poposindege
JF-Expert Member
- Nov 22, 2010
- 456
- 175
Simu ya Iphone 7 imedaiwa kusababisha kuwaka kwa moto katika gari
moja huko nchini Australia.
Mmiliki wa simu hiyo Matt Jones anasema aliiacha simu yake katika gari
na kuelekea darasani na ndipo aliporudi na kuona moshi mzito ukitoka katika gari
na alipofungua mlango wa gari aligundua kuungua kwa vitu vilivyomo ndani ya gari.
Alikuta jozi ya suruali aliyoiacha ndani ya gari ikiwa imeshika moto na chini yake kulikuwa na simu ya iphone 7 ambayo nayo ilikuwa imeungua vibaya.
"Wakati naangalia nikaona simu ikiwa kama imeyeyuka. Hakuna shaka kwamba simu hii imekuwa chanzo cha moto", alisema Matt Jones.na kuongeza kuwa "Na hakukua na vitu vingine vyenye kusababisha moto zaidi ya simu"
Betri za lithium-ion zinaelezwa huweza kusabaisha mlipuko endapo zitagongwa au kupata joto kali. Kampuni ya Apple Inc wamekataa kutoa maoni yao kuhusiana na tukio hilo, na walibainisha kuwa watafanya uchunguzi wao wenyewe kilichosababisha kutokea mlipuko huo.
Kumbuka matukio ya ulipukaji wa simu yaliliripotiwa kutokea kwa Simu za Samsung Galaxy Note 7 kiasi cha kupelekea kampuni hiyo kusitisha utoaji wa simu hizo.
Link:
iPhone 7 пошел по стопам Galaxy Note 7? – Naked Science
NB: matukio ya ulipukaji ya iphone huko siku za nyuma
http://www.telegraph.co.uk/news/2016/08/02/exploding-iphone-leaves-man-with-third-degree burns/
http://www.smh.com.au/technology/mo...ns-after-iphone-exploded-20160801-gqirdx.html
Briton Burned After iPhone Explodes In Pocket