Iramba Tuna Bahati Mbaya ya Wabunge

Iramba Tuna Bahati Mbaya ya Wabunge

Kama Wanyiramba wote wangekuwa werevu kama wewe (Iramba), matembe yangebaki kuwa historia mkoani Singida. Ila, mh! Ni wachache ndo wanajitambua.
 
Niko Hapa Nje Ya Tembe Langu Nikijiandaa Kwenda Kuwafukuza Kwelea Kwelea Wasinimalizie Mtama Wangu!
Ninapoiwaza Changamoto Hii,Ninazi Waza Pia Changamoto Zingine Ambazo Wabunge Karibu Wote Zimewatoa Technical Knock Out(K.O)!
Si Kilimbah,si Mwigulu!
Mathalani Kuna Ahadi za Muda Mfupi Alizo Ziahaidi Madelu Ambazo Mpaka Sasa Zimemgalagaza!
Aliahidi Maji Kata ya Mtoa Ndani ya Miezi Miwili,Umeme Kata ya Mtekente Ndani ya Miezi Minne,Kumalizia Kipande cha Barabara ya Old Kiomboi na Kumalizia Barabara ya Shelui-Kidaru Miezi Akisha Apishwa,ila Mpaka Sasa Hatuoni Lolote!
Madelu,Barabara ya Tulya-Kiomboi Kupitia Juu ya Mlima Sekekenke,ni Mbovu na Laiti Kama Ingeboreshwa,Tungeokoa Maisha ya Wagonjwa Wengi Wanaotokea Mingela,Misri,Bambaraga,Yombo,Mesi,Doromoni,Migilango Shauritanga na Mauguru!Wangewaishwa Kupata Huduma Tofauti na Sasa,Ebu Rudi Uichonge Upya!
Madelu,Jesica Kishoka Mwanamke Mwenye Sumu Kali,Analiwinda Jimbo la Iramba Na Sumu Anayo Wadunga Vijana ni Kali na Haiwezi Kuwa Neutralized!
Rudi,Vijana Wako Wamekosa Hoja Mbele ya Wana CHADEMA"
Rudi na Ukae Na Sio Kama Majuzi Ulipo Tuchungulia Katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Fedha na Mipango!
Rudi na Umkumbuke Kijana Wako Imma Mapikiki na Siye Wote Kama Ulivyo fanya 2010!
Najua Umeme Ushakupiga Toba Baada ya M.C.C2 Kukupiga Chenga ya Mwili na Hata Ahadi ya Kujenga Kiwanda cha Kukamua Mafuta ya Alizeti Hapa Kata ya Tulya Ishakufa Kibudu!
Ubunge Kwanza Uwaziri Baadae!
Jamani Acha Niwawahi Kwelea Kwelea Wasije Nitenda!
Karibuni Kiporo cha Nyama ya Punda na Magae Makanta!
Poleni sana mkuu miaka mitano sio mingi kinachotakiwa ni kufanya mabadiliko ya kweli 2020 . Kinachonishangaza ni haya magamba yanalalamika lema hajajenga hospital wakati wabunge Wao wamehamia Dar . Hawaonekani majimboni na hawafanyi maendeleo yyte.
 
Kama Wanyiramba wote wangekuwa werevu kama wewe (Iramba), matembe yangebaki kuwa historia mkoani Singida. Ila, mh! Ni wachache ndo wanajitambua.
walevu wachache,wajinga wengi!ila kuna siku tutafika tupatakapo!
 
chadema wangeanza mapema na zile kampen zao za mkoa kwa mkoa.... (kama zile za m4c, sangara)

wataongeza wanachama.
izo kampeni zitaanza mapema baada ya bunge la bajeti,huo ndio mpango wa wanachadea,ila mikutano huwa inawafungua watu wengi,kwani hufundishwa elimu ya uraia na elimu ya haki zao,na ndio maana mwigulu anamwogopa yule mama wa chadema,JESICA KISHOA
 
Magufuli hawezi akatoa katiba mpya yenye TUME huru 2020 sababu ya nguvu ya Lowassa!

Magufuli kaisha wagawa hadi wana CCM so atakuwa na upinzani mkubwa sana 2020 kwanza ndani ya chama na baadae uchaguzi mkuu,hawezi akaruhusu TUME HURU
kumbe!hio itaufanya uchaguzi wa 2020 kuwa mkali sana,na kama haitoshi magufuli ana bifu na watumishi wa umma,sasa kama ni hivi ategemee kupata kura za wanavijiji hasa wale wasio jua kinacho endelea katika siasa za Tanzania
 
Niko Hapa Nje Ya Tembe Langu Nikijiandaa Kwenda Kuwafukuza Kwelea Kwelea Wasinimalizie Mtama Wangu!
Ninapoiwaza Changamoto Hii,Ninazi Waza Pia Changamoto Zingine Ambazo Wabunge Karibu Wote Zimewatoa Technical Knock Out(K.O)!
Si Kilimbah,si Mwigulu!
Mathalani Kuna Ahadi za Muda Mfupi Alizo Ziahaidi Madelu Ambazo Mpaka Sasa Zimemgalagaza!
Aliahidi Maji Kata ya Mtoa Ndani ya Miezi Miwili,Umeme Kata ya Mtekente Ndani ya Miezi Minne,Kumalizia Kipande cha Barabara ya Old Kiomboi na Kumalizia Barabara ya Shelui-Kidaru Miezi Akisha Apishwa,ila Mpaka Sasa Hatuoni Lolote!
Madelu,Barabara ya Tulya-Kiomboi Kupitia Juu ya Mlima Sekekenke,ni Mbovu na Laiti Kama Ingeboreshwa,Tungeokoa Maisha ya Wagonjwa Wengi Wanaotokea Mingela,Misri,Bambaraga,Yombo,Mesi,Doromoni,Migilango Shauritanga na Mauguru!Wangewaishwa Kupata Huduma Tofauti na Sasa,Ebu Rudi Uichonge Upya!
Madelu,Jesica Kishoka Mwanamke Mwenye Sumu Kali,Analiwinda Jimbo la Iramba Na Sumu Anayo Wadunga Vijana ni Kali na Haiwezi Kuwa Neutralized!
Rudi,Vijana Wako Wamekosa Hoja Mbele ya Wana CHADEMA"
Rudi na Ukae Na Sio Kama Majuzi Ulipo Tuchungulia Katika Kikao cha Kamati ya Kudumu ya Fedha na Mipango!
Rudi na Umkumbuke Kijana Wako Imma Mapikiki na Siye Wote Kama Ulivyo fanya 2010!
Najua Umeme Ushakupiga Toba Baada ya M.C.C2 Kukupiga Chenga ya Mwili na Hata Ahadi ya Kujenga Kiwanda cha Kukamua Mafuta ya Alizeti Hapa Kata ya Tulya Ishakufa Kibudu!
Ubunge Kwanza Uwaziri Baadae!
Jamani Acha Niwawahi Kwelea Kwelea Wasije Nitenda!
Karibuni Kiporo cha Nyama ya Punda na Magae Makanta!
Hili la mwisho liseme pole pole, kwako wewe ni kitoweo ila una kula pingu ndugu yangu nyara za nchi hizo,na utaulizwa ilipo ngozi ni balaa.
 
pole mtumishi,vipi aliwaambia nini?sie alituambia atatujengea kiwanda cha kukamua alizeti hapa kata ya tulya,vipi nyie aliwaahidi nini?
Pengine hivi sasa yuko busy sana sana,ila nina imani muda mfupi kabla ya uchaguzi ujao atakuja na fulana,vitenge na bendera yake shingoni kuwa tekelezea wala msiwe na hofu.
 
Pengine hivi sasa yuko busy sana sana,ila nina imani muda mfupi kabla ya uchaguzi ujao atakuja na fulana,vitenge na bendera yake shingoni kuwa tekelezea wala msiwe na hofu.
Ndivyo ilivyo hata mkulima mmoja walaji ni wengi.
ahahaha,poa mkuu,mziga wa asal mmojai,mlina asali,walaji weni
 
Si mulisema mbele kwa mbele funga mkanda tu jamaa angu siku zote utavuna ulichokipanda

#ccm ni Ile ile#
 
Duu umenikumbusha mbali magae bwane, umesahau na mapama, hayo ya uchaguzi siwezi kukupa pole wala kukuhurumia sababu huwa mnalalamika ikifika uchaguzi nyie ndio wa kwanza kumchagua baada yakupata matundu na ntila za CCM, si alikamatwa anatoa rushwa mkamtetea? Mtalalamika sana, hebu nambie aache wakulima na wafugaji wanauana aje kwenu Ati awaletee umeme!! Kwani mafuta hakuna,? Tumieni vibari na 2020 mpeni tena maana mtaanza kumuona 2019 akija kuwasalimia nyumba hadi nyumba na kuacha kitu kidogo, nimesema sikupi pole wewe na wenzio
 
Kama Wanyiramba wote wangekuwa werevu kama wewe (Iramba), matembe yangebaki kuwa historia mkoani Singida. Ila, mh! Ni wachache ndo wanajitambua.
Moja ya wasomi wengi wa kwanza Tanzania wanyiramba wapo wengi mno ila wamejazana dar kwenye maofis makubwa... Ila hawatak kupambana kuelimisha jamii iliyobaki kijijini
 
Wanyiramba ni watu wakarimu sana tu na wenye misimamo thabiti kama wa Pemba wanapotetea haki yao, tatizo lao kubwa walilozaliwa nalo tofauti na waPemba ni kwamba hawawezi kukwepa mtego mdogo sana wa " Nama ne Ntulu/Magae" mnyiramba asilia hata kama ulimuua mtoto wake ukimpa nyama na pombe basi atakusamehe mara mia na mtaanza maisha upya
 
Back
Top Bottom