FEBIANI BABUYA
JF-Expert Member
- Mar 5, 2022
- 2,229
- 4,345
- Thread starter
- #341
2000.Vipande vilivyobakia ni bei gan mkuu?
Vipande 59
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
2000.Vipande vilivyobakia ni bei gan mkuu?
Nope mfumo wa kulipa
Sisi wa jf tunaipata lin mkuu
Tupe siku muendelezo linSisi wa jf tunaipata lin mkuu
Mkuu kuwa na amani inaendelea, leo yenyewe tunasoma kama kawaida.Tupe siku muendelezo lin
Huyu kijana nadhani atakuwa ni jabir yule mdogo wake na Jason aliyeokotwa na Mr.Denilo FelixSTORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA SABINI NA NANE
SONGA NAYO................
Majira ya usiku huo wa mapema, baada ya Jason kuona ile taarifa ya kukamatwa na IGP tena mhusika mkuu akiwa ni CDF ambaye alikuwa kama baba mkubwa kwake, alitaka kwenda kukutana na mtoto wa kiongozi huyo ambaye alikuwa anajulikana kama Oden Mkupi Makubilo, alihitaji sana kujua uhusika wa Oden kwenye jambo jilo, alikumbuka vyema wale vijana ambao aliwaua kule Mbagala waliwahi kumwambia kwamba walikuwa wametumwa na Oden ili wakamchukue yeye na kama itashindikana kumchukua basi wahakikishe kwamba wanamuua moja kwa moja ili kusiwe na ushahidi wowote wa jambo ambalo lilikuwa limetokea maana ilionekana kama kijana huyo atakuja kuwa tatizo hapo mbeleni.
Nyumbani kwa Oden,
Jioni hiyo Oden akiwa na kijana wake alimuita na kumpatia maelekezo mafupi sana ambayo alitakiwa kuyafanyia kazi mapema.
"Kwa sasa mke wangu ni mjamzito na hilo ni jambo ambalo litanifanya niwe salama kwa upande wa baba maana nilikuwa nimechoka sana kelele zake lakini yule kijana hatakiwi kuishi tena anatakiwa kufa mara moja kwani kama hili jambo likija kujulikana basi nitaingia kwenye aibu ambayo sijawahi kuishuhudia kwenye maisha yangu" alimpa kijana wake maelekezo ambayo yalitakiwa kufanyiwa kazi haraka sana ili kumaliza hilo tatizo ambalo halikutakiwa kufika kwa watu wengi zaidi.
Mwanaume huyo alikuwa ana tatizo la nguvu za kiume na hivyo kumfanya yeye kutokuwa na uwezo wa kulala na mwanamke yeyote wala kuweza kutungisha mimba, hilo ni jambo ambalo lilimfanya yeye kuwa na roho ngumu ya kumruhusu mke wake kufanya mapenzi na mwanaume mwingine kila alipo hitaji tena mbele ya macho yake. Mwanamke huyo huenda alihisi mwanaume huyo anajali sana hisia zake ndiyo maana alikubali kumuacha afurahie na kijana mwingine ambaye yeye alimchagua, na hakumchagua tu huyo ni kijana bali alimpenda sana kutoka moyoni. Lakini mwanamke huyo kitu ambacho yeye hakukijua ni mwamba mwanaume huyo alikuwa anapitia wakati mgumu na maumivu makali sana kushuhudia mkewe anavuliwa nguo na kijana mwingonr tena mbeba vyuma wa mtaani tu.
Hayo maagizo aliyatoa akiwa anaweka msisitizo kwamba kijana huyo kazi yake ilikuwa imeishia hapo na alitakiwa kuuliwa ili maisha mengine yaendelee maana hakukuwa na namna ya kumuacha ili waendelee kuitunza hiyo siri yao bila kuacha hatua hata moja ambayo ingeleta mtafaruko. Ila kwa bahati mbaya sana wakati anaongea hayo maneno na huyo kijana wake mke wake alisikia vyema sana akiwa amejibanza kwenye kona ya ukuta, kitu ambacho kiliwashtua ni baada ya mwanamke huyo kudondosha chungu ambacho kilikuwa na maua wakati akiwa anatetemeka baada ya kusikia hilo jambo.
Kisu kidogo kilimkosa kwenye shingo baada ya kuinama akiwa analia sana mwanamke huyo
"Hey stop, unataka kumuua mke wangu?" Oden alimpiga jicho baya sana huyo mlinzi wake baadanya kurusha kisu ambacho kama mwanamke huyo asinge inama basi kilikuwa kinapita na shingo yake, kijana huyo alijua huenda ni mtu anawapeleleza ndiyo maana alihitaji kutoweka na maisha yake kiwepesi sana lakini alikuwa anataka kujiingiza kwenye matatizo mazito sana kama angemuua mke wa bosi wake ambaye alimpenda kuliko kitu chochote kile.
"Kijana amekukosea nini yule mpaka unataka kumuua?" Mwanamke huyo aliongea huku akiwa anampiga piga Oden kwenye kifua chake, mwanaume alimshika mkewe kwa nguvu na kutaka kumtuliza lakini je kweli angetulia kwa mtu ambaye alikuwa anampenda sana? Abadan! asingeweza.
"Au kwa sababu una pesa sana na baba yako ana mamlaka makubwa sana nchini ndiyo maana hauwezi kuijali furaha yangu? Nani atanifanya mimi niridhike? Nampenda yule mwana....." kabla hajaongea sana alipigwa kofi zito sana kwenye uso wake mpaka akajigonga ukutani.
"Unasemaje mpuuzi wewe? Unampenda yule kijana, hahahahaha hahahaha nadhani bado haujanijua wewe mwanamke, yaani nikuchukue chuoni huko ambako ulikuwa na maisha magumu leo unajijibu mimi jeuri na kuniambia bila uoga kwamba unampenda yule hayawani? Sasa leo ngoja nikupe somo la maisha, subiri huyo mpuuzi wako aletwe hapa halafu nimuue mbele yako mjinga mkubwa wewe na utanieleza vyema" Oden aliongea kwa hasira sana akiwa anamwangalia kijana wake kwa hasira sana, kijana huyo alielewa wajibu wake kwamba ulikuwa ni upi hivyo aliitoa simu yake mfukoni na kutuma sms upande wa pili.
"Nimewapa taarifa bosi waende wakamchukue hivyo siyo muda sana watakuwa naye hapa" kijana hiyo aliongea na kwenda kwenye friji, alitoa pombe kali sana na kumpatia bosi wake bilauri ili atulize moto kwanza wakati huo mkewe alikuwa amejikunyata chini akiwa analia sana.
Gym,
Eneo la mabibo mwisho palikuwa na gym ya kawaida tu ambayo walikuwa wanaenda watu wa hali ya chini sana kwa sababu bei yake ni bei ya nyanya kulipia hapo. Kwenye hiyo gym ndipo alipokuwa anapatikana kijana Ignas, huyu ndiye ambaye alikuwa anamridhisha kimapenzi mke wa Oden kwa malipo, haikuelewaleka walikutanaje mpaka yeye ndiye akaipata hiyo nafasi.
Kijana huyo alikuwa na kifua kipana na sura yake pana yenye weupe kiasi na mwili ambao ulijigawa kwa usahihi sana, alikuwa kijana wa mtaani ambaye alikuwa mkimya mno na hakuwa mtu wa kujichanganya sana na watu, alikuwa anaenda gym, anafanya zake mazoezi na kuondoka pasipo kuwa na stori nyingi sana na watu wengine na hayo ndiyo yalikuwa maisha yake ya kila siku. Hakuna ambaye alikuwa anayajua kiundani maisha ya kijana huyo kwani alikuwa anaonekana mara moja moja hapo gym kisha angepotea kwa muda halafu angerudi tena, na hakukuwa na mtu wa kumfuatilia kwa sababu mjini kila mtu anashika yale yaliyo yake pekee.
Siku hiyo aliingia gym mapema sana na kutoweka mapema ni kama alikuwa na hesabu zake kali mno. Simu yake muda wote ilikuwa ipo on, alikuwa yupo nayo makini isivyo kawaida na huenda alijua kwamba kuna mtu ambaye angemtafuta hakuwa na wasiwasi na hilo jambo. Sehemu ambayo alikuwa anaishi ni Mabibo Jeshini, huko alikuwa na chumba chake safi ambacho kilikuwa na kila kitu ndani yake, hakuwa kijana mnyonge sana bali alijitosheleza kwa maisha yake.
Baada ya kutoka zake gym qlienda mpaka sehemu aliyokuwa amepanga mapema, akavaa na kuondoka mpaka Loyola hapo alikaa maeneo ya barabarani pembeni akiwa hana hata tone la wasiwasi, mwili wake hakukuonyesha kuwa mtu mnyonge sana licha ya watu wengi kuhisi huenda ana mwili wa gym tu na hakuwa na lolote, hata Oden alimjua kijana huyo kwa namna hiyo ila je walikuwa sahihi? Hakuwa na papara mdomoni mwake alikuwa anatafuna karanga zake mbichi taratibu.
Majira hayo ya usiku ndio muda ambao mlinzi wa Oden aliwatumia ujumbe vijana wake waende kumchukua bwana mdogo huyo na kumpeleka kwa bosi kwa nguvu, tofauti na ziku zote ambapo kijana huyo alikuwa anafuatwa kwa gari na mlinzi mmoja tu na kwenda mpaka kwa bosi huyo kwa ajili ya kumridhisha mkewe ambaye kwa wakati huo alikuwa ni mjamzito. Wanaume hao walikuwa na gari yao ambayo walienda kuiacha karibu na maeneo ya KKT Mabibo, walikuwa ndani ya mavazi ya suti, kwa sababu mitaa ya Jeshini kidogo wanaishi watu ambao hawana unyonge sana wa maisha hususani watu wajivuni kutoka kaskazini magharibi mwa Tanzania basi kila aliye waona watu hao alijua basi walikuwa na ndugu yao huko ambaye ndiye walimfuata.
Wanaume hao walifika sehemu ambayo kijana huyo alikuwa anaishi, walishtushwa na hali waliyo kutana nayo hapo maana mlango ulikuwa wazi kabisa wa chumba chake na hiyo sehemu hakuwepo mtu mwingine yeyote yule, walikagua kila sehemu ila hawakumuona.
"Nadhani huyu mjinga alijua kwamba tutakuwepo hapa amekimbia" mmoja wa hao wanaume aliongea akiwa anairudishia bastola yake kiunoni.
"Hawezi kukimbia, kwani amejuaje kama sisi tutakuwepo hapa?" Mwanaume mwingine ambaye alikuwa na sauti nzito zaidi alitamka huku akiwa anakizima kipisi cha sigara ambacho kilikuwa kinakaribia kuisha.
"Sina jibu la moja kwa moja kuhusu hili, ila haiwezekani kwenye jiji kama hili ambalo wizi umeshamiri mtu akaacha mlango wake wazi halafu akawa hayupo, nadhani huu ni mtego kama siyo kufanya makusudi ili kutuonyesha kwamba alikuwa anajua kwamba sisi tungekuja hapa kwake" hayo maneno yaliwafungua watu hao inawalazimu wakubaliane kumtafuta kwa njia ya kuitraki simu yake kupitia namba waliyokuwa nayo.
Lilikuwa jambo la muda mfupi sana, namba hiyo hata haikuwa mbali sana kutoka sehemu ambayo walikuwepo, ilikuwa inaonekana karibu sana na shule ya sekondari Mabibo tena ikiwa inatembea kwa mwendo wa taratibu sana, basi ilitakiwa wawahi huko. Wakati huo kijana huyo alikuwa anajongea taratibu kutoka Loyola kurudi kwake baada ya kukaa kwa muda mrefu kidogo, alienda kukaa kwenye miti ambayo ipo barabarani akiwa anatafuna karanga zake taratibu hapo shuleni.
Wanaume hao walisimama baada ya kuona simu hiyo inaonekana karibu sana na walipo kuwepo, walipo angalia mbele walimuona kijana huyo akiwa anawasubiria kwenye huo mti, wala hakuwa na haja wa kuwakimbia watu ambao hakujua amewakosea kitu gani.
"Mmenifanya nimewasubiri kwa muda mrefu sana halafu huwa sipendi sana kupotezewa muda bila sababu za msingi hivyo kwa atakaye fanikiwa kutoka salama hapa ahakikishe siku nyingine anawahi sana. Maana nimewasubiri mpaka nimechoka na kama mngechelewa basi mimi ningewafuata mwenyewe" kijana huyo alitamka huku akiwa ananyanyuka na kujifuta futa vumbi, akiiendelea kutafuna karanga zake. Wote walibaki wanashangaa kwa maneno yake maana walimjua kama kijana muoga mno tena mnyenyekevu sasa leo hiyo jeuri ya kuongea nao kwa namna hiyo aliitoa wapi?
"Bwana mdogo yaani badala ya kupiga magoti na kutuomba tukuache ukiwa hai na wewe unapandisha kibezi mbele yetu?"
"Mhhhhhh nyie ndio ambao militakiwa kukimbia kabla hatujakutana ili muyaokoe maisha yenu ila na nyie bila kuwaza mmejileta wote. Kwahiyo wewe ndo unahisi mimi unanijua sana? Jichagueni ni nani kati yenu ambaye anatakiwa aishi ili arudishe ujumbe" alikuwa anaongea vitu ambavyo hata wao hawakuamini kutoka kwa huyo kijana dhaifu.
Mwanaume qmbaye alikuwa mbele zaidi aliona kama kijana huyo amewakosea heshima pakubwa sana hivyo walitakiwa kumfundisha adabu kwa jeuri yake kabla hawajaondoka naye, alisogea kwa jeuri na kujirusha kizembe akijua kijana huyo ni goi goi kama alivyo fikiria. Mguu wake ambao ulibakia chini ulipigwa mtama kwa nguvu, wakati anatua na kupipa makelele alipigwa teke ambalo ungehisi ni mtu anapiga penati kwenye kifua chake, alijipigiza vibaya kwenye mti ambayo ulikuwa jirani ila hakupewa nafasi ya kufika chini kabisa ya mti alipitiwa na goti kwenye shingo ambapo shingo ilivunjika vibaya mno na kumfanya kufa huku akiwa ameyafumbua macho yake.
Lilikuwa ni jambo la sekunde ambazo hata kumi na tano hazikufika walikuwa wamempoteza kijana wao mmoja kimasiara sana.
Unadhani huyo kiajna ni nani? Na ameingiaje humu ndani? Mbona kama anawajua hawa watu kuliko hata wao wanavyo mfahamu? Na kwanini aliamua kujifanya mjinga ili awe anafanya mapenzi na mke wa Oden?......78 inafika tamati, tukutane tena wakati ujao.
Wasalaam
Bux the storyteller.
Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu ngoja tuone kama upo sahihiHuyu kijana nadhani atakuwa ni jabir yule mdogo wake na Jason aliyeokotwa na Mr.Denilo Felix
Hongera
Amina ndugu yangu. Asante sanaFEBIANI BABUYA kaka unatishia sana kwenye utunzi Allah akuongoze katika hilo Inshaallah
