Betterhalf
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 2,882
- 2,565
Ulitoa maelezo mazuri ambayo yaloambatana na ulizo lako.Mdau amejitahidi kufafanua, nawe unakanusha na kufafanua vile ujuavyo wewe.Ndugu kwanza kabisa napenda nikwambie uko sawa na hauko sawa.INTELLIGENCE DUNIANI kote ni Strategic na sio random.Intelligence sio Jeshi la Polisi wala Sio mahakama na wala sio Jeshi la Ulinzi.Intelligence ni Strategic unit.Ndio maana ktk maelezo nimesisitiza swali Je hawa ni walinzi binafsi wa Rais kwa sbb kazi kubwa ya intelijensia ni kukusanya taarifa,kutambua tishio na kulizuia.
Nachukia pale watu wa intligence wanapohusishwa na mambo ya kihuni kama kutishia watu,kuteka na kujaribu kuua na hata kuua.Intelijensia haihitaji front page kwenye magazeti.Ndio maana wataalamu wa haya mambo husema kuwa Spies are people who walk at sidelines of history,not to be honoured or remembered.
Kama TISS wakiwa ni walinzi binafsi wa Mkuu wa nchi kuna hatari hasa kutokana na ukweli kwamba Rais mwenyewe aweza kuwa na Tishio hapo ndio kama taifa tunaona umuhimu wa kuwa na Taasisi huru ya Usalama wa Taifa ambayo haina maslahi ya kisiasa wala kiuchumi
Sijaelewa lengo lako, utupakulie unayoyajua ili tukujue kuwa wewe ndo wale na una-show off.
Au lengo lako upime uelewa WA watu ili uweze kuwakosoa?