Ingekuwa heri JK uage sasa!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ingekuwa heri JK uage sasa!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kashaija, Oct 27, 2008.

 1. K

  Kashaija JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 255
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ingekuwa heri JK uage sasa


  MHESHIMIWA Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya
  Muungano wa Tanzania, salaam aleykum. Juma lililopita
  niliwasiliana na Watanzania wote kwa njia hii ya makala.
  Nilijaribu kuwachokonoa ili kupata mawazo yao juu yako.

  Na kwa bahati nzuri nilikuwa nimeongea moja kwa moja na
  Watanzania wote wakiwamo wasaidizi wako muhimu. Na ili
  kuwahakikishia kwamba niliwalenga na wao pia niliamua
  kuwataja kabisa pale niliposema, "Yote kwa yote ni
  kwamba
  kila mtu anajua sasa Rais Kikwete uwezo wake wa
  kuliongoza
  taifa na chama chake umepungua.

  "Ninaamini ndani ya dhamiri yangu kwamba hata
  wasaidizi wake, wakiwamo usalama wa taifa, mawaziri na
  manaibu mawaziri, wanamtandao na wapambe wake, wabunge,
  viongozi wenzake ndani ya chama, watendaji wake
  serikalini
  na wasaidizi wake wengineo wote wanajua hili".

  Nilifanya hivyo kwa makusudi ili kupata maoni yao juu ya
  hili. Nawatambua sana wasaidizi wako. Ni watu mahiri sana
  kwa kulinda maslahi yao na ya wakubwa wao. Nilijua
  watanijibu haraka haraka kwa kukanusha ukweli huo mdomoni
  huku mioyoni mwao wakiutambua. Lakini hawakufanya hivyo.
  Hii inathibitisha kwamba hata wao ukweli uliwagusa na
  wamefikia mahali ambapo hawawezi kupingana nao.

  Wa kwanza kabisa kuwasiliana nami ni kiongozi wa zamani wa
  CCM katika mojawapo ya nafasi za uongozi ndani ya chama
  ngazi ya kitaifa. Yeye alinipigia simu kabisa na
  kujitambulisha kwa jina, nami nikamtambua kwa sauti
  kwamba
  ni yeye. Akanipongeza kwa kusema nimeandika vizuri sana na
  kwa kweli maneno yake na sauti yake yalionyesha dhahiri
  kukubaliana na ukweli niliouainisha.

  Huyu ndiye akazidi kuthibitisha nilichokizungumza katika
  aya hiyo hapo juu. Ukweli umewasuta ndani ya dhamira zao
  na
  kwa kweli umefika wakati ambao ukweli hauwezi kufichika
  tena. Wengi sasa wanaogopa kukutetea hadharani
  wasijeonekana vituko kwa kuupinga ukweli ulio wazi (naked
  truth).

  Mheshimiwa Rais, wasomaji walionitumia ujumbe mfupi wa
  simu, walionipigia simu, walionitumia barua pepe na hata
  waliozungumza nami uso kwa uso, wote wamenipongeza kwa
  ujumbe uliokuwa wazi ukieleza ukweli halisi na kila mmoja
  wao aliishia kusema 'atang'oka' 2010. Baada
  ya
  kutafakari ujumbe wa wasomaji na matukio yaliyoripotiwa
  kwenye vyombo vya habari juma lililopita, nimeamua
  kukuandikia waraka huu ili nikupatie ushauri makini
  lakini
  bure.

  Msomaji mmoja, kwa mfano, aliongea kwa uchungu jinsi
  ulivyojibu swali la mwanahabari kule Ufaransa.
  Ulipokuuliza
  kwa nini nchi yako ni maskini ukasema eti hata wewe
  hujui.
  Kwa maoni yake ilikuwa ni aibu kubwa kwa kiongozi wa nchi
  kujibu hivyo tena mbele ya viongozi na wanahabari wa
  kimataifa. Uliuonyesha ulimwengu kwamba nchi hii ni ya
  ajabu na watu wake ni wa ajabu. Ni kama ulikuwa
  unathibitisha kauli iliyopata kutolewa na mwandishi mmoja
  kwamba Tanzania ni nchi pekee duniani inayoweza kukaa
  miaka
  10 bila rais na bado ikabaki na amani.

  Kwa maoni yangu pia, rais wa nchi kusema hajui umaskini wa
  wananchi wake unatokana na nini ni sawa na kusema nchi
  haina kiongozi. Rais wa namna hiyo hawezi kuhangaika na
  mipango ya kuiondoa nchi katika umaskini, maana hajui kwa
  nini wananchi ni maskini. Anafikiri pengine ni
  "wavivu tu
  wa kufikiri" ama "fursa zipo ila kwa ujinga wao
  hawataki
  kuzitumia".

  Rais wa namna hiyo hawezi kujua madhara ya ufisadi wa EPA,
  Meremeta, Tangold, Kiwira, mikataba ya Richmond, IPTL na
  jinsi inavyochangia umaskini wa watu wake. Hawezi kuona
  ubaya wa rais na mke wake kujiingiza kwenye biashara kwa
  kutumia ofisi, fursa na vyeo vyao vya Ikulu kuwanyonga
  wananchi. Na kwa sababu hiyo hawezi kujihangaisha
  kuyashughulikia madudu kama hayo kama unavyofanya wewe
  hivi
  sasa.

  Rais wa namna hiyo atakuwa 'busy' na safari za nje
  zisizo na kikomo, kukutana na marais wakubwa kama akina
  George Bush tena wanapokutana Bush atampiga piga mabegani
  rais kama huyo kama alivyofanya alipokuja hapa Dar es
  Salaam, na tungetamani kupata tafsiri ya kitendo hicho
  cha
  George Bush, ambaye wafuatiliaji wanasema hata
  mlipokutana
  Japan alikupiga piga begani tena, kutoka kwa Salva
  Rweyemamu yule mwandishi wa zamani aliyeisakama serikali
  kwa kalamu yake, lakini baadaye akawa mwanakampeni wako
  mahiri kwa kutumia kalamu hiyo hiyo na baadaye
  ukamzawadia
  ukurugenzi wa mawasiliano Ikulu.

  Mheshimiwa, watu wanashangaa hata kitendo cha serikali yako
  kushindwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maji,
  visivyokauka
  tulivyonavyo hapa nchini na ardhi safi tena kubwa
  inayofaa
  kwa kilimo cha umwagiliaji kujihakikishia chakula cha
  kutosha. Lakini badala yake unakwenda Italia kwa kutumia
  mamilioni ya shilingi kuomba chakula kwa WFP.

  Mheshimiwa Rais, si siri ni aibu kubwa. Mabilioni
  yaliyopotea kwenye ufisadi yangetosha kuanzisha
  'scheme' kubwa 13 za umwagiliaji kwenye mikoa 13
  ya
  nchi hii. Na hesabu zake ni rahisi mno wala huhitaji
  kutumia shahada yako ya kwanza ya uchumi ambayo hata
  hivyo
  sijui kma umewahi kuitumia.

  Chukua milioni 152 kwa siku kwa mwaka mmoja tu zilizolipwa
  kwa Richmond/Dowans ambazo kwa siku 365 za mwaka ni
  bilioni
  55. Jumlisha bilioni 2,098 zilizolipwa kwa IPTL kwa miaka
  minane tu kwa kuzingatia kauli ya aliyekuwa Naibu Waziri
  wa
  Nishati na Madini, William Ngeleja, bungeni Dodoma
  Agosti6,
  2007 kwamba kwa kipindi cha Julai 2005 hadi March 2006
  peke
  yake IPTL ililipwa jumla ya bilioni 262.3. Kwa vipindi
  vinane tu kama hivyo kampuni hiyo imelipwa jumla ya
  bilioni
  2,098. Jumlisha bilioni 133 zilizoibwa kupitia EPA, kisha
  juu yake ongeza bilioni zisizopungua 600 zilizopotea
  kupitia ujenzi wa minara miwili pacha pale BoT. Halafu
  umalizie na mabilioni yaliyopotea kupitia viufisadi
  vingine
  vingine kama ubinafsishaji wa TTCL, NBC, Kiwira, n.k
  ambazo
  nazo si chini ya 100.

  Halafu chukua hiyo jumla inayofikia bilioni 2,986 bila
  kuongeza bilioni ulizozitumia wewe kwa safari zako za nje
  tangu uchaguliwe kuwa rais. Igawanye jumla hiyo kwa
  gharama
  za mradi mzima wa kupeleka maji Shinyanga ulioshikiwa
  bango
  na best yako ili aje kuonekana anafaa kuwa waziri mkuu wa
  nchi hii. Utapata 13 ambazo ni scheme kubwa za
  umwagiliaji
  zenye thamani ya sh bilioni 225 kila moja.

  Ina maana tungeweza kuwa na scheme kama hizo katika mikoa
  13 inayoongoza kwa ardhi inayofaa kwa umwagiliaji. Njaa
  ingetupata wapi. Hivi sasa dunia inapolia na kupanda kwa
  bei za vyakula sisi tunaoita kilimo uti wa mgongo wa
  uchumi
  wetu tungekuwa matajiri kwa kuuza chakula.

  Lakini hivi sasa eti serikali yako inapiga marufuku kuuza
  chakula nje ya nchi, mkulima anayetegemea kuuza chakula
  chake cha ziada ili apate matumizi yake mengine ikiwamo
  kusomesha watoto unamwambi nini?

  Mheshimiwa Rais, watu waliodunisha maisha ya Watanzania
  kiasi hicho eti bado hutaki kuwachukulia hatua hadi leo.
  Umeunda tume juu ya tume nyingine lakini mafisadi
  wanaendelea kutesa. Ajabu zaidi chama unachokiongoza juma
  lililopita, kimetangaza eti kumpa onyo kali aliyekuwa
  naibu
  meya wa Ilala na kumzuia kugombea cheo chochote zaidi ya
  udiwani alionao, sababu eti ni kushiriki bomoabomoa ya
  Tabata Dampo na kuisababishia hasara serikali ya sh
  bilioni
  1.8, kuwasababishia usumbufu wananchi wa Tabata Dampo na
  kukiaibisha chama.

  Gazeti hili likaiandika habari hiyo Jumatatu wiki hii, kwa
  kichwa kilichosema; 'CCM yacharuka'. Naomba
  kupingana moja kwa moja na maneno aliyoyatumia mwandishi
  wa
  habari hiyo. Kimsingi CCM haijacharuka. Bali ina mkakati
  pengine unaosimamiwa na wewe mwenyewe mwenyekiti wako
  kukisafisha chama. Msitudanganye kiasi hicho, kwamba mna
  uchungu sana na pesa za serikali, mnawajali wananchi na
  kulinda hadhi ya chama chenu.

  Fikiria hasara za mabilioni ya serikali niliyoyataja hapo
  juu, yote yamesababishwa na wana-CCM, fikiria Watanzania
  milioni 40 wanaoteseka kwa ajili ya wana CCM na ukumbuke
  jinsi hadhi, si tu ya chama unachokiongoza bali pia ya
  serikali unayoiongoza ilivyoporomoka ndani ya mwaka
  mmoja,
  kwa ajili ya wana-CCM. Lakini hamjawakaripia wala
  kuwafuta
  uanachama kama mlivyofanya kwa Naibu Meya Yakubu.

  Huu ni usanii ambao umeshajulikana kwa Watanzania.
  Mheshimiwa Rais, juma lililopita umetoa kali nyingine ya
  mwaka. Umewaasa Watanzania wavumilie shida wasikate
  tamaa.
  Hii nayo ni kauli nyingine ya mzaha kwa Watanzania kama
  ile
  ya kusema hujui umaskini wao unasababishwa na nini.

  Natamani ungekuwa unasoma maoni ya wasomaji. Siku hizi
  Tanzania Daima imeanzisha sehemu ya maoni ya wasomaji
  wanaosoma gazeti hili, kwenye tovuti. Msomaji mmoja
  aliposoma alisema hivi: "Kaka yetu usipate tabu wewe
  sema
  tu.

  Sisi tumezoea shida, huna tofauti na Karume anayewaambia
  Wazanzibari watazoea tu. Sasa sisi tumezoea na wewe
  endelea
  kula nchi maana mafuta si kazi yako. Wewe linda mtandao
  wako
  usisambaratike, maana inabidi uutumie kurudi madarakani
  mwaka 2010." Haya si maoni ya mtu anayekuambia kwa
  wema.
  Huyu ana uchungu ndani ya moyo wake na kwa ujumla maneno
  yake ni laana kwa serikali yako.

  Mwingine akasema hivi: "...Kikwete suala la mafuta na
  maisha magumu havimhusu kabisa. Ndiyo, si anatuonyesha
  hivyo kwa kuwalinda mafisadi? Na sasa kapata kisingizio
  cha
  bei ya mafuta basi ndiyo itakuwa hadithi. Hivi
  wadanganyika
  wenzangu mnafikiri bei ya mafuta ikishuka (let's say)
  hadi nusu, ndiyo maisha yatakuwa bora kwa kila
  mdanganyika?
  "Dhahabu imepanda sana bei katika soko la dunia. Kwa
  nini vitu kama hivi vimeshindwa kufidia pengo la mafuta
  yaliyopanda?

  Watu wengine wanafananisha Bongo na Marekani - eti na
  Marekani maisha yamepanda. Nyie ndugu zangu hebu acheni
  mzaha! Wewe unakula humburg na pizza Macdonald halafu
  unatuambia maisha yamepanda? "Chonde chonde jamani.

  Natamani mngerudi huku mkapigika mkashindia kauzu ndiyo
  mngejua watu wanaongea nini…" Ukurasa huu
  hautatosha
  kukupatia maoni ya kila msomaji, lakini natamani
  ungejisomea mwenyewe habari hiyo kisha chini yake usome
  maoni ya watu.

  Wasaidizi wako wanaweza kukusaidia kutembelea
  http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/7/21/habari1
  Mheshimiwa Rais ningekushauri jambo moja tu. Kukubali pia
  ni uungwana wa aina yake na Watanzania wanapenda watu
  waungwana.

  Baada ya ziara yako ndefu mkoani Tanga, utakaporejea Ikulu
  fanya jambo moja tu. Andaa hotuba yako ya mwezi bila
  kumshirikisha msaidizi wako yeyote. Ita waandishi wa
  habari
  kana kwamba unakuja kujibu tu maswali watakayokuuliza
  halafu
  wakisha fika toa hotuba yako kabla hujaulizwa maswali.

  Waeleze wanahabari na Watanzania kwa ujumla kwamba wakati
  unachukua fomu za kugombea urais mwaka 2005 hukuijua
  vizuri
  sababu ya umaskini wa Watanzania. Waeleze kwamba wewe
  ulidhani kazi uliyokuwa nayo ni kuwaita tu wawekezaji
  uliokuwa umeshazoeana nao sana ukiwa waziri wa Mambo ya
  Nje
  na Ushirikiano wa Kimataifa, na kwamba wakishakuja
  kuwekeza
  tayari maisha bora kwa kila Mtanzania yanajipa.

  Sema kwamba umekuja kugundua kuwa mambo sivyo yalivyo.
  Umaskini wa Watanzania una uhusiano wa karibu mno na
  utawala wa nchi. Na kwamba utawala wa nchi kwa miaka
  mingi
  umebaki kuwa mbovu hasa kupitia 'system'
  iliyojengwa na
  Chama chako Cha Mapinduzi ya kulindana viongozi, bila
  kujali
  madhara yanayosababishwa na viongozi mafisadi hapa nchini
  na
  hivyo hata malaika akiwa rais wa nchi hii kupitia CCM
  hakuna
  maendeleo yatakayopatikana.

  Sema wazi wazi kwamba kama rais wa nchi hata kama ungekuwa
  na dhamira ya kuikwamua nchi kutoka kwenye umaskini
  unaosababishwa na uongozi mbovu, ungeshindwa kwa kuwa
  kikulacho ki nguoni mwako. Maswahiba zako waliofanya juu
  chini upate urais ndiyo hao hao mafisadi waliokubuhu hata
  jina la mafisadi haliwafai tena. Nasikia wengine wameanza
  kuwaita 'mafisidi'.

  Na wewe huwezi kuwatupa wakati ungali ukikumbuka mchango
  wao mwaka 2005. Kwa sababu hiyo, ili kulinda uhusiano
  wako
  nao na wakati huo huo kulinda heshima kupita kiasi
  uliyopewa na watanzania, umeamua kuachia ngazi na hivyo
  mwaka 2010 hutagombea tena.

  Wapatie Watanzania nafasi ya kuanza kufikiria tangu sasa
  chama kitakachowafaa kuongoza nchi hii hapo 2010,
  kutokana
  na sera zake kabla hawajafikiria ni nani atawafaa kuwa
  rais wa nchi baada yako. Uhakika mmoja tu nakupatia kwamba
  hutabaki ulivyo machoni mwa Watanzania.

  Najua wapambe wako watakulaumu sana, maana kwa kung'oka
  wewe utakuwa umewakosesha ulaji mkubwa. Lakini utakuwa
  umejiweka katika nafasi nzuri ya kuwa shujaa mbele ya
  Watanzania, kwa kutoboa ukweli na utapumzika kwa amani
  baada ya miaka 10 ya kusaka urais na miaka mitano ya
  kushutumiwa na Watanzania kwa kutotoa (not delivering)
  kile
  ulichotarajiwa.

  Naamini pensheni itatosha, isipotosha utaongezea kilimo cha
  kisasa. Fanya uamuzi sasa ama utakuja kujuta
  utakapostaafu.
  Watafanya kama walivyomfanyia Chiluba hadi
  utashangaa.
  Uamuzi ni wako Mheshimiwa Rais
   
 2. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Kashaija unadhani huwa zinamfikia hizi habari au unategemea wale vijana wake ndio wampitishie??

  Nadhani next term watanzania hawataangalia sura ya mtu katika kuchagua raisi...
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Naomba kudiffer. Pamoja na yote uliyoeleza ni ya kweli, mimi binafsi yangu toka moyoni nisingependa Rais wetu mpendwa, na handsome boy Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete ajiuzulu sasa. Mbona 2010 sio mbali.

  Kama kawaida baada ya Kubenea kusema wana CCM wenye uchungu wa dhati na nchi hii wanapanga mkakati wa kumuengua JK asiwe mgombea wa CCM 2010 ili kuinusuru nchi, hoja hiyo imetafsiriwa kama Uhaini.

  Na wenye mkakati huo wamesha uabandon baada ya kujulikana hivyo JK ndiye mgombea wa CCM 2010.

  Huu ndio wakati wa watanzania kumjulisha wamechoka na sasa watasema basi inatosha.

  Tatizo ninaloliona hapa ni ile kauli ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyere kuwa kiongozi bora ni lazima atatoka CCM.

  Hivi hawa wapinzani waliopo wako tayari kuunganisha nguvu wamsimamishe John Memosa Cheyo?.
  Makamo awe yoyote ila waziri mkuu Zitto Kabwe.Wakipanga safu nzuri, wananchi watawaamini na CCM itapumzika kwa amani na Mtukufu mpendwa wetu, Mhe. JK kipenzi cha watu, atajumuika na watu wake. Tena itakuwa afadhali angalau kile kijiwe chetu cha
  Saigon kitachangamka tena.
   
 4. Tonga

  Tonga Senior Member

  #4
  Oct 27, 2008
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Uchaguzi wa sura umeigharimu Tanzania almost miaka 5 ya ubabaishaji natumaini watajifunza in a hard way kutokana na kosa hili. Ninamwomba Mungu alinisuru Taifa tupate Rais mwenye uchungu na nchi na anayejua analofanya in 2010.
   
 5. M

  Mama JF-Expert Member

  #5
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0

  Pasco huwatakii mema wapinzani,, ooops vyama mbadala. Si wamsimamishe Mtikila.
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Cheyo? Huyu si ndiye yule aliyekwapua mihela ya Waswazi? Awe rais?
   
 7. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2008
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Umesema ndugu yangu na sina la kuongezea. Kama kweli Mwalimu alikuwa anawatandika watu viboko, hapa kifimbo kingepata ajira ya uhakika. Na mimi nasema wakati wa JK kuondoka ni sasa, ameshindwa kazi, period.
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Yes Cheyo ndiye the only opposition leader mwenye presidential personality kama wapinzani wakiungana kumsimamisha. JK chali 2010.

  Ni cheyo ambaye anacomand respect ya wote hata wanasisiem waliochoka na udhaifu wa CCM watampa kura zao.

  Aliyoyafanya Swazi siyajui ila alisaidia sana Watanzania waliofika huko. Yeye na Mwizarubi walijitolea nyumba zao kuwa makao ya kufikia Watanzaia wote bila ubaguzi.

  The truth jamaa ana roho nzuri na anabishana kwa hoja na sio kwa jazba.

  Hebu nipatie mpinzani mwingine yoyote atakayeweza kusimama na JK akambwaga?.

  Naweza nikakupa madhaifu ya wengine wote kama ukuhitaji. Nakiri upinzani una viongozi wengi wazuri swali la kujiuliza ni je wanachagulika?.
   
 9. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #9
  Oct 27, 2008
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama wasaidizi wa raisi hawamwambii kinachoendelea watoto wake je? Will some one invite them to join this forum if they still havent! Someone better inform daddy dearest that there's some serious socio-political movement going on in cyberspace. A political party in the making perhaps....
   
 10. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2008
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Ni matumizi mabaya ya maneno (misuse of phrase). Huyu jamaa alipofikia hawezi tena kusikia lugha ya namna hii; ya kumpapasa na kutekenya tekenya! Sana sana atalala usingizi wa pono! Lugha anayotakiwa kusikia ni moja tu,.... siyo maneno wala kelele ....bali vitendo. Kumwondoa pale mahali kwa kutumia nguvu ya wale waliompa hiyo nafasi, nukta. Haya mambo mengine ni kujifariji na kufurahisha baraza/kijiwe tu!
   
 11. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #11
  Oct 28, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hii ya kuwasaidia watu na kuwa na roho nzuri si kigezo cha kumpa urais. Hata Don Corleone aliwasaidia sana marafiki zake na kuonekana kuwa mwenye roho nzuri lakini alikuwa ni Mafia tu. Cheyo alikwapua mihela ya Waswazi na hata alipopata ubunge Waswazi walitushangaa sana Watanzania. Kwa Tanzania tunachohitaji sasa hivi si personalities. Tunachohitaji ni vision na baada ya hapo ndipo tuangalie ni nani anayeweza kutusaidia kuifikia hiyo vision. Haya ya personalities ndiyo yaliyotugandisha na akina Mrema na chama chake na Cheyo na chama chake.
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Oct 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,178
  Likes Received: 5,595
  Trophy Points: 280
  Nyere alishase,a ikulu hakuna uzuri pale si sehemu ya kujipaka poda wala perfume mlidhan anaota hao sasa mabrazameni wenu!!!!!
  Jk&lowassa wanashindwa hata kuangaliana kwa uchafu wao@@@@@@@@@@

  wait lowasa atakapotajwa kuwa waziri##$#$#$

  eeeeeeeeeeeeeehhhhhhhhhhhhhh

  babay face wetu mnatisha babukubwa!!!!!!!!!!
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Oct 28, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  QUOTE=Jasusi;310833]Hii ya kuwasaidia watu na kuwa na roho nzuri si kigezo cha kumpa urais. Hata Don Corleone aliwasaidia sana marafiki zake na kuonekana kuwa mwenye roho nzuri lakini alikuwa ni Mafia tu. Cheyo alikwapua mihela ya Waswazi na hata alipopata ubunge Waswazi walitushangaa sana Watanzania. Kwa Tanzania tunachohitaji sasa hivi si personalities. Tunachohitaji ni vision na baada ya hapo ndipo tuangalie ni nani anayeweza kutusaidia kuifikia hiyo vision. Haya ya personalities ndiyo yaliyotugandisha na akina Mrema na chama chake na Cheyo na chama chake.[/QUOTE]

  Kwa wakati huu uliobakia kabla ya 2010. Huu sio muda wa kugroom new leader. Aliyoyafanya Swazi has nothing to do with with Tanzania. Hoja yangu hapa ni... Kama sio yeye nani?. Lipumba?, Mrema?, Mbowe?, Zito?, Dr.Slaa?, Mbatia?, Mtikila?. Makaidi?, Chipaka? Au nani anauzika, anachagulika na ana Presidential Personality?. Kwa taarifa tuu, JK hana Presidential Pesonality ila ni handsome boy mwenye haiba ya kupendwa na watu. His smiles doesen't reflect integrity. We need a man of integrity kama Obama.
  Tuletee majina ya watu sio kuishia na kina Don, pamoja na Umafia wao, wao ndio wafadhili wakuu wa kanisa Katoliki ndiyo dini yenye wafuasi wengi zaidi duniani. Bulusconi ni Don na alikuwa PM itakuwa Cheyo.

  Mbona JK kaupata kwa ufadhili wa pesa za ufisadi? Itakuwa Cheyo?.
   
 14. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #14
  Oct 28, 2008
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kwa wakati huu uliobakia kabla ya 2010. Huu sio muda wa kugroom new leader. Aliyoyafanya Swazi has nothing to do with with Tanzania. Hoja yangu hapa ni... Kama sio yeye nani?. Lipumba?, Mrema?, Mbowe?, Zito?, Dr.Slaa?, Mbatia?, Mtikila?. Makaidi?, Chipaka? Au nani anauzika, anachagulika na ana Presidential Personality?. Kwa taarifa tuu, JK hana Presidential Pesonality ila ni handsome boy mwenye haiba ya kupendwa na watu. His smiles doesen't reflect integrity. We need a man of integrity kama Obama.
  Tuletee majina ya watu sio kuishia na kina Don, pamoja na Umafia wao, wao ndio wafadhili wakuu wa kanisa Katoliki ndiyo dini yenye wafuasi wengi zaidi duniani. Bulusconi ni Don na alikuwa PM itakuwa Cheyo.

  Mbona JK kaupata kwa ufadhili wa pesa za ufisadi? Itakuwa Cheyo?.[/quote]
  Pasco,
  Naona hujanielewa ndugu yangu. Tanzania ya sasa haitafuti au haihitaji mkombozi as in personality. Tunachohitaji Watanzania ni ukombozi. Ndio maana nimesema kwanza tu-identify vision itakayotuletea ukombozi na baada ya hapo ndipo tusema katika visheni hii ni nani aliye na uwezo wa kutuongoza. Wewe umekazania personalities mimi nimepanua uwanja kidogo. Najua kuna Watanzania wengi tu wenye uwezo. Nakubali kabisa kuwa tunahitaji mtu mwenye integrity lakini hawezi kuifanya kazi hiyo peke yake. Kwa hiyo kama unataka majina mimi huko hunikuti. Tuzungumzie vision itakayotuondoa kwenye matatizo tuliyo nayo and then we can identify who among us is dedicated and can help lead to the promised land. For your info I also know Cheyo more than you can imagine.
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Oct 28, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Haya tena tunarudi kule kule.. tunatafuta KUIGA!... jamani kiongozi wetu apatikane kulingana na sisi wenyewe ktk mazingira haya magumu tuliyokuwa nayo..
  Hawa ma Don mnaozungumzia tunao kina Rostam na tumeyaona matokeo yake iweje tufikirie kuwa ma Don nchini wanaweza kuwa sawa na Marekani wakati watu na mazingira yetu hayafanani?...
  Mimi namtaka Dikteta mmoja mwana mapinduzi kama Chavez wa kibongo bongo!
  Nani mweye Ubavu huo hata sijui, lakini tunahitaji dikteta mwenye kuweka maslahi ya Taifa mbele dhidi ya propaganda zote za kifisadi iwe toka ndani ama nchi za nje!
   
 16. MyTanzania

  MyTanzania Senior Member

  #16
  Oct 29, 2008
  Joined: Sep 9, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Watu wa karibu wa rais hawamwambii ukweli,wanachokifanya ni kumpa moyo tu.Mnakumbuka alisema KELELE ZA CHURA HAZIMZUII MWENYE NYUMBA KUPATA USINGIZI.
   
Loading...