Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,194
- 10,929
Maamuzi ya Iran kushambulia maeneo ndani ya Iraq na Pakistan bila ruhusa ya nchi hizo kwa kisingizio cha kuwafuata maadui zake yanaweza yakawa ni maamuzi ya kizembe katika kipindi hiki kigumu kupambana na Israel ili aiachie Palestina.
Iran isingepaswa kuchukua maamuzi ya kibabe kama yale yanayochukuliwa na Marekani na washirika wake na kwa kweli haijawa na nguvu za kufanya ubabe kama wa nchi hizo.
Pakistan ni moja ya mataifa muhimu kati ya nchi za kiislamu ambayo japo haijaamua kuingia vitani rasmi kutetea wapelestina lakini wananchi wake ni miongoni mwa makundi makubwa yenye hasira sana kutokana na maumivu wanayoyapata wapalestina chini ya mikono ya Israel
Ilichopaswa kufanya Iran hasa kwa Pakistan ilikuwa ni kuishawishi iungane naye kwa kutoa silaha zake ili kuwasaidia wale wote wanaopigania Palestina kama vile wanamgambo wa Houth.
Wanamgambo wa Houth wana nia thabiti na wameiweka wazi ya kutaka kuipiga Israel ili isiendelee kuwaua watu wa Palestina hasa kule Gaza.Pamoja na nia hiyo na majaribio yao kadhaa bado Houth hawajafanikiwa kuizamisha meli yoyote wala kuleta mripuko kwenye meli inazozipiga kiasi ya kusababisha hasara kubwa kwa Israel.
Miongoni mwa nchi ambazo zina silaha na teknolojia kubwa za kivita kati ya mataifa yanayopaswa kuwatetea watu wa Gaza ni Uturuki na hiyo Pakistani.Katika ukweli huo Iran ilipaswa kulielewa hilo na bila sha inalielewa na hivyo ilitakiwa wawafuate kidiplomasia kuwaomba watoe ushirikiano ili kuidhabu Israel badala ya wao kwenda kupiga maeneo ya nchi zao hata kama kuna wapinzani wao.