Ni vigumu kuwaombea Viongozi wetu iwapo ratiba zao hazitolewi kwa Umma. Ndio utakuta Kanisani tunawaweka kwenye Kapu la Maombi ya Jumla!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,036
142,108
Hili nalisema kiimani Zaidi kwa Sababu Maombi siyo swala la Siasa au mizaha

Pale Anglikana kwa mfano kila Jumapili Litugia yao ina Vifungu Vya Maombezi na Moja ya kifungu hicho ni kumuombea Rais wa JMT na Wasaidizi wake.
Pale kwenye Wasaidizi wa Rais pamewekwa ( hasa......) ambapo mchungaji atamtaja kwa jina Kiongozi mwenye Uhitaji maalumu wakiwemo Wagonjwa na Walio Safarini

Sasa kama Ratiba za Viongozi hazijulikani basi anaombewa Rais na Mawaziri wanaoswali pale tu mfano St Albans watamtaja Mkuchika, Ndugai na Kabudi basi

Nitoe wito hasa kwa Dr Tulia PhD aliyeomba tuwe tunawaombea basi wasisahau kutujulisha mahitaji yao maalumu ya kuyaweka kwenye Maombi

Ahsanteni sana!
 
Back
Top Bottom