Konda wa bodaboda
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 7,981
- 4,174
Hilo basi lipo kenya sehemu gani?
Na condakta amechwa kisongo alishikwa na tumbo la kuhara hawezi hata kunyanyuka inabidi jumatatu amuone Dr pale maeneo karibu na gymkana Arusha Uzunguni pana mtaalam ana msubiri!Habari zenu mabibi na mabwana. Natumai mu wazima wa afya.
Nimeamua kuja mbele yenu nikifofia usalama abiria wanaopanda mara nyingi hili bus linalo fahamika kwa jina la SIJALI.
Kila asubuhi naliona hili bus likiondoka kwa mwendo wa kasi bila kujali sheria za usalama barabarani, huku abiria wanao keti siti za mbele wakishangilia kwa nguvu na kumpa mizuka dereva yakuongeza kasi. Na dereva huyu anafahamika kwa jina la Mpambalyoto, huwa hasikilizi abilia wanyuma wanao lalamika kuwa dereva ana unja sheria.
Nilipojaribu kumsogelea askari wa usalama barabarani nakumuuliza kulikoni, mbona huyu dereva anavunja sheria? Akijibu hata yeye hafahamu ni kwanini, kwani dereva Mpambalyoto amekuwa ni mwalimu wa madereva kuwafundisha wenzake wazingatie sheria za usalama barabarani, lakini alipopewa hilo bus tu, amekuwa wa kwanza kuzivunja.
Ukitazama kwa nje, hilo bus ni kuu kuu hivi, matairi yake yanavipara lakini bwana Mpambalyoto analiondoa kwa kasi ya ajabu hasikii ya mtu. Lakini siku za hivi karibuni naona hata wale abiria wa mbele wameacha kumtia mizuka dereva, wanaona hali ya hatari mbele yao, akili imewajia. Abiria wa nyuma wamejawa hofu ya kukata tamaa na maisha yao.
Kumbe mlengwa wa hii post ni Juma pimbi magugumaji??? JPM?Mpambalyoto kumbe DJ hana hata leseni ya udereva, ndiyo maana ana-change gia angani, mbaya zaidi ni mkwepa kodi na ana madeni kila benki.
brake pads zimekwisha mkuu,na hapa tulipo tunashuka mlima kitonga.Kwa sasa ndani ya basi kuna harufu ya kitu kama kinaungua.
Kwani tayari umemuelewa huyo Mpambalyoto? Mkuu mie sijaona ndani hebu ninong'oneze.Mpambalyoto kumbe DJ hana hata leseni ya udereva, ndiyo maana ana-change gia angani, mbaya zaidi ni mkwepa kodi na ana madeni kila benki.