Bangi ni dawa ya kulevya. Na mara kadhaa watu wamekamatwa kwa kukutwa na bangi nchini. Ila ni dhahiri serikali haijatilia maanani kutekeleza sheria dhidi ya bangi na ndiyo maana imefika mahali bangi imeonekana kama siyo dawa ya kulevya kama dawa za kulevya zingine. Hatahivyo, kitabibu madhara ya bangi ni kidogo ukilinganisha na dawa nyingine za kulevya kama heroine na cocaine.
Dawa nyingine za kulevya ni opioids ambazo zinatumika mahospitalini kupunguza maumivu makali kama maumivu ya mwanamke kujifungua, au maumivu ya kung'oa jino, au kama sehemu ya matibabu ya cancer. Hapa nchini haifahamiki sana kwamba opioids zinatumika kwa mtu aliyeng'oa gego, lakini nchi zilizoendelea kama USA ni kawaida sana kwa mama anayejifungua au mtu anayeng'oa jino kupewa hizi dawa. Kwenye maduka ya madawa zinatambulika kama Oxycontin, Oxycodone, Percocet etc.
Kwa kifupi, hizi dawa za kulevya nyingi zina matumizi halali mahospitalini, tatizo ni pale zinapotumika nje ya ushauri wa daktari, kwa dozi kubwa zaidi, na kwa muda mrefu kwa malengo ya kujiburudisha kama mtu anavyovuta sigara au kunywa pombe kama sehemu ya burudani ya mwili. Hapo ndipo effect ya madawa ya kulevya inapoanzia.