Safari ya Mars na miale ya jua

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Moja wapo ya sayari iliyokuwa muhanga wa nyota Jua ni sayari jirani yetu Mars ambapo kwa muda mrefu sana imekuwa ikishambuliwa na miale ya jua na kusababisha kuwa kavu katika baadhi ya maeneo yake haswa maeneo ya equator.

Mojawapo ya sababu kuwa inayopelekea Mars kuwa muhanga ni kile kitendo cha kukosa anga hewa na kukosa magnetic field ambayo huwa kama kinga dhidi ya miale mikali ya jua na miale yote ya nyota zilizo mbali kabisa na dunia yetu (Cosmos radiation).

Anga hewa la Mars si kubwa sana kama ilivyokuwa anga hewa la duniani kwetu kitu kinachopelekea dunia kuhimili miale mbalimbali mikali kitu ambacho Mars inashindwa kwakuwa ina anga hewa dogo jembamba.

Tunasema anga hewa la sayari fulani ni dogo au jembamba na la sayari fulani ni kubwa na nene kwa maana ifuataayo;

~ Kuwa na wingi wa matabaka mbalimbali kuanzia kwenye uso wa gimba au sayari fulani hadi kutoka nje kabisa yaani kule kwenye outer space, kama sayari itakuwa na anga hewa nyingi zenye migandamizo ya aina mbalimbali ya hewa basi moja kwa moja tutasema sayari hiyo au gimba hilo lina tabaka la anga hewa nene au kubwa.

~ Na kama gimba au sayari litakuwa na uchache wa matabaka mbalimbali ya anga hewa kuanzia kwenye uso wake hadi kufikia nje kabisa ya gimba hilo basi tutasema kuwa sayari au gimba hilo lina tabaka la anga hewa lililo dogo.

~ Kukosekana kwa tabaka la anga hewa kubwa katika sayari ya Mars kumepelekea miale mingi ya jua kushambulia sayari hiyo na kupelekea kuwa kavu na kukosa hali ya kuwa na uwezo wa kuwezesha maisha yetu sisi.

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili
FB_IMG_1674761738779.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom