Innocent Killer (The Revenge)

Innocent Killer (The Revenge)

Kumekucha sasa wanaume wameshaingia kazini kusakana. Shukrani sana mkuu kwa burudani kabambe
 
2000

Ukitaka kuisoma yote kwa pamoja mpaka mwisho, unalipia 2000 tu kwa sasa, nakutumia hapo hapo hata ukitaka kitabu kizima kwa pdf ukisha lipia nakupa.

Mwisho kabisa ni sehemu ya 135.

Unataka kujua huu mzigo ndani yake kuna mambo gani haswa?

Lipia ili uisome yote kwa pamoja.

Namba za malipo

0621567672 ....HALOPESA

0745982347 .....MPESA

Zote jina FEBIANI BABUYA.

WhatsApp au kupiga 0621567672.


Muwe na asubuhi njema.
FB_IMG_1694410254412.jpg


Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
STORY: INNOCENT KILLER (THE REVENGE)
TELLER: Bux the story teller
WhatsApp: 0621567672
Email: thomasibabuya@gmail.com
AGE: 18+
SEHEMU YA THEMANINI NA NNE

SONGA NAYO................

"Seven" monalisa aliita kwa mshangao huku akiwa analipuuza swali la Alphonce

"Ndo huyo bwana mdogo ambaye amefanya siku nzima umesusa kabisa kurudi nyumbani" Seven aliuliza swali hilo ndani yake kukiwa na sauti ya wivu mkali sana pamoja na hasira zisizo na kipimo. Alphonce kuitwa bwana mdogo kwake ilikuwa ni moja kati ya dharau kali kuwahi kukutana nayo kwenye maisha yake, halafu leo mwanaume mmoja tu tena akiwa ndani ya kanzu ndiye alimuita yeye bwana mdogo.

"Hey, kujuana na huyu bibie isikufanye ukajisahau sana nitakufanya kitu ambacho hata kwenye maisha yako haujawahi kukutana nacho, funga hilo domo lako na ujitahidi sana kulitumia kistaarabu kwa watu ambao hauwajui vinginevyo utakuja kujutia sana nafasi ndogo ya maisha ambayo umepewa ili uendelee kuwa hai" kauli hiyo ilimfanya Monalisa ampe ishara ya kukataa Alphonce aliona kabisa watu hao wawili wanaelekea kwenye ugomvi ambao ungetokana na yeye. Seven aligeuka huku na huku kuangalia kama labda hayo maneno kulikuwa na mtu mwingine wa pembeni ambaye alikuwa anaambiwa ila cha ajabu alishangaa wapo watatu tu pekee maana yake huyo kijana ambaye yeye alimuita bwana mdogo hayo maneno alimpatia ni yeye mwenyewe.

Hakuamini alibaki anajishangaa yeye, aibu ya mwaka hiyo alikuwa anaipata kupata kitisho kwa kijana kama huyo, alisogea hatua kadhaa mbele akiwa anamshangaa sana kijana huyo

"Bwana mdogo hayo maneno yaliyo kosa heshima ulikuwa unanipatia ni mimi au mimi ndo sijakuelewa?" aliuliza kwa mara nyingine tena, bila kujua kwamba kukaa tu karibu na Monalisa lilikuwa ni moja kati ya kosa kubwa sana basi Alphonce aliendelea kuvimba kwa hasira sana maana mtu huyo alikuwa anendelea kumkosea heshima kwa kumuita yeye bwana mdogo.

"Nakuonya kwa mara ya mwisho, kama ukiirudia tena hiyo kauli yako basi nitakuua" aliongea kwa jazba huku akiwa amemnyooshe seven kile kisu chake kidogo ambacho muda mwingi sana kilikuwa kikishinda kwenye kiuno chake

"Ok njoo uniue" Seven aliongea kwa hasira kali, kwa maana aliona kama kijana huyo anaendelea kumkosea heshima, hiyo ndiyo ilikuwa nafasi ya kumuua kwa kukaa karibu na mwanamke ambaye alikiri kwa maisha yake yote alimpenda kuliko kitu chochote kile, angemuua hapo asingekuwa na lolote la kujibu kwa Monalisa ambaye hakujua walikuwa wana mahusiano gani na kijana huyo japo kwa yeye aliunganisha ya kwamba watu hao ni wapenzi, asingekuwa na kesi kwa sababu hayo yote kijana huyo alikuwa anajitakia mwenyewe.

Alphonce baada ya kuitwa hata hakuvunga maana mwili ulipata moto ghafla, alihitaji kumuonyesha uwezo wake huyo mwanaume, na sasa hapa Monalisa alipata kumshuhudia kwa uchache Alphonce mwenyewe. alikimbia hatua mbili na kudunda chini kwa nguvu, alijigeuza kama paka kwa buti la nguvu sana likiwa linaenda sambamba na mkono wake wa kulia, Seven alijigeuza kama vile ni mkeka unakunjwa na kumfanya kwenda pembeni kwa hatua kama nne hivi, Alphonce alitua chini kwa goti lake kwa sababu mkono ulimkosa mwanaume huyo na hata goti kwani alisogea pembeni. Ile sehemu ya ardhi ambapo alitua palipasuka na kuacha alama, hayo yote Monalisa aliyaona kufuatilia ule mwanga wa taa za gari ambazo zilikuwa zinamlika hilo eneo.

Alphonce alitabasamu baada ya kumkosa mwanaume mwenzake huyo ambaye hakuwa hata na wasiwasi mikono yenyewe alikuwa ameiweka nyuma yake, Monalisa alikimbilia kati na kumzuia Alphonce asisogee mbele ya Seven hivyo akawa amempa Seven mgongo, mwanaume huyo alipitisha kiganja chake shingoni kwa Monalisa na mwanamke huyo akazimia kisha akawekwa kando. Seven hakutaka kumbakisha tena huyo kijana jukumu la kuyaokoa maisha yake lilikuwa ni juu yake mwenyewe.

Alphonce akiwa na kisu chake mkononi alimsogelea mwanaume huyo na kurusha ngumi tano zilipita kavu bila kumgusa akiwa anasogea nyuma mpaka kwenye ukuta wa nyumba ambayo ilikuwa pembeni mwa hiyo barabara ndogo, ngumi ya mwisho ilitua ukutani na kuufanya ukuta huo uyumbe kiasi. Alphoce alirudi nyuma kidogo kujipanga akiwa anakishika vizuri kisu chake ila hilo lilikuwa kosa kubwa sana ni kama alipewa muda mchache sana wa kuyatawala hayo mapigano.

Alipokea teke la kifua ambalo lilimnyanyua mpaka upande wa pili karibu na ile sehemu ambapo lilikuwepo gari ambalo alikuja nalo Seven, uzito wa nyundo nzito ndio ambao aliusikia kifuani kwake, mtu ambaye alimpiga ni wazi alikuwa na nguvu zilizo pitiliza kwenye mifupa yake, alitema damu Alphonce. Hata hivyo hakupewa muda wa kupumzika kwani mwanaume huyo alifika hapo akiwa anashuka chini na ngumi nzito iliyo mkosa Alphonce na kuifanya ardhi ibomoke, hivyo Alphonce alirukia pembeni ila alihisi kama vile anapata maumivu makali ndipo ilipo mlazimu kuangalia ubavu wake wa kulia.

Eneo hilo lilikuwa na alama kubwa sana ya kukatwa, alishangaa kakatwa saa ngapi wakati alikatwa eneo dogo tu ambalo Monalisa alimgusa mle ndani ya klabu? hapo sasa aliinua macho yake na kumuona Seven akiwa ameushika upanga kwenye mkono wake, ulihifadhiwa ndani ya mtandio wake. Ujio wa ile ngumi Alphonce aliizingatia ngumi pekee ila iliambatanishwa na utoaji wa ule upanga wakati anaikwepa nguvi hiyo mkono wa kushoto wa Seven ulizungusha upanga kwa nguvu ulio ishia ubavuni mwa Alphonce, sasa hapo alama nyekundu ilipiga kwenye kichwa chake kwamba alikuwa anapigana na binadamu hatari sana kuliko hata hiyo kanzu ilivyokuwa inamdanganya.

Alikuwa amesha punguzwa nguvu kiasi na mtu mwenyewe hata hakuwa akiongea kabisa, Alphonce aliwaza kujilinda kisha ikiwezekana atoweke kabisa hilo eneo. Alimsogelea mwanaume huyo kwa nguvu akiwa anakuja kwa zigzaga maana alijua akicheza vibaya anakutanishwa na huo upanga, Seven hakuwa akijongea zaidi ya kumhesabia hatua Alphonce, baada ya mwanaume huyo kumkaribia sana alipo, Seven alihesabu hatua moja tu kurudi nyuma kwa kasi sana kisha akasogea upande ule ule ambao ndio Alphonce alishika kisu chake.

Alirusha mkono wenye kisu kwa nguvu sana kiasi kwamba hata kama mtu huyo angekipangua basi lazima kingepenya tu kwenye mwili wake, ila ule mjongeo wa haraka sana wa Seven ambao hata yeye hakuutarahia kabisa ulimharibia mahesabu yake hivyo akajikuta anamkosa na kuishia kupigwa kikumbo ambacho kilimfanya ayumbe kidogo na kushindwa kujilinda, alizamishiwa ule upanga tumboni na kupigwa ngumi kumi mfululizo kwenye mwili wake, zilimmaliza nguvu kabisa na kumlainisha mithili ya mlenda. Ngumi ambazo zilikuwa zinaingia kwenye mwili wake zilikuwa na uzito mkubwa sana na asingeweza tena kuzihimili, alidondokea mbali sana na taratibu alikuwa anaona siku zake za kuishi kama zinaanza kumjia kwa kasi sana bila yeye kutarajia.

Alikuwa anatoa damu sana Alphonce kwenye mdomo wake na tumboni pamoja na ubavuni, alisimama huku akiwa anauma meno yake kwa maumivu makali mno, mwanaume alijikaza na kuuchomoa upanga huo kutoka tumboni kwake ambapo alipiga mekelele sana kwa aina ya maumivu ambayo alikuwa akiyapata hapo. Aliurushia upanga huo pembeni akiwa hoi maana alishuka chini na kusimama tena teratibu kwa kujikongoja, mkono wake mmoja ulikuwa na kile kisu kidogo bado.

Sasa huo ndio muda ambao yeye alikumbuka kuhusu bastola ambayo ilikuwa kiunoni kwake kwamba huenda ndio ulikuwa msaada wake wa mwisho, bastola hiyo hakutaka kuitumia tangu mwanzo kwa sababu kubwa mbili. Kwanza alikuwa akijiamini sana kwani sanaa ya mapigano ilikuwa ni sehemu ya maisha yake hivyo hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba mtu huyo anaweza akamkalisha yeye kwenye hiyo tasnia, lakini sababu ya pili hakuhitaji kuitumia kwani ingepiga makelele sana huenda polisi ambao hawakuwa mbali sana na hilo eneo wangefika na kuwaletea matatizo ikiwemo yeye mwenyewe hivyo huo mchezo ilitakiwa waumalize tu wenyewe kimya kimya.

Ila mpaka muda huo hakuwa na namna nyingine zaidi ya kuitumia silaha hiyo iliyokuwa imebakia kama mkombozi wake pekee, alijipapasa kiunoni ajabu hakuiona kabisa, sasa hapo kichwa kilipata moto aligundua kwenye harakati za kupigana hapo ilikuwa imedondoka na hakujua imedondokea wapi. Hayo mambo yote aliyawaza kwa muda mfupi sana basi aliangaza huku na huku aliona vitu viwili, mtaro wa maji machafu na kona moja ya nyumba ambavyo vyote vilikuwa hatua kadhaa kutoka sehemu aliyokuwepo. Alipaswa kuzichanga karata zake vyema sana ili amkimbie mwanaume huyo kwa kutumia akili kuliko mbio maana kwa mbio za kawaida na hali yake licha ya kuwa mkimbiaji bora asingeweza kufua dafu hivyo huo mtaro na hiyo kona kimoja wapo kilitakikuwa kutumika kama kamali ya kujaribu kuyaokoa maisha yake.

Mwanaume alikirusha kisu chake kwa nguvu sana kikiwa kinajigeuza geuza upande upande kuelekea pale alipokuwepo Seven, Seven alikiona kisu vyema kutoka kwa mhanga wake ambaye alijua hana pa kukimbilia ndiyo maana alikuwa anamuangalia kijana huyo mwenye jeuri ili aone atafanya nini. Ujio wa kisu hicho na namna kilivyokuwa kinakuja kilimfanya aanze kurudi nyuma ambapo alifika mpaka kwenye gari na kufungua mlango wa nyuma kwa nguvu, kisu hicho kikaishia kukita kwenye mlango huo huku yeye akiwa upande wa pili wa mlango na kuinama, Seven alivyokuja kuinuka baada ya sekunde kama nne tu hakuona mtu sehemu yoyote hilo eneo zaidi ya yeye na Monalisa ambaye alikuwa amezimishwa na kulazwa pembeni mwa barabara.

Seven alisogea mpaka pale ulipokuwa upanga wake, aliinama na kuuchukua huku akiwa anaangalia huku na huku lakini hakuona alama yoyote wala mchakacho wowote ule, hivyo aliinuka na kumfuata Monalisa pale chini, alimbeba na kuondoka naye.

Ule muda ambao kile kisu kilirushwa ni muda ambao Alphonce alicheza na vitu viwili kwa wakati mmoja. Kitu cha kwanza ilikuwa ni mbinu ambayo ingetumika kukizuia kile kisu ndiyo ingesaidia kitu chake cha pili kukamilika, kitu cha kwanza alijua kwa namna ya ujio wa kile kisu huyo adui yake asingekizuia kwa mikono kwani lazima kingemkata tu hivyo kwa umbali aliokuwepo angelitumia gari kama ngao yake. Kama kisu kingekita kwenye gari basi lazima kingetoa mlio tu kwani gari ni kama bati, sasa ule mlio ndio ulikuwa mpango wa mbinu ya pili.

Kile kisu wakati kinapiga kelele kwa kugonga kwenye lile gari huo ni muda ambao alikuwa anataka kuutumia kurukia kwenye ule mtaro wa maji machafu ambao ulijengewa pembeni kwani kishindo chake kingemezwa na zile kelele hivyo kumsaidia yeye kutojulikana na adui yake kwamba ameingia wapi huku akijitahidi kuruka kuendana na kasi ya damu kutoka kwenye mwili wake. Ilikuwa ni moja ya kamali kubwa sana ya maisha ila hakuwa na namna na ilizaa matunda, wakati ule Seven amesogea lile eneo kuchukua ule upanga, Alphonce akiwa amezama kwenye maji hayo machafu sehemu alipokuwa amejichomeka, alikuwa amezama kabisa akiwa ameacha tu sehemu ya juu na macho yake kidogo hivyo kwa vitundu vidogo ambavyo vilikuwa juu ya eneo hilo lililo jengewa, alifanikiwa kumuona mtu huyo ambaye hakumjua ni nani, alitoka wapi akiwa anachungulia kila sehemu lakini baadae akafanikiwa kuondoka baada ya kutojua adui yake aliingia wapi.

baada ya dakika kama tano tangu Seven aondoke ndio muda ambao Alphonce alitoka ndani ya mtaro huo wa hayo maji machafu, alikuwa kwenye hali mbaya mno huku akiwa anatoa harufu kali isivyo kawaida. Alipiga hatua ya kwanza, ya pili, wakati anahitaji kumalizia ya tatu mwili ulimsaliti alidondoka chini na kupoteza fahamu.

Haukupita muda mrefu sana kuna gari nyeusi ilifika hilo eneo, wakashuka wanaume wawili ambao miili yao ilikuwa imefunikwa na nguo nyeusi kila sehemu, walimbebea na kutoweka naye hilo eneo.

Alphonce ataishi tena? Na kama ataishi kaingia kwenye mikono ya watu gani tena?.....84 sina la ziada nakusanya kilicho changu.

Wasalaam

Bux the storyteller.View attachment 2754555

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Mkuu tupe na leo aisee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom