bukoba boy
JF-Expert Member
- Jan 15, 2015
- 5,370
- 3,956
Ule mpango wa binadamu wa kuweza kuishi nje ya sayari yake asili unaonekana uko mbioni kukamilika.
Kampuni binafsi ya Space X inayojihusisha na masuala ya anga(ambayo kwa sasa ina tender ya kupeleka mizigo kituo cha anga cha kimataifa) imepania kupeleka watu Mars ndani ya miaka 6 na baada ya miaka 50-100 tayari watakua wameanzisha mji(self sustainable city) katika sayari hiyo.
Safari ya kwenda Mars imepangwa igharimu kiasi cha $200,000 kwa mtu mmoja.Waliulizwa mbona na hela kidogo sana mtawezaje kufanya kitu kikubwa hivo?
Jibu lao liko katika mfumo wao wa roketi(ITS) ambayo inaweza kutumika zaidi ya mara moja tofauti na zile za NASA zinatumika mara moja tu kwa matumizi maalum.
ITS ina hatua mbili,hatua ya kwanza mashine nzima(Spaceship na Booster) inawashwa injini zikiwa 47 zinazotumia Methane zinapaa mpaka orbit ya dunia,Booster inajitenganisha na spaceship[inabaki inaelea angani] then inarudi duniani(Booster) inawekewa kichwa kingine(propellant) kilichojaa mafuta inarudi mpak orbit inajaza tank ya spaceship iliyokua inaelea orbit. Hatua ya pili inaanza kwa spaceship iliyojazwa mafuta kuanza safari yake ya miezi 6 kuelekea sayari ya Mars.
Safari ya Mars itakua inafanyika kila baada ya miezi 26 ili kuivizia sayari ya mars ikiwa karibu na dunia katika harakati zao za kuzunguka jua
Kwa nini iwe Mars na sio kwenda kua wakoloni wa mwezi?
Mars ina rasilimali nyingi ambazo pia zipo duniani.
Ina gravity ambayo ni theluthi ya gravity ya dunia
Siku yake ina masaa 24 na dakika 40
Ina atmosphere