Iran anachokifanya kwa nchi za Iraq na Pakistan, ni unafiki kusema kuna umoja wa nchi za Kiislamu

Nsanzagee

JF-Expert Member
Jun 28, 2023
1,939
4,117
Ujinga tupu kama nchi yako ikajiunga na kuwa miongoni mwa nchi za Kiislam!

Aliyeikataa OIC nchini petu Tanzania, apewe mauwa yake.

Kinachofanyika na kufanywa na nchi ya Kiislamu IRAN kwa nchi za kiisilamu nyenzake, ni uhuni na ulimbukeni kuendelea kuamini kwamba hili nalo ni taifa linalounga mkono umoja huo wa Kiislamu na kwamba ukijiunga kwenye umoja huo unaweza kupata msaada wowote panapotokea mgogoro wa kivita na nchi nyingine.

Badala ya kuwa na umoja ili kuwalinda na kuwatetea Wapalestine, wao kwa wao tena wanainukiana kufyatuliana makombora! 😂 utadhani siyo waislamu kwa waislamu.

Aliyetaka kutuaminisha kuwa OIC ni suluhisho la ulinzi na kupewa nguvu zote za kiulinzi kutoka nchi washirika wa Kiislamu, alaaniwe mara elfu moja.

Palestine leo inaangamizwa huku nchi hizo za Kiislamu zikichekelea na kutwangana zenyewe kwa zenyewe.

Umoja wa Kiislamu unafaida zipi sasa?
 
Unaongelea umoja wa nchi za Kiislamu unasahau ya kwetu hapa EA community. Juzi tu watu wamepigana pini za ndege kutua. Na bado kuna mengi tu yapo.
Kila mtu anajilinda haijalishi huo umoja.
Eee bhana eee!!!
 
Kurusha makombora nchi ya mwingine unafananisha na mambo ya biashara ya ndege ambayo yamekuwa resolved ndani ya mifa mfupi?
Siasa za mashariki ya kati ni complicated. Mbona hukuuliza Saudia kuishambulia Yemen? Au ugomvi wa Iran na Saudia?
Kuna tofauti gani alichofanya Iran kushambulua maeneo ya anaodai walisababisha mashambulizi nchini mwake na kile alichofanya US kuishambulia Afghanistan kwa madai kuwa Osama kafichwa huko?
 
Ujinga tupu kama nchi yako ikajiunga na kuwa miongoni mwa nchi za Kiislam!

Aliyeikataa OIC nchini petu Tanzania, apewe mauwa yake

Kinachofanyika na kufanywa na nchi ya Kiislamu IRAN kwa nchi za kiisilamu nyenzake, ni uhuni na ulimbukeni kuendelea kuamini kwamba hili nalo ni taifa linalounga mkono umoja huo wa Kiislamu na kwamba ukijiunga kwenye umoja huo unaweza kupata msaada wowote panapotokea mgogoro wa kivita na nchi nyingine

Badala ya kuwa na umoja ili kuwalinda na kuwatetea Wapalestine, wao kwa wao tena wanainukiana kufyatuliana makombora! utadhani siyo waislamu kwa waislamu

Aliyetaka kutuaminisha kuwa OIC ni suluhisho la ulinzi na kupewa nguvu zote za kiulinzi kutoka nchi washirika wa Kiislamu, alaaniwe mara elfu moja

Palestine leo inaangamizwa huku nchi hizo za Kiislamu zikichekelea na kutwangana zenyewe kwa zenyewe

Umoja wa Kiislamu unafaida zipi sasa?
Hizi silaha za hatari kadri zinavyoingia kwenye mikono ya wehu, dunia itaendelea kupata tabu sana.
 
Ujinga tupu kama nchi yako ikajiunga na kuwa miongoni mwa nchi za Kiislam!

Aliyeikataa OIC nchini petu Tanzania, apewe mauwa yake

Kinachofanyika na kufanywa na nchi ya Kiislamu IRAN kwa nchi za kiisilamu nyenzake, ni uhuni na ulimbukeni kuendelea kuamini kwamba hili nalo ni taifa linalounga mkono umoja huo wa Kiislamu na kwamba ukijiunga kwenye umoja huo unaweza kupata msaada wowote panapotokea mgogoro wa kivita na nchi nyingine

Badala ya kuwa na umoja ili kuwalinda na kuwatetea Wapalestine, wao kwa wao tena wanainukiana kufyatuliana makombora! 😂 utadhani siyo waislamu kwa waislamu

Aliyetaka kutuaminisha kuwa OIC ni suluhisho la ulinzi na kupewa nguvu zote za kiulinzi kutoka nchi washirika wa Kiislamu, alaaniwe mara elfu moja

Palestine leo inaangamizwa huku nchi hizo za Kiislamu zikichekelea na kutwangana zenyewe kwa zenyewe

Umoja wa Kiislamu unafaida zipi sasa?
Kaikataa oic lkn wanasiasa hasa wapinzani wanasema
1. Nchi maskini
2. Wanafungwa kila mechi
3. Rushwa
4. Woga
 
Back
Top Bottom