Intelligence heredity: Je, uwezo wa akili hurithiwa?

Wakuu kama tulivyomsoma lifecoded kwenye maandiko yake huko juu anasisitiza Intelligence is inherited, kuna kitu kimenijia sasa hivi, inakuwaje binadamu wa zama hizi wanaakili sana kuliko babu zetu, kwa kuangali zama hizi kuna invertions nyingi kuliko zama za mababu, sijui ni tafiti nyingi zinaleta haya au sisi tunaakili sana kuliko babu zetu? Tizama hawakuwa na makomputer, sisi tunayo n.k, ni tabu zetu ndio zimetufanya tufungulie code zingine au mazingira au ni intelligence ya kizazi hiki kubwa kuliko ya kina babu. Na kwanini hatukurithi ujinga wao au kwanini hatukuendelea kuishi vilevile kama wao lakini tunabadirika na kuongeza manjonjo meengi.
 
Na je Size ya kichwa ina maanisha ubongo mkubwa? ukiachana na hydrocephalus, yanii kuna watu hawana hydrocephalus lakini vichwa vyao vikubwa, je hii inamanisha ubongo wao mkubwa, na hii inahusianaje na intelligence ya mtu, na vipi kwa wenye vichwa vidogo, ingawa sijui ipi ni normal head size associated to what brain size is normal.
please wenye kuelewa hili.
 

Inalithiwa
 
Ngoja nijaribu kukujibu kinagaubaga.
Size ya kichwa ina uhusiano na uwing wa neural networks, kwamba kadri kichwa kinavyozidi kuwa kikubwa, ndivyo kunavyozidi uwezekano wa neurons nyingi kutengenezezwa na kuwa more interrelated as per activities. Activities like information processing & impulse conduction depending on speed of respective neurons.
Note: siyo mtaalamu mbobezi wa masuala hayo ya ubongo na neurons, ila nimekujibu kwa kadri ya uelewa wangu mdog.
==================================
Kwa maelezo zaidi waweza soma hapo chini as one of referenced article. [emoji116]

Neuronal factors determining high intelligence
 
Hii shule uliyoitoa hapa Mkuu hata sisi wataalamu wa jukwaa la mambo ya kikubwa na siasani tumeelewa vizuri, yaani umesummarize elimu ya kitabu kizima ukaiweka katika meneno machache, na niseme hivi ili kuelewa unayozungumza katika uzi huu bado pia IQ kiasi flani inahitajika, ikiwa kuna mtu anaIQ chini ya hicho kiasi basi kamwe abadani daima dumu hatokaa kuelewa.. Knowledge ni issue ndogo sana, ndio maana huyu anaweza kuwa mtamu kwenye udereva yule akawamtamu kwenye uvuvi ila INTELLIGENCE hii baba mtu anazaliwa nayo hafundishwi..!!!! Yaani huwezi kwenda shule ukapachikwa INTELLIGENCE... Hii ipo katika "nasaba"...

Kama mtu Ana IQ ndogo ndo basi tena siyo bahati yake, ni sawa na kuzaliwa mfupi au mrefu huwezi kufanya maajabu yeyote labda wakafanyie "welding" ugoko.
 
welll said mkuu
 
Hapana mkuu,race ya sasa hivi ina Intelligence ndogo kuliko race ya zamani ,sema race ya sasa hivi imebe subjected kwenye Artificial Intelligence era ambayo imejaaa knowledge nyingi sana...

Inshort tupo kwenye knowledge transcendent zaidi na tunazaidiwa na mashine kuliko kutumia akili zaidi..

Ndo mana IQ trend imeshuka zaidi na knowledge trend inaongezeka zaidi...

Ukitaka kuamini fanya utafiti huo utakuja kutuambia...
 
Haya unayoyasema ni kweli kabisa, juzi nilikua na mshkaji wangu flani sehemu ikapita landcruiser mkonge katika kuisifia sifia ikaja hoja kwamba hii ni kati ya gari chache zinazotengenezwa kwa mkono wa binadamu kuhusika kwa kiasi kikubwa tofauti na gari zingine ambapo roboti anahusika zaidi, mwisho tukaangukia kwenye mjadala kati ya binadamu na mashine/roboti nani anaufanisi zaidi.
 
Hahaha! Unamaaanisha watu km akina Newton na wenzake au? I dont think so...asili yetu ni moja mazingira ndo yanakuwa tofauti.
 

Kitu kingine mkuu kinachotupa utofauti mkubwa na race ya zamani ni geneological construction ambayo imefanyiwa mabadiliko makubwa mno...

Race ambayo ilikuwa more intelligence ilizuiwa kuinterbreed ina kuruhusu intelligence flow Inheritance kwa kizazi au vizazi endelevu..

ukitaka kuamini hilo chunguza rangi na physical morphology ya magenius wa kale yani hawafanani na kizazi cha sasa hivi..

Ukitazama hata Mfumo wa mwili wao au ngozi au nywele ilikuwa ni selected race kabsa mkuu na hawakutakiwa ku Interbreed kabsaa na Lung'wecha wengine,na most of famous genius had'nt married at ol...
look at their morphology kwanza hapa chini..

Wa kwanza ni Newton huyo.


Mtazame Picaso mwenyewe hapo halafu utafute na sura za sasa hivi huko kwao kama wafanana...


Just look at their hairs and so on..very different na kizazi cha sasa hivi...


Sasa ukitaka kujua kuwa kuna utofauti mkubwa sana tazama group hili hapa chini la mandezi wa kizazi cha leo chenye IQ range ya 100 na kushuka..

Hapo ndo utajua Genetic reconstruction ilifanyika kwa gharama zote kuhakikisha Genetic make up ya IQ kubwa inabaki kuwa restricted na kuzuia flow yake ikiwa ni pamoja na kuwatengenezea mabadiliko ya kigenetic zaidi au kuwazuia kuinterbreed na wengine...

angalia kundi jingine la kindezi la leo hili hapa na ni wageruman pamoja na mataifa mengine lakini hawafanana na kundi la Wenye IQ kubwa


Njia pekee ya kuzuia Intelligence flow ya geneology husika ni kuzuia interbreed au kufanya genetic reconstruction kwa kupangua gene flow system kwenye DNA strand ya mtu husika kisha kumruhusu afanye interbreed..

kizazi cha sasa hivi ni reconstructed hybrid kabisa kupitia program kabambe ya GENETIC MODIFIED FOOD ambayo imebeba gene control za kutosha za kubadilisha mfumo wa Intelligence wa mwanadamu ,na hivyo vyakula vimejaa gene mbadala ambazo zinaleta mabadiliko kwa haraka zaidi...

Our body are subjected to construct sub-normal Intelligence range kupitia Artificial reconstructed genes kupitia genetic editing ya sasa hivi na ndo hichi kitu kilichobadilisha mfumo mzima mwilini wa Inheritance trend ya kila kitu..

It is genetic modification through gene where we can change the genetic make up also of our Inheretance pattern of any Traits and not the enveronment..

,mabadiliko haya ni ya kidunia ,no one to escape this mpaka tuwe complete replaced na Artificial Intelligence mashine ndo mpango wao unakamilika,.

Hii imeelezewa zaidi kwenye kitabu kipya cha Stephen Hawking cha A brief answe to the biggest Questions kwenye page yake ya Artificial Intelligence na hi halipingiki..

We are going to be totally replaced by the mashine katika kufikili zaidi na hapo ndo utaona msaada wa mwanadamu unashuka zaidi.
Watu wanaenda kuunda uhusiano mpya na new reconstructed beings ambazo zitakuwa na uwezo wa kubadilishana mawazo na wew kwa rate kubwa sana ambayo mwanadamu hatakuwa nayo,and its true ila hapo watu wanasema haitatokea but keep waiting the fantasy of genetic reconstructed ilivyotuharibu akili ..

Hizi IQ tulizonazo ni wazazi wetu waliobesubjected kwenye genetic make up reconstruction za miaka ya nyuma hapo ambayo haikuwa na Mazara makubwa sana kivile ila kadri muda unavyozidi kwenda genetic editing inafanyika kwa haraka sana ili kuua gene morphology original ...

Na ndo mana kwenye human clone jamaa wanaclone watu wa nyuma zaidi ambao Intelligence pattern yao ilikuwa tofauti na ya sasa hivi .

Wanavuruga kama sio kuinvet upya Intelligence gene bases kwenye ubongo kisha kuruhusu tuinterbreed huku matokeo yakiwa tofauti kabsa .

kama Gene arrangement ni AGG GGC wao wanainvert inakuwa ni CGG GGA kwenye upande wa Intelligence tu huku mabadiliko mengine yanabaki hivyo hivyo ili uendelee kufanana na baba yako huku uwezo wenu wa akili ukibadilika kwa kasi kubwa sana .

Only genetic editing can reconstruct the Inheritance pattern and not the enveronment as people tend to claim.

Genetic makeup changes kupitia abnormal reconstruction ya gene ndo italeta mabadiliko ya papo kwa papo na suo vinginevyo..
 

Attachments

  • Screenshot_20181117-084041~2.jpg
    27.8 KB · Views: 46
Fikirishi.
 
Wanazuia genetic flow kwa sababu zipi za msingi katika mustakabali wa maendeleo ya dunia?
Kama wakina Newton walileta mapinduzi makubwa ktk ulimwengu wa Sayansi na technology, kwa nini wasiachwe wa-interbreed ili kuruhusu passage of genetic flow to another generation kwa lengo la maintain maendeleo ya kisayansi na technolojia?

kizazi cha sasa hivi ni reconstructed hybrid kabisa kupitia program kabambe ya GENETIC MODIFIED FOOD ambayo imebeba gene control za kutosha za kubadilisha mfumo wa Intelligence wa mwanadamu,
Je, hathari za mbeleni kiafya za watu kuendelea kutumia GMP ni zipi?

kama Gene arrangement ni AGG GGC wao wanainvert inakuwa ni CGG GGA kwenye upande wa Intelligence tu huku mabadiliko mengine yanabaki hivyo hivyo ili uendelee kufanana na baba yako huku uwezo wenu wa akili ukibadilika kwa kasi kubwa sana.
Ni nani huyo mratibu wa masuala ya kubadili DNA coding?
Je, ni kwa faida ya ulimwengu mzima?
Je, ni kwa faida ya nchi chache au nchi moja tu?
Je; ni kwa faida ya kikundi cha watu?
Mwisho:
Kwa nini waamini machine ndizo mbadala wa kazi zote zifanyazwo na mwanadamu?
 
hapo sasa..[emoji4] [emoji4] you can find the answers at your own risk
 
[emoji16] [emoji16] [emoji16] yaani kwa my own risk, duh!!!!! [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125] something is still myth.
ujue nini mkuu..kuna mambo ukijitowa kumweleza mtu yapo atayapinga tu with no reasons ati [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] inafikia mahali kila mtu arisk maisha kivyake ..au wew unasemaje mkuu..??
 
Yawezekana....
 
ujue nini mkuu..kuna mambo ukijitowa kumweleza mtu yapo atayapinga tu with no reasons ati [emoji4] [emoji4] [emoji4] [emoji4] inafikia mahali kila mtu arisk maisha kivyake ..au wew unasemaje mkuu..??
Sawa nimekusoma mkuu.
"I wish one day I could be you" kwa kuwa inaonekana we ni zaidi ya encyclopedia.
[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji120] [emoji120] [emoji120]
 
Hahaha! Unamaaanisha watu km akina Newton na wenzake au? I dont think so...asili yetu ni moja mazingira ndo yanakuwa tofauti.
Nilichokuwa na maanisha ni kwamba, ikiwa intelligence in rithishwa/rithiwa genetically, mbona hatuwaoni kina Newton wa zama hizi?! Au genes zao zilikosa warithi au zilidumaa after some time, Na vipi ilikuwaje tukarithi kisichokuwepo, yani tuliorithi kwao hawakuwa na uwezo kutengeneza computer, iphone, satellite. Ndio maana nikauliza mbona naona hiyo theory inakinzana na hali halisi. Ni kwamba kizazi hiki tunaakili sana, kuliko tuliorithi kwao?! Lakini lifecoded lifecoded kajibu tayari.
Lakini why zama hizi hakuna kina archmedis, Newton, Galileo, na the like, genes zilidumaa au warithi waludumazwa na prevailing knowledge?! Na kwanini vyote visiende hand in hand?!
 
Hahaha sasa sijui ni mimi au wewe nachanganya/unachanganya.
Huko juu ulisema Gene inayohusika na intelligence haijulikani, na kama ingekuwa inajulikana kuna uwezekano in future wangeweza kubreed kizazi cha intelligent watupu, na hii ulisema haijawezekana, sasa wanawezaje kureconstruct kizazi kama intelligent gene haijulikani, yet!.
Je, unamaanisha hao kina Picaso na kina Newton walitengenezwa kama sample?! If not mbona unasema walizuiwa ku breed na ku interbreed?! Nani aliwazuia kuoa au kuzaa?! Inamaana kuna watu au kikundi/society ilikuwa inawa control wao na ilihakikusha hawaachi mbegu?! Mi ningedhani kizazi hicho ndicho kingeendelezwa badala ya kuwa limited?! Maana kilifanya maajabu na kupelekea kuwepo knowledge iliyopo leo.
Na inawezekanaje hizo GMO ziwe na uwezo kubadili genes za mtu aliyekwisha kuwa coded and wired to a core. Ulisema, ukiisha zaliwa na kuwa ulivyo huwezi kubadirika, maana kila mtu ana DNA zake unique. Maana intelligence genes hazijulikani sasa vipi uweze kubadili usichokijua, na unajuaje kimebadirika?! Maana kama wanafahamu intelligence gene, through IVF tungeona magenius kuliko kina Newton leo, au mimi ndio dish linayumba mkuu?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…