Ipo siku, hili bus litaua watu kwa kweli!

Habari zenu mabibi na mabwana. Natumai mu wazima wa afya.

Nimeamua kuja mbele yenu nikifofia usalama abiria wanaopanda mara nyingi hili bus linalo fahamika kwa jina la SIJALI.

Kila asubuhi naliona hili bus likiondoka kwa mwendo wa kasi bila kujali sheria za usalama barabarani, huku abiria wanao keti siti za mbele wakishangilia kwa nguvu na kumpa mizuka dereva yakuongeza kasi. Na dereva huyu anafahamika kwa jina la Mpambalyoto, huwa hasikilizi abilia wanyuma wanao lalamika kuwa dereva ana unja sheria.

Nilipojaribu kumsogelea askari wa usalama barabarani nakumuuliza kulikoni, mbona huyu dereva anavunja sheria? Akijibu hata yeye hafahamu ni kwanini, kwani dereva Mpambalyoto amekuwa ni mwalimu wa madereva kuwafundisha wenzake wazingatie sheria za usalama barabarani, lakini alipopewa hilo bus tu, amekuwa wa kwanza kuzivunja.

Ukitazama kwa nje, hilo bus ni kuu kuu hivi, matairi yake yanavipara lakini bwana Mpambalyoto analiondoa kwa kasi ya ajabu hasikii ya mtu. Lakini siku za hivi karibuni naona hata wale abiria wa mbele wameacha kumtia mizuka dereva, wanaona hali ya hatari mbele yao, akili imewajia. Abiria wa nyuma wamejawa hofu ya kukata tamaa na maisha yao.

Na mbaya zaidi barabara lenyewe ni mabonde na makorongo tupu........sijui safari hii kama tutafika salama.
 
Nawashauri traffic watumie kile kifaa cha kupima pombe maana jamaa anapenda pombe mpaka wamempa jina la utani alcoholic
 
Abiria wameongea sasa wamefika mahali wamemwachia dereva afanye atakavyo,kila mtu anaomba kile anachofikiri kunusuru roho yake,maana hawanauhakika wa kufika huko waendako,Bus lenyewe limeshapoteza njia kila mtu hajui litaenda kuangukia wapi,!!!!!!
 
Angalau ile jf yamiaka ile imeanza kurudi. Hakuna aliye juu kuhusu ujuaji. Kila mmoja anamapungufu yake ila kwa dereva mpambalyoto au pogba wao wamefuzu sehemu zote ilhali kuna wa nyuma yao wako vizuri zaidi
 
Habari zenu mabibi na mabwana. Natumai mu wazima wa afya.

Nimeamua kuja mbele yenu nikifofia usalama abiria wanaopanda mara nyingi hili bus linalo fahamika kwa jina la SIJALI.

Kila asubuhi naliona hili bus likiondoka kwa mwendo wa kasi bila kujali sheria za usalama barabarani, huku abiria wanao keti siti za mbele wakishangilia kwa nguvu na kumpa mizuka dereva yakuongeza kasi. Na dereva huyu anafahamika kwa jina la Mpambalyoto, huwa hasikilizi abilia wanyuma wanao lalamika kuwa dereva ana unja sheria.

Nilipojaribu kumsogelea askari wa usalama barabarani nakumuuliza kulikoni, mbona huyu dereva anavunja sheria? Akijibu hata yeye hafahamu ni kwanini, kwani dereva Mpambalyoto amekuwa ni mwalimu wa madereva kuwafundisha wenzake wazingatie sheria za usalama barabarani, lakini alipopewa hilo bus tu, amekuwa wa kwanza kuzivunja.

Ukitazama kwa nje, hilo bus ni kuu kuu hivi, matairi yake yanavipara lakini bwana Mpambalyoto analiondoa kwa kasi ya ajabu hasikii ya mtu. Lakini siku za hivi karibuni naona hata wale abiria wa mbele wameacha kumtia mizuka dereva, wanaona hali ya hatari mbele yao, akili imewajia. Abiria wa nyuma wamejawa hofu ya kukata tamaa na maisha yao.
Teh teh teh teh
 
Mpambalyoto keshasema tatizo sio spidi zake, tatizo ni hiki kipande cha barabara...huko mbeleni kuna lami, mambo yatakaa sawa. Hata wauza kimea mapato yatapanda kwa kuwa basi likifika kwenye lamii halitingishiki kwa hiyo watu wataanza tena kunywa kimea
 
Naomba uzidi kutuletea Habari zaidi kuhusu dereva wa basi Hilo....

OVA
 
Back
Top Bottom