GE2025 INEC, NIDA wamkana Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Thank you
 

kwani wangekubali, unadhani?????

#KATAA WAHUNI#
 
Pole Pole alihitimisha kwa kusema "nimetimiza wajibu wangu, na pia naombeni watanzania na Mungu wa Mbinguni mnisamehe"

Mwisho wa kunukuu.
 
Aibu sasa ngoja ataje kbs aliyeunganisha mifumo walioshiriki
 
Mhusika si tu katoa hiyo shutuma, pia ameshauri, chombo huru cha wataalaamu kichunguze na kupinga au kieleze tofauti na shutuma zake. Hao waliotokea ni wajibu wao kupinga, wafanye nini zaidi?
 
Siku zote tunajua CCM wanaiba kura ila swala la mifumo kusomana ni chumvi
 
Asante kwa Polepole kutufungua macho.
 
Ili kupata card ya unachama ya ccm NIDA ni moja ya mahitaji,kujiandikisha kuwa mpiga kura NIDA ni moja ya mahitaji though ni optional
 
Wanaukana ukweli?sisi tuliowahi kucheza huko tulihitaji sana mtu kama polepole aje alipue Bomu mambo yaeleweke.
Mfumo wa NIDA uko integrated na mfumo wa VRS na ni kweli CCM ndiyo wanatumia kujipigia wawezavyo. Iko wazi
 
Hata ivo hata sisi hatutaki wakubali
 
"Najua watakanusha, sasa wakikanusha waambieni basi kije chombo huru kikafanye uchunguzi pale INEC, NIDA na CCM" alisema Polepole
 
Kama kuna mtu kamuelewa polepole anisaidie kueleweshwa vipi kura zinapatikana kwa kuunganisha hiyo mifumo wakati kura zinapigwa kwa makaratasi.
Vipi mawakala wakatazwe kupewa matokeo vituoni kama mambo yote yanaenda kwa makaratasi? Vituo vikiwa wazi kutoka matokeo vyama vinaweza kujumlisha matokeo yao nakujua kura walizopata, INEC wakitangaza tofauti ni rahisi kuwa na ushahidi. Huwezi ukachakachua bila kuwa na takwimu halisi.
 
Katika kujitenga naona ndo wametangaza kujiunga rasmi!
 
Nimetafakari kwa kina alichokisema H Polepole kuwa yeye alihusika pia kuunganisha mfumo wa NIDA,TUME NA WA CCM kwa nia ya kuhujumu uchaguzi 2015 na bila shaka hadi leo. je wananchi wote hakuna hata mmoja wa kufungua mahakani shauri la kikatiba kuhoji kuhusu mfumo huo. Mahakama iruhusu kuthibitisha ukweli wa hii tuhuma kabla ya uchaguzi 2025. Na ikibidi vyombo vya nje viruhusiwe kupitia mifumo hii. Shahidi namba moja ni Polepole,Mkurugenzi wa Nida nk. kuliko kukaa mitandaoni pekee na kupiga kelele.
 
Habari za jumamosi tulivu Wana jF,

Baada ya press ya HP juzi usiku juu ya hoja ya kuunganisha mifumo ya iNEC na NIDA , na baadae kukatokea matamko na makanusho kutoka Kwa wakuu wa mamlaka hizo zilizohusishwa kwenye press, sijaona haja ya kukataa kuunganishwa au kuwepo Kwa ukweli huo, kwani jambo ambalo lipo wazi kabisa na pia hakuna ubaya wowote Kwa mifumo hiyo kuunganishwa.

Kwanini nasema imeunganishwa?
Wakati wa zoezi la kuboresha taarifa katika daftari la wapiga kura, kulikuwa na njia Moja wapo ambayo mteja anaweza kuanzisha mchakato wa wkuboresha taarifa zake binafsi kupitia mfumo wa ovrs.inec.go.tz(Kwa Sasa upo offline) ambapo mteja huyu alitakiwa atjaze namba ya NIDA na namba yake ya mpiga kura(kadi ya zamani), baada ya hapo mfumo utavuta taarifa za mteja kutoka NIDA na kuzijaza katika mfumo wa iNEC.
Sambamba kama utoaji wa kadi za wanachama wa CCM unahitaji mwanachama kuwa na naba ya NIDA, Kuna uwezekano mkubwa wa pia mfumo huu kuunganishwa na mfumo wa NIDA Kwa ajili ya verification ya mwanachama.Hope hata vyama vingine wanaweza link na NIDA endapo nao wanatoa kadi wa wanachama wao Kidijitali.
#OKTOBA TUNATIKI
#NRNE
KUra Yako,Haki Yako. Tunza Kadi Yako Ya Kupigia Kura Kwa wivu Wote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…