamaa alikuwa ni Mjerumani mwenye asili ya Uyahudi, baada ya kuona Hitler anawaua wayahudi akahisi na yeye siku moja watamshtukia kuwa ana asili ya uyahudi hivyo akawahi kujisalimisha na kukimbilia kwa wamarekani.

Wernher von Braun, Rocket Pioneer: Biography & Quotes | Space.com


[FONT=microstile, arial][h=3][/h][/FONT]
 

Kwa hiyo kumbe hata founding fathers walikuwa Wayahudi eeh? Na baada ya wao kuandika katiba ya Marekani (ambayo kwa kweli ni timeless) ndo Marekani ikaanza kuwa bonge la taifa?

Halafu, hao Wayahudi na hizo akili zao ilikuwaje Hitler akawakaanga namna hiyo hadi wengine wakakimbilia Marekani? Hawakuwa na akili za kumdhibiti au....?
 

kambi za kijeshi za nchi zilizoendelea hazipo naked kama za hapa kwetu to the extent that unawezo kufanya surveillance kutokea angani...kunakuwaga na anti-satellite shield hivyo ni vigumu sana aisee!
 

mkuu unazo taarifa zozote kuhuzu uwezo wa Israel katika utengezaji wa silaha za neclear na mambo yanayohusu tiba? nako ni tegemezi? kuna mkono wa nchi gani ya nje hapo. marekeni? unahitaji kiwanda kikubwa kiasi gani chini ya ardhi kutengeza nuclear war head?
 


naona hitler aliwalia tu timingi...kila binadamu ana flaw mkuu; hata akiwa na akili kiasi gani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…