DON YRN
JF-Expert Member
- Jan 14, 2019
- 474
- 999
Pale Buguruni darajani kuna mchezo unaofanyika ni hatari sana kwa maisha ya watu kuliko maelezo.
Kuna siku kadhaa nimekuwa nikishuhudia vijana wako pale Buguruni darajani wakifungua koki za malori ya mafuta na kujaza kwenye mifuko ya nylon kwa kushirikiana na madereva.
Iko hivi; Lori la mafuta likifika pale darajani(njia ya kutokea Ubungo kwenda mjini) likiwa linasubiri foleni ya mataa, kuna vijana huwa wanatokea na kufungua koki ya tank kisha hukinga na kujaza mafuta kwenye mifuko ya nylon kwa ruhusa ya dereva kisha baada ya mataa kuruhusu mchezo unaisha, linasubiriwa lori la mafuta litakalosimama usawa wa daraja. Na hali hii huendelea hadi siku inaisha.
Cha kusikitisha ni kwamba huu mchezo unafanyika kwenye foleni ya magari mengi zikiwemo daladala za abiria, magari binafsi, n.k. Je!, yakitokea km yale ya Morogoro tutalaumu nani km tunashindwa kuchukua hatua na tahadhari mapema?.
Mbaya zaidi, Polisi na viongozi mbalimbali wanaona mchezo huu ukiwa unafanyika.
Anyway, naamini mm siyo wa kwanza kuona hili jambo kwa watu wote tuliomo humu.