Kampuni ya Viber Media Inc amabayo imekuwa ikitoa huduma ya kupiga simu na kutuma au kupokea ujumbe mfupi wa maandishi kwa kutumia application yao ya Viber sasa wamepiga hatua na kuamua kuzindua application hiyo kwa watumiaji wa Windows na Mac.
Watumiaji wa computer za Windows na Mac wataweza kupiga simu, kutuma au kupokea ujumbe mfupi wa maandishi kwenda au kutoka kwa mtumiaji yoyote wa Viber duniani kote.
Ili uweze kutumia Viber kwenye Windows au Mac unachotakiwa kufanya ni kutembelea
Viber - Free calls, Free text messages, photo and location sharing na kudownload application hiyo na kisha kuinstall kwenye PC yako.
Ukisha install utatakiwa kuingiza namba yako ya simu ambayo ulikuwa ukiitumia kwenye application ya Viber ambayo tayari umekwisha install kwenye simu yako.
Baada ya kuingiza namba yako ya simu kwenye application yako ya Viber ya Windows au Mac utatumiwa activation code kwenye application yako ya Viber iliyokwisha kuwa installed kwenye simu yako.
Baada ya hapo utatakiwa kuingiza code hizo ulizotumiwa kwenye application yako ya Viber ya Mac au Windows na u-click on activate. Baada ya hapo PC yako itakuwa imeunganishwa na application ya Viber.
Furahi kupiga au kupokea simu na kutuma au kupokea sms duniani kote ukiwa Viber.