Ipi ni thread bomba MMU kwa mwaka 2011?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Tunapoelekea mwishoni mwa mwaka huu wa 2011 ni lazima tufanye tafakari ya yaliyojiri kwenye mwaka huu. Kwangu mimi kama kuna thread bomba ndani ya MMU basi ni hii iliyoanzishwa na Finest, "What made you Stay." Wewe ya kwako uliyoona ni bomba kwa mwaka 2011 ni ipi?

domestic-violence.jpg

Hiki ni kisa cha kweli cha rafiki yangu ila jina la muhusika ndio nimelibadilisha. Naandika kwa masikitiko sana kwa jinsi hali aliyonayo sasa hivi inasikitisha sana nafikiria ila kichwani mwangu maswali ndio mengi kuliko majibu, najiuliza ni kwanini lakini??

Ukimuona Angela sio yeye ile hali ya uanamke haipo tena, nguo anazovaa yeye ni zile zinazofunika mwili kuanzia juu hadi chini. Angela is not confident anymore anaonekana kama vile ana miaka 40. Angela amekuwa kwenye abusive relationship kwa muda mrefu amekuwa akipigwa na mumewe mara kwa mara na kumfukuza nje ya nyumba kwa kuwa ana watoto na huyu mume Angela ilikuwa inambidi arudi kwa mumewe kumuomba msamaha hii yote alikuwa anafanya kwa ajili ya watoto wake, alikuwa anataka watoto wake wamalize shule kabla hajachukua uamuzi mwingine.

Mumewe alikuwa ameishajua udhaifu wake uko wapi na ndio akaamua kuwa anatumia nafasi hiyo kumdhalilisha, Angela naye aliendelea kuishi na hali hiyo akitegemea iko siku labda mambo yatabadilika, ila siku mambo yalipokuwa magumu ndipo aliamua kuchukua uamuzi wa kuondoka hii ni baada ya mumewe kumjeruhi kwa kisu na mpaka sasa Angela ana makovu ya visu mwilini, natamani laiti kama mngeweza kumuona jinsi alivyo sasa hivi inasikitisha sana swali nililomuuliza ni kuwa pamoja na haya yote kwanini aliendelea kukaa kwenye ndoa ya namna hiyo akanijibu ni kwasababu ya watoto.

Nashindwa kueleza mambo mengine zaidi sababu ni ya aibu na ya kusikitisha sana mwanaume ambaye umezaa naye watoto leo hii anakuuliza "Kama wewe ni mwanamke kweli basi nionyeshe huo uanamke wako uko sehemu gani"? hivi sielewi.

NB: Mume wake ameishafikishwa kwenye vyombo vya kisheria kwa kosa la kumjeruhi

Najua ni wengi sana wako katika hali kama hii lakini hawasemi kwa kuhofia wakiacha ndoa zao jamii itawaelewa vibaya, ni kitu gani kinachokufanya uendelee kukaa kwenye ndoa ya namna hiyo????
 
Mh!Ngoja nifukunyue halafu nije nikiwa na kitu mkononi!
 
Kwangu Mimi thread ninazo zikumbuka sasa hivi ni hizi hapa (Sio MMU peke yake, sorry):

This meant a great deal to me... I waas very touched by such solicitude from JF members na mlinisaidia sana, hamjui tu.

Hii nimeipenda sababu watu walichangia na kubishana kwa heshima na adabu. Pia ilinisaidia kubadili mtazamo wangu kuhusu ndoa. Sio ndoa yangu lakini. Baada ya thread hii, na jibu lake, ilibidi nikubali kua kuna watu wengi wanacheat sababu wanapenda na pia wengine wanacheat sababu wake zao hawaoni ubaaya. So next time I speak for 'women' nitakua nakumbuka kua wanawake tuko tofauti na kitu mimi naona 'unacceptable and cause of divorce' wengine wanaona sio mbaya kiivo for as long as she is sure to be loved.

This one haina maelezo, bado ipo fresh in our memories, I had so much fun. lol

Hii niliipenda sababu sio kila siku mkuu anakuja kujadili na sisi live jamvini. Ila kuna mtu alinifurahisha sana, eti katika mada serious kama hiyo akamuuliza mkuu kama mkuu kaoa. JF kiboko haki. lol

Hii nimeipenda sababu watu walifunguka (for personal reasons sikushiriki). Big up Lizzy, it is rare that you start a thread that doesn't touch me.

I loved this thread. The ideas of members, the respect of different opinions, the variety of approaches... and I made some friends in the process... Nilijitoa mapema kidogo katika discussion lakini it doesn't mean I waas not following.

That is it kwa sasa, nikikumbuka zingine I will be back. Of course kuna zingine ila either sizikumbuki or sitaki kuzitaja hapa. :)
 
1. Jf udaku by Tanmo ilinichekesha sana, nikagundua hata watu wawe siriaz kiasi gani bandama zao bado zinafanya kazi na kila mtu anauchizi wa muda.

2. Tofauti ya wanamme na wavulana by the boss, imenipa ufahamu wa jambo lilikuwa linanichanganya sana kwa muda mrefu

3. Thread ya kufungia mwaka MMU by Bishanga
hapa nilifurahi kuongelea mambo mbalimbali bila kukunja sura kwenye keyboard yangu wala sikutumia akili zaidi ya silika

Na urudi kweli.
 
Kwangu Mimi thread ninazo zikumbuka sasa hivi ni hizi hapa (Sio MMU peke yake, sorry):

This meant a great deal to me... I waas very touched by such solicitude from JF members na mlinisaidia sana, hamjui tu.

Hii nimeipenda sababu watu walichangia na kubishana kwa heshima na adabu. Pia ilinisaidia kubadili mtazamo wangu kuhusu ndoa. Sio ndoa yangu lakini. Baada ya thread hii, na jibu lake, ilibidi nikubali kua kuna watu wengi wanacheat sababu wanapenda na pia wengine wanacheat sababu wake zao hawaoni ubaaya. So next time I speak for 'women' nitakua nakumbuka kua wanawake tuko tofauti na kitu mimi naona 'unacceptable and cause of divorce' wengine wanaona sio mbaya kiivo for as long as she is sure to be loved.

This one haina maelezo, bado ipo fresh in our memories, I had so much fun. lol

Hii niliipenda sababu sio kila siku mkuu anakuja kujadili na sisi live jamvini. Ila kuna mtu alinifurahisha sana, eti katika mada serious kama hiyo akamuuliza mkuu kama mkuu kaoa. JF kiboko haki. lol

Hii nimeipenda sababu watu walifunguka (for personal reasons sikushiriki). Big up Lizzy, it is rare that you start a thread that doesn't touch me.

I loved this thread. The ideas of members, the respect of different opinions, the variety of approaches... and I made some friends in the process... Nilijitoa mapema kidogo katika discussion lakini it doesn't mean I waas not following.

That is it kwa sasa, nikikumbuka zingine I will be back. Of course kuna zingine ila either sizikumbuki or sitaki kuzitaja hapa. :)

ahsante mamie kuna thread kama NANI ya lizzy nilikua sijapata kuiona ndo nimetoka kuichek nw
 
Back
Top Bottom