Ipi tafsiri sahihi ya madawa ya kulevya?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,343
38,502
Hivi madawa ya kulevya kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ni nini hasa. Na ni wakati gani mtu anaweza ama hawezi kuwa na umiliki wa madawa hayo? Maana kwa mfano kama mtu anatumia majani ya Bangi kama Mboga ama mbegu zake kama kiungo cha mboga, je akikamatwa itakuwa amekamatwa na madawa ya kulevya ama mboga?

Hao watu wanaokamatwa na "madawa ya kulevya" huwa wanakamatwa na aina moja ya madawa. Ama wanaotajwa kuhusika na biashara hiyo wanauza aina moja ya madawa na wakikamatwa kosa huwa sawa kwa wote? Yaani kwa mfano anayekamatwa na Heroine na anayekamatwa na Bangi wote kosa lao huwekwa kwenye daraja moja kisheria?
 
Hapa Iringa mirungi inatafunwa kama mboga na wala haina shida. Kumbe kwa maana hii madawa ya kulevya Tanzania yanaweza yasiwe ni madawa ya kulevya Kenya. Kenya Mirungi inalimwa na inauzwa kama mchicha sokoni!!
Tanzania kuna Waziri Mkuu Kenya hawana Waziri Mkuu,Kila nchi ina sheria zake
 
Tanzania kuna Waziri Mkuu Kenya hawana Waziri Mkuu,Kila nchi ina sheria zake
Elewa mantiki. Hoja hapa ni nini tafsiri kuhusu madawa ya kulevya na jee hayo madawa ya kulevya yana hadhi sawa mbele ya sheria?
 
Hata ukichukua cocaine ukaiweka kwenye kopo la kahawa waweza sema ni kahawa nyeupe. Tatizo ni jinsi ya kutumia, je kuna mtu anajidunga kahawa kwa bomba la sindano ?

Na washawasha!
 
Mkuu hii issue uliyogusia ni muhimu sana.

Wananchi wanatakiwa wafahamishwe makundi ya dawa za kulevya na aina zinazokatazwa.

Maana hata pombe ni drug na inalewesha, nayo ni madawa ya kulevya vile vile.
 
Hata gundi yaan patex ni madawa ukivuta unalewa kuliko.je nayenyewe nayo inahusika?
 
Kama bangi ni madawa ya kulevya, basi usisahau kuitaja na pombe!
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania bangi iko kwenye kundi la madawa ya kulevya while pombe(ukiondoa gongo) sio madawa ya kulevya,kumbuka pombe mfumo wake wa utengenezwaji unathibitishwa na TFDA na TBS na pia watengenezaji wa pombe wanalipa kodi ambayo ni chanzo kikuu cha mapato ya serikali
 
Elewa mantiki. Hoja hapa ni nini tafsiri kuhusu madawa ya kulevya na jee hayo madawa ya kulevya yana hadhi sawa mbele ya sheria?
Bangi iko kundi la madawa ya kulevya,hadhi mbele ya sheria inategemea na kiasi ambacho utakutwa/kamatwa nacho
 
Hata ukichukua cocaine ukaiweka kwenye kopo la kahawa waweza sema ni kahawa nyeupe. Tatizo ni jinsi ya kutumia, je kuna mtu anajidunga kahawa kwa bomba la sindano ?

Na washawasha!
Kuna madawa unaweza kutumia kwa recomendation ya daktari hapo unakuwa hujafanya kosa.Kuna madawa ya kulevya yanatumika kutengenezea dawa ambazo zinatumika kwenye hospitali kwa matibabu ya wagonjwa
 
Tuna ufinyu wa maneno katika Kiswahili ndiyo maana vitu vinachanganywa na kurundikwa bila mpangilio.
Kwa Kiingereza neno "narcotics" linajumuisha kila kitu kinacholevya ikiwemo bangi, pombe, mirungi, cocaine, heroine na mengineyo yote.
Lakini sasa unapotaka kuvitenganisha hivi vilevya ndiyo sasa unakuta "cocaine, heroine, crystal meth" na vinginevyo vyenye asili au muonekano wa vidonge au ungaunga ambavyo vinaitwa "drugs".
Wasiwasi wangu ni kwamba kwa lugha yetu hii yenye udhaifu waasisi wa jina "madawa ya kulevya" walimaanisha hayo yenye muonekano wa vidonge au ungaunga ingawa kwa sasa wanalazimisha kupanua wigo wa maana ya jina hili ili aidha kila kilevya kiwemo kwenye kapu moja au ili iwe rahisi kumshitaki mtu kwa kosa la jumla jumla kama ambavyo tumeshuhudia kwa Wema Sepetu.
Binafsi naamini tunahitaji tafsiri ya Kiswahili ya neno "narcotics" lakini kutumia jina "madawa ya kulevya" kumaanisha kila kilevya tunapotosha maana.
 
Kwa mujibu wa sheria ya Tanzania bangi iko kwenye kundi la madawa ya kulevya while pombe(ukiondoa gongo) sio madawa ya kulevya,kumbuka pombe mfumo wake wa utengenezwaji unathibitishwa na TFDA na TBS na pia watengenezaji wa pombe wanalipa kodi ambayo ni chanzo kikuu cha mapato ya serikali
Kwa hiyo maana yako, ina maana kuwa as long as gongo na pombe nyingine ambazo hazijathibitishwa na TFDA na TBS,basi hizo ni dawa za kulevya.
 
Back
Top Bottom