Infidelism: Nani rahisi kukamatwa na kwa nini?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,475
39,991
Zipo sababu nyingi zinazowafanya watu wawe na mahusiano ya nje ya mahusiano yao rasmi (kucheat). Tangu enzi na enzi mambo haya yamekuwa yakiwatokea wanaume na wanawake wa kila kabila, dini, lugha na mahali na kila mtu anayo sababu yake ya kumfanya hivyo. Japo wakati mwingine inaendana na hisia ya kujisikia vibaya lakini ukweli ni kwamba watu huamua na kuhalalisha kwa sababu ambazo ni wao wanazijua na vigumu watu wengine kuweza kuzielewa. Wengine wanafikiria ni suala la tamaa tu za kimwili lakini sayansi ya jamii yote inaonesha kuwa kuna mambo mengi zaidi ambayo yanaweza kusababisha mtu kuikubali itikadi ya infidelism. Hata hivyo hili siyo somo langu la leo.

Kuna watu wanaamini kabisa kuwa wanawake ndio 'cheaters' wazuri sana na kuwa wana uwezo wa kuweza kuwachanganya watu wawili au zaidi bila mhusika mkuu kuweza hata kushuku. Wengine, hata hivyo wanaamini kuwa ni wanaume ambao ni cheaters 'wazuri' kwani anaweza kuwa na mahawara kadhaa kwenye mji ule ule mmoja bila hata kushukiwa. Lakini wengine hudai kuwa wanawake huweza kushuku mapema kuwa mtu anacheat lakini huwa wanaamua kumezea as long as yule mtu anatimiza wajibu wake wote wa pale nyumbani.

Wapo wanaume hata hivyo ambao hawaamini kabisa kuwa mke/mtu wake anaweza kucheat kwani amejiaminisha kuwa mwanamke yule yuko hoi bina taaban (hasa kama ni mwanamme anayeamini sarakasi za chumbani kama kigezo). Lakini mwisho wa siku mjadala ambao hudumu mara nyingi ni yupi rahisi kukamatatika. Wapo wanaosema wanaume ni rahisi sana kukamatika kwani kucheat kwao ni sawa na kurusha rusha mipira mitatu angani (juggling) kiasi kwamba anaweza kurushwa kwa muda fulani tu mwisho wa siku atadondosha mmoja au yote (wengine hudai wanaodondoshwa ni mahawara!). Lakini wapo wanaoamini kuwa ni wanawake ambao wanaweza kushikika kirahisi kwa sababu wao wakianza kweli kucheat huwa wanahamisha kabisa hisia na majeshi yao kule kwingine kiasi kwamba hawawezi kujitoa kule kwingine na wakarudi nyumbani wakawa kama kawaida.

Kwa wale wataalamu (wenye uzoefu au waliowahi kujisomea dhana hii wakiwa vyuoni) msimamo upi unaelekeana na ukweli na ni kwanini hasa?
 
Kila mmoja anaweza kukamatika, hakuna aliye untouchable. Mwanamke sio rahisi kukamatwa:
1 wanawake ar good at multitasking na hawasahau haraka wala kujisahau (tuite u-Dellilah). Groomed to be smart, nafikiria in terms of covering tracks
2 wanawake hawategemewi ku-express feelings waziwazi. Mfano sex inawezafanyika kama wajibu and they can fake na isigundulike. Na kuna cycle na mood za kujitetea (maybe it is something to do with my hormones blah blah)
3 aren't women good actors? Kama mume anakupiga mangumi na unaweza kutabasamu mbele yake na mbele ya dunia nzima...na yeye bado akajiskia kuwa mume? Basi nadhani huwezi kustukiwa unless hajali tena

4 secret keepers. Kwanza wanawake hatuaminiani. Unajua siku mkitofautiana shosti atamwaga maharage.At most wanawake wana siri zao wasizoshare na mtu. Atakua na affair, mashosti wanaweza jua bt they will never have details. Wanaume hadi kaka zake wata-meet small house. Katika harakati za kujinadi for any benefit, mwanaume atatumia umbea kusema popote hadi habari zitafika
Eh,ngoja niishie hapa.
 
MMM kuna post enzi hizo nilisemaga while we MEN think we are the players...................actually we the ones being played ; mfano unaweza ukacheat na mke wa mtu ukamtia mimba na akakudhulumu damu yako and there is no way ukajua na hata ukijua ni wachache wenye ubavu wa kudai haki katika hii scenario nad the vice versa is the same
 
King'asti umesema almost kila nilichotaka kusema, zaidi naweza kusema wanawake ni ngumu sana kunogewa na penzi la nje na kujisahau kitu ambacho ni tofauti kwa wanaume walio wengi
 
Wanawake wako 'smart' sana katika hiyo game ya kucheat....yaani unaweza kula meza moja (zamani sahani moja!) na mume mwenzio bila kujua. Lakini na wanaume nao hawajambo.......kuna visa vingi tu vya wanaume kutembea na 'beki tatu' bila mwenye mali kustuka...akija kustuka 'beki tatu' tayari ana mimba!
 
Lakini sasa kwanini wanaume huwa wanashtuka sana wakigundua mke au mpenzi wake anacheat?

hata mambo yana 'cultural differences '
kwa waafrika karibu wote 'polygamy' ilikuwa ni sehemu ya maisha

na kwenye 'culture' ya polygamy mwanaume alikuwa 'ha cheat' only labda

atembee na mke wa mtu.....

sasa kwa kuwa i was normal kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,
ndani ya 'subconscious ' ya mwanaume hasa wa kiafrika ni kuwa 'cheating is not a bid deal for a man'

wakati haikuwa kawaida kwa mwanamke kuwa na waume wawili,ndo maana mshutuko unakuja
kwa sababu hatukuzoea kuwa ni kawaida
 
hata mambo yana 'cultural differences '
kwa waafrika karibu wote 'polygamy' ilikuwa ni sehemu ya maisha

na kwenye 'culture' ya polygamy mwanaume alikuwa 'ha cheat' only labda

atembee na mke wa mtu.....

sasa kwa kuwa i was normal kuwa na mwanamke zaidi ya mmoja,
ndani ya 'subconscious ' ya mwanaume
hasa wa kiafrika ni kuwa 'cheating is not a bid deal for a man'

wakati haikuwa kawaida kwa mwanamke kuwa na waume wawili,ndo maana mshutuko unakuja
kwa sababu hatukuzoea kuwa ni kawaida

Nimevutiwa na mchango wako ila naomba kukuuliza ni mambo mangapi hayakua kawaida na siku hizi ni kawaida?
Kwanini unashtuka sasa!
 
Nimevutiwa na mchango wako ila naomba kukuuliza ni mambo mangapi hayakua kawaida na siku hizi ni kawaida?
Kwanini unashtuka sasa!

kuna mambo meengi sana aisee
nafikiri wazee wetu 'hawakujua' kuwa wanawake nao wana mahitaji sawa na wanaume hasa kwenye sex
na pengine zaidi.......kwa hiyo unakuta wanawake kumi au ishirini wanaolewa na mtu
mmoja na 'wana fake' kuridhika na kuwa na furaha...

sasa wanawake wa sasa wameelimika na kujitambua na wamekuwa na demands wazi kabisa..
na wanaume ndani ya subcouncious yetu bado tunafikiri kizamani....ndo maana tunashtuka
tukiuona ukweli mbele ya macho yetu...

bado kwa kiasi kikubwa wanawake wana cheat ili 'kuziba pengo la intimacy au sex'
while wanaume huwa tuna cheat hata kama unae anaekuridhisha home....
 
Wanawake huwa hawakamatiki kirahisi, wanajua sana kuficha siri tofauti na wanaume.(King'asti ameeleza vizuri hapo juu)..na hii mara nyingi inachangiwa na uoga.
 
Mi sijui nikoje,

Siamini kama wanawake wanacheat kama wanaume wanavyocheat aisee. Na midume iko smart ikisaidiwa na mi-advantages kibao inayowafeva. Wanawake hata kama wapo wanaocheat lakini ODM najiaminisha hawawezi fikia kiwango cha midume. Na hata hao wanaocheat idadi yao haifikii idadi ya midume bana.

Majukumu yanayomkabili mwanamke mara nyingi yanampa nafasi finyu kucheat ukilinganisha na mwanaume.
Imani iliyozoeleka kuwa mwanamke akicheat basi ni malaya wakati mwanaume akicheat anaonekana kidume nayo inachangia wanawake wengi wasicheat kama wanaume.
Ile mazoea pia kuwa mtongozaji lazima awe mwanaume inachangia pia.....mwanamke asipotongozwa na mwanaume atabaka? Ila vidume vinatongoza mpaka wanawake sita kwa siku. Na kukataliwa na wote sita ni mwiko.

Kwanini vidume havikamatwi ugoni?..... Rejea sheria mama kumi za infidelity.
Ngoja ODM asepe.
 
Back
Top Bottom