Intelijensia ya Rwanda sio ya mchezo mchezo, kinara wa Hotel Rwanda anashangaa kujikuta Kigali Airport

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Sep 10, 2017
10,561
19,056
Paul Rusesabina aliyekua Manager wa Hotel Rwanda akiwaokoa Watutsi wasivamiwe na kuchinjwa na Interahamwe hatimaye amefikishwa mbele ya sheria kwa makosa ya kuhusika na njama za mauji hayo hayo.

Baada ya filamu ya Hotel Rwanda kueleza kisa cha Rusesabina, wakati wote dunia ilimuona kama shujaa aliyesaidia kuokoa maisha ya makumi ya Watutsi wasio na hatia waliokimbilia Hotel Rwanda hadi pale uchunguzi ulipofanyika na kugundua naye alikua mmoja wa walioshiriki kutekeleza genocide ile. Suala kama ana hatia au la mahakama itaamua lakini kilichoacha watu midomo wazi ni namna alivyofikishwa Rwanda, maana alikua akiishi Ubelgiji na alishachukua urai wa huko.

Inasemekana alikua Dubai na alidanganywa kupanda ndege ambayo labda aliamini inaenda sehemu nyingine. Kuja kutahamaki anajikuta anashuka Kigali Airport na pingu zikimsubiri!. Kabda ya hapo kuna jamaa wa Kinyarwanda aliandika makala akisema alijipa jukumu la kufuatilia nyendo za Rusesabagina duniani kote na alifanya hivyo kwa miaka 15 na kwa kukamatwa kwa Paul Rusesabagina basi ametimiza kazi yake akiwa kama Mzalendo wa nchi yake! Maofisa wa Rwanda wanasema jamaa amerudi mwenyewe kwa hiyari yake jambo ambalo ndugu wanalikanusha wakidai kua ametekwa, na sababu ni kwamba alianza harakati za kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kuongoza kundi la FNL ambalo Kigali inasema ni lakigaidi.

Serikali ya rais PK kama alivyo yeye mwenyewe ina mkono mrefu na wanamsemo wao kua "There is a price to pay in betraying Rwanda" na kwamba hicho ndio kilichomkuta Paul Rusesabagina.
 
Mkuu Acha uongo basi, aliyeact kama Paul Rusesabagina ni Don Cheadle

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Uko sahihi kabisa Mkuu na niombe radhi kwa kukosea hapo. Hata hivyo Paul Rusesabagina ndio alikua Manager mwenyewe(halisi) wa ile Hotel, inawezakana nimekosea kupata facts kwamba aliyeigiza kama yeye ni Mmarekani lakini msingi wake ni kumuonyesha Rusesabagina kua alikua shujaa aliyewakoa Watutsi waliokimbilia hotelini kwake.
 
Mie ninachoshindwa kufahamu mpk sasa ilikuaje akapanda ndege hiyo, ni kwamba alitekwa? Au hiyo ndege ilisoma vingine mpk yeye akashawishika kupanda au alikodi private kumbe majasusi wa Kagame ndio wamiliki wakampeleka kwa Pilato
 
Lazima atakuwa alirudi kwa hiari,au rwanda walifanya kama saudi arabia inavyofanya,,yaani ndege inabadilishwa route na kutua rwanda,,,
Rwanda wakiamini mtu fulani anahatarisha usalama wa nchi yao basi ajue hayuko salama popote pale alipo duniani. Nakumbuka miaka ya 1980s Nigeria walijaribu kumteka aliyekua waziri wao wa mambo ya nje akakimbila Uk lakini issue ika backfire airport
 
Mie ninachoshindwa kufahamu mpk sasa ilikuaje akapanda ndege hiyo, ni kwamba alitekwa? Au hiyo ndege ilisoma vingine mpk yeye akashawishika kupanda au alikodi private kumbe majasusi wa Kagame ndio wamiliki wakampeleka kwa Pilato
Hii ime confuse watu wengi sana. Hata ndugu hawajui ilikuaje. Wanajua tu hakurudi kwa hiyari.
 
Hii ime confuse watu wengi sana. Hata ndugu hawajui ilikuaje. Wanajua tu hakurudi kwa hiyari.
Kama hujafuatilia story za maprince wa saud arabia wanaoishi ulaya jinsi wanavyotekwa na kurudishwa saud arabia utashangaa,
Pesa huwa haishindwi, wanakusoma tangu mwanzo mizunguko yako, siku wanajua labda unapanda ndege toka ubelgiji kuja uganda ama congo, ndege inatuishwa kigali, kuja kusituka uko kigali airport bafala ya entebbe au Kinshasa, baadae ndege inaondoka kuendelea na route yake baada ya wewe kuwekwa nguvuni.
 
Kama hujafuatilia story za maprince wa saud arabia wanaoishi ulaya jinsi wanavyotekwa na kurudishwa saud arabia utashangaa,
Pesa huwa haishindwi,,wanakusoma tangu mwanzo mizunguko yako,siku wanajua labda unapanda ndege toka ubelgiji kuja uganda ama congo,,ndege inatuishwa kigali,,kuja kusituka uko kigali airport bafala ya entebbe au kinshasa,,baadae ndege inaondoka kuendelea na route yake baada ya wewe kuwekwa nguvuni.
Dah! Kweli pesa mwanaharamu😀😀😀
 
Ahsante mkuu, hapa umeeleweka
 
Ni kweli nilichanganya Mkuu, lakini Paul Rusesabagina original ndio katiwa nguvuni sasa
Ni kweli mkuu Ila nashangaa wazungu wanambrand kama humanitarian activist
Screenshot_2020-09-13-10-21-22-924_com.google.android.googlequicksearchbox.jpg

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Ni kweli mkuu Ila nashangaa wazungu wanambrand kama humanitarian activistView attachment 1568374

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
Wazungu wakiamua kukunyanyua wanakupaisha tu. Hata hivyo kuna watu wanadai kwamba serikali ya Kigali ilanza kumuandama Rusesabagina baada ya kutangaza kumpinga na kutaka kumuondoa madarakani Rais Kagame kwa kutumia nguvu baada ya juhudi za kumuondoa kidemokrasia kushindikana
 
Back
Top Bottom