#COVID19 Internews, MPC yatoa elimu ya UVIKO 19 kwa wanahabari

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza wakiwa kwenye mkutano wa tathimini ya chanjo ya UVIKO 19 na Uhuru wa Kupata Taarifa ulioandaliwa na Taasisi ya Internews na kuratibiwa na MPC.

Waandishi wamehimizwa kuendelea kuandika habari chanya za kuelimisha wananchi ili kupata chanjo muhimu ikiwemo ya UVIKO 19.

Mgeni rasmi katika mafunzo hayo alikuwa ni Mganga mkuu wa mkoa wa Mwanza DKT. Thomas Rutachonzibwa.

DKT. Rutachunzibwa amesema mkoa wa Mwanza umevuka lengo la kitaifa la utoaji wa chanjo ya UVIKO 19 la asilimia 70 ifikapo Desemba mwaka huu.

Hata hivyo, mpaka kufikia Desemba mwaka huu, watu milioni 1.6 wamepata chanjo kamili ya UVIKO 19 sawa na asilimia 87 hatua ambayo alihimiza wanahabari hao kuendelea kuandika Habari za UVIKO.
IMG-20221018-WA0084.jpg
IMG-20221018-WA0076.jpg
IMG-20221018-WA0067.jpg
IMG-20221018-WA0064.jpg
 
Back
Top Bottom