Ipi ni Hatarishi kati ya kauli ya NDUGAI na kauli ya TULIA?

Wanabodi habari!

Naenda kwenye mada yangu moja kwa moja!

NDUGAI yeye alitahadharisha umma au watawala juu ya madhara ya Serikali kukopa fedha toka taasisi mbalimbali Duniani.

Kwamba tukiendelea kwa spidi ile basi huenda nchi ikaja kuuzwa baada ya kushindwa kulipa,baada ya kujitumbukiza kwenye mlolongo wa mikopo bila tahadhali,huku tukifurahia mikopo hiyo kwa sasa!

Ilikuwa ni Angalizo zuri na lenye Point kabisaa.

Lakini kwa sababu ya siasa za ajabu za nchi hii....visasi,vinyongo na kukomoana.

Wale waliokuwa na chuki binafsi na Ndugai walifanya yao na hatimae Ndugai akaonekana mbaya wa Taifa.

Leo imekuwa zamu ya Tulia Akson mrithi wa kiti cha uspika wa bunge la JMT.

Kuna clip imetoka inayomuonyesha akiwahamasisha vijana wa UVCCM kwamba wale sahani moja ( sijui kwa namna ipi au mbinu zipi).

Kwamba wale wote wanaomsema vibaya Mama Samia Rais wa JMT.

Haijulikani ni wanaomsema vibaya Rais wa nchi ni wapi? na maneno yapi?
ndio mabaya na yapi ndio mazuri kwake.

Pia haijulikani yeye Tulia anawataka wale nao sahani moja kwa mtindo gani?

My Take:

Kama Ndugai aliwajibishwa na Rais kwa kulazimishwa kujiuzuLu Kwa kutoa tahadhari kwa nchi dhidi ya mikopo isiyo na muelekeo sahihi.

Je, Tulia ambae anahamasisha uvunjifu wa Amani baina ya watanzania.
Kwamba yeyote anayemkosoa Rais wa nchi,awe CCM au Upinzani.jambo linaloweza kusababisha uvunjifu wa Amani na umwagikaji damu.

Yeye atafanywa nini?
Ni ipi kauli hatarishi kati ya "Tutauzwa wote" na hii ya "kuleni nao sahani moja"

Huu ni mtihani mwingine kwa CCM pamoja na mwenyekiti wao,wajitafakari na kuchukua hatua stahiki kama ilivyokuwa kwa Ndugai.

Ili jamii iweze kuwaamini,vinginevyo tutaamini kulikuwa na mpango rasmi wa kundi ndani ya CCM lilipanga kumfurusha Ndugai na kumuweka Tulia kwa maslahi yao binafsi na kwa kuwaza uraisi wa 2025 zaidi.
Sikiliza video ya Tulia mpaka mwisho utagundua una chuki hakumanisha mlichokisema alimanisha watafute njia sahihi ya kutoa taarifa katika sekta sahihi ili mambo yanyosemwa yafanyiwe kazi
 
sikia mkuu hii nchi ina wananchi takriban Million 50... na ambao hawajaelmika n weng zaidi unapotoa kauli km ile mbele ya watu tena bila maelez basi tegemea mrejesho wa maon tofaut tofauti

kauli km ile ya job unadh ingekuwa inaleta aman kipind ambacho nchi ipo kweny tahamaki km ya uchaguz.

ukweli ambao wengi hawapend kuhsukia kuwa watanzania tuna kitu chuki ndan yetu kila kitu tunapinga eti kisa ss ni wapinzani maisha hayaend hvy wakuu
Je!
Tangu alipoitoa mpaka leo kuna taharuki gani imetokea?

Kati ya Ndugai na Serikali nani amekuwa mkweli mpaka sasa?

Tozo ba ukataji fweza kwenye akaunti za watu wanazotunza Benki si ndio dalili za kulazimishwa kusaidia kulipa hayo madeni?
 
Sikiliza video ya Tulia mpaka mwisho utagundua una chuki hakumanisha mlichokisema alimanisha watafute njia sahihi ya kutoa taarifa katika sekta sahihi ili mambo yanyosemwa yafanyiwe kazi
Wewe nae ni walewale tu.

Hamna hata haya kwa watanzania.

Nini maana ya "nyookeni nae"
 
Je!
Tangu alipoitoa mpaka leo kuna taharuki gani imetokea?

Kati ya Ndugai na Serikali nani amekuwa mkweli mpaka sasa?

Tozo ba ukataji fweza kwenye akaunti za watu wanazotunza Benki si ndio dalili za kulazimishwa kusaidia kulipa hayo madeni?
Boss pitia reply yang ya kwanza acha kukza fuvu nimesem kaul zote ni hatar kutgmea na mda na watu husika wanaofkishiwa hz taarifa .... cjasem hz kauli zina zua taaruk kuna watz wangap hawajaelimika chief ...
 
Wanabodi habari!

Naenda kwenye mada yangu moja kwa moja!

NDUGAI yeye alitahadharisha umma au watawala juu ya madhara ya Serikali kukopa fedha toka taasisi mbalimbali Duniani.

Kwamba tukiendelea kwa spidi ile basi huenda nchi ikaja kuuzwa baada ya kushindwa kulipa,baada ya kujitumbukiza kwenye mlolongo wa mikopo bila tahadhali,huku tukifurahia mikopo hiyo kwa sasa!

Ilikuwa ni Angalizo zuri na lenye Point kabisaa.

Lakini kwa sababu ya siasa za ajabu za nchi hii....visasi,vinyongo na kukomoana.

Wale waliokuwa na chuki binafsi na Ndugai walifanya yao na hatimae Ndugai akaonekana mbaya wa Taifa.

Leo imekuwa zamu ya Tulia Akson mrithi wa kiti cha uspika wa bunge la JMT.

Kuna clip imetoka inayomuonyesha akiwahamasisha vijana wa UVCCM kwamba wale sahani moja ( sijui kwa namna ipi au mbinu zipi).

Kwamba wale wote wanaomsema vibaya Mama Samia Rais wa JMT.

Haijulikani ni wanaomsema vibaya Rais wa nchi ni wapi? na maneno yapi?
ndio mabaya na yapi ndio mazuri kwake.

Pia haijulikani yeye Tulia anawataka wale nao sahani moja kwa mtindo gani?

My Take:

Kama Ndugai aliwajibishwa na Rais kwa kulazimishwa kujiuzuLu Kwa kutoa tahadhari kwa nchi dhidi ya mikopo isiyo na muelekeo sahihi.

Je, Tulia ambae anahamasisha uvunjifu wa Amani baina ya watanzania.
Kwamba yeyote anayemkosoa Rais wa nchi,awe CCM au Upinzani.jambo linaloweza kusababisha uvunjifu wa Amani na umwagikaji damu.

Yeye atafanywa nini?
Ni ipi kauli hatarishi kati ya "Tutauzwa wote" na hii ya "kuleni nao sahani moja"

Huu ni mtihani mwingine kwa CCM pamoja na mwenyekiti wao,wajitafakari na kuchukua hatua stahiki kama ilivyokuwa kwa Ndugai.

Ili jamii iweze kuwaamini,vinginevyo tutaamini kulikuwa na mpango rasmi wa kundi ndani ya CCM lilipanga kumfurusha Ndugai na kumuweka Tulia kwa maslahi yao binafsi na kwa kuwaza uraisi wa 2025 zaidi.
Labda anapaogopa jimboni kwake bila ubabe anajua hapati kula nae kiti kimeishamnogea ahahaaa bora niendelee kuuza dafu mie
 
Tulia hawezi kuchukuluwa hatua yeyote kwa sababu amemsifu anayependa kusifiwa.Hii ni hatari kwa taifa na imejidhihirisha ubutu wa huu mhimili
 
Back
Top Bottom