Iran wazipongeza nchi za Afrika kwa kuwatimua Wafaransa na Wakoloni wa Magharibi

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Rais: Mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni ni ishara ya mwamko na kuwa macho

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza kusimama kidete na mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni na ugaidi, na kuyataja kuwa ni ishara ya mwamko, kuwa macho na utambuzi sahihi wa mahitaji ya zama ya nchi hizo.

Rais Sayyid Ebrahim, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo Jumatatu katika mazungumzo yake na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso, Bibi Olivia Rouamba aliyeko safarini mjini Tehran. Ameashiria uhusiano mzuri wa Iran na nchi zote za Afrika baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, na utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu kuhamishia tajriba na mafanikio yake kwa nchi marafiki hususan za bara la Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema kuanzishwa wa Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Burkina Faso kutakuwa na taathira katika kuharakisha mabadilishano ya uwezo wa pande mbili na kuboresha kiwango cha uhusiano na ushirikiano.

Kwa upande wake Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso, Bibi Olivia Rouamba ameeleza kuwa nchi za Kiafrika, ikiwemo Burkina Faso, zimetiwa moyo na muqawama wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya ubeberu na kusema: "Ajenda muhimu zaidi ya serikali ya Burkina Faso ni kutia msukumo katika ushirikiano wake na Iran."

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso amesema: Nchi yake ina hamu ya kuimarisha ushirikiano na nchi rafiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4c3pc708eb57a22cvne_800C450.jpg
 
Hawa wairan waache ujeuri.
Wakae meza moja na mahasimu wao 'wazungumze kiume' uhasama ufike mwisho, maisha yaendelee...
 
Mazungumzo yalishafanyika na muafaka ukapatikana alivyoingia trump akavunja makubaliano yote sasa ww unataka iran azungumze nn tena hyo tabia ya kunyenyekea wazungu tunayo sisi africa kuogopa kunyimwa misaada tunafanya hata ambavyo havina maslahi kwa mataifa yetu kwa kuwaogopa
 
Mbona wao wapo Yemen, Lebanon na Syria na wao wakitolewa berenge tushangilie?
 
I get your point. American leaders should be guided by 'mere prudence' to understand that this is an hour of need for the World at large, where the oil prices are skyrocketing and choose to ease sanctions (for 6 months at least) so that Iran can start again to export oil around the World to cover for Russia's lost supply.
 
Mbona wao wapo Yemen, Lebanon na Syria na wao wakitolewa berenge tushangilie?
Wao wapo Syria tu kwamualiko rasmi huko kwengine hawapo kama wapo leta ushahidi na kila alipo Iran hua analeta Amani sio kama hao mabeberu mauaji makubwa hayo
 
Mazungumzo yalishafanyika na muafaka ukapatikana alivyoingia trump akavunja makubaliano yote sasa ww unataka iran azungumze nn tena hyo tabia ya kunyenyekea wazungu tunayo sisi africa kuogopa kunyimwa misaada tunafanya hata ambavyo havina maslahi kwa mataifa yetu kwa kuwaogopa
True thus huwezi ona wazungu wakiwalazimisha wachina waarabu wapandane kama wanayo kwetu
 
Rais: Mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni ni ishara ya mwamko na kuwa macho

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amepongeza kusimama kidete na mapambano ya nchi za Kiafrika dhidi ya ukoloni na ugaidi, na kuyataja kuwa ni ishara ya mwamko, kuwa macho na utambuzi sahihi wa mahitaji ya zama ya nchi hizo.

Rais Sayyid Ebrahim, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo Jumatatu katika mazungumzo yake na Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso, Bibi Olivia Rouamba aliyeko safarini mjini Tehran. Ameashiria uhusiano mzuri wa Iran na nchi zote za Afrika baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, na utayarifu wa Jamhuri ya Kiislamu kuhamishia tajriba na mafanikio yake kwa nchi marafiki hususan za bara la Afrika.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pia amesema kuanzishwa wa Kamisheni ya Pamoja ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Iran na Burkina Faso kutakuwa na taathira katika kuharakisha mabadilishano ya uwezo wa pande mbili na kuboresha kiwango cha uhusiano na ushirikiano.

Kwa upande wake Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso, Bibi Olivia Rouamba ameeleza kuwa nchi za Kiafrika, ikiwemo Burkina Faso, zimetiwa moyo na muqawama wa Mapinduzi ya Kiislamu dhidi ya ubeberu na kusema: "Ajenda muhimu zaidi ya serikali ya Burkina Faso ni kutia msukumo katika ushirikiano wake na Iran."

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Burkina Faso amesema: Nchi yake ina hamu ya kuimarisha ushirikiano na nchi rafiki ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

View attachment 2740205

MWANAPROPAGANDA MUQAWAMA WA KISHIA KWA UPANDE WA AFRIKA MASHARIKI.
 
Back
Top Bottom