Sio za sa100?!?Polepole kapuliza upepo nyeti za kuku zote hadharani.
Sio za sa100?!?Polepole kapuliza upepo nyeti za kuku zote hadharani.
Kura za Urais ubunge na udiwani huunganishwa kwa nchi nzima. Lakini mifumo ndiyo husaidia kujua mambo ya idadi ya wapiga kura na Demografia Yao.Kama kuna mtu kamuelewa polepole anisaidie kueleweshwa vipi kura zinapatikana kwa kuunganisha hiyo mifumo wakati kura zinapigwa kwa makaratasi.
Matokeo uchaguzi wa s/mitaa 2024 yalitangazwa mapema/haraka sana. Idadi ya uwapiga kura imesemwa ni milioni 37 waliojiandikisha, ni mifimo gani inatumoka na je, huu ni uhalisia?Kwahiyo unadhani watakubali
Kwenye majumuisho ya kura kura feki na vituo feki ndipo zinapo ingizwa kutumia huo mfumo waoAssume we ni mtu A, unashindana na mtu B kuhitaji kura za watu 20 ambazo mtapigiwa kwa karatasi, mtu B anavitambulisho vya watu wote 20.
Unaweza nambia nikwanamna gani Vitambulisho vitamsaidia mtu B kukuibia kura ulizopigiwa na miongoni mwa wale watu 20 ?
Hupati uteuzi acha kujisumbua wewe hakuna mwenye Akili Timamu atakaa akuelewe licha ya kujifaragua kuandika mandishi mengi yasiyo na point hata moja, ni wajinga pekee watakaa kukusikilizaKauli ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kwamba mifumo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeunganishwa na ile ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaibua wakuu wa taasisi hizo na kukanusha madai hayo.
Wakuu hao wamebainisha kwamba hakuna mfumo wowote kwenye taasisi zao uliounganishwa na ya chama chochote cha siasa na kwamba jambo hilo si siri, na endapo lingekuwa hivyo lingekuwa tayari limejulikana.
Katika mazungumzo yake aliyoyafanya usiku wa kuamkia leo Agosti 22, 2025, Polepole amedai kwamba mifumo ambayo chama hichoimeijenga, inakiwezesha kupata ushindi hata kabla hawajakwenda kwenye uchaguzi.
INEC yakanusha
Akizungumzia tuhuma zilizoibuliwa na Polepole, Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele amesema hakuna mfumo wowote wa taasisi hiyo uliounganishwa na chama chochote cha siasa, hususani CCM.
“Hakuna. Sisi ni Tume huru na vitu kama mifumo kuunganisha si vitu vya siri, ukienda tu kitaalumu utajua, ni mfumo gani tuliounganisha na mtu mwingine,” amesema mwenyekiti huyo.
Jaji Mwambegele amesisitiza kwamba hata kama wangekuwa wameunganisha, hiyo inawahakikishiaje ushindi, kwani Tume hiyo inafanya kazi kwa mfumo wa dijitali? amehoji katika majibu yake.
“Kwa maana; je, kura zitapigwa kielekroniki? Kwa hiyo, hakuna kitu kama kuunganisha mifumo ya INEC na chama kingine, lakini nataka nimsikilize anavyozungumza huyo Polepole,” amesema Jaji Mwambegele.
Mwenyekiti huyo amesema mifumo yao haijaunganishwa na chama chochote cha siasa na hata Daftari la Kudumu la Wapigakura wameligawa kwa vyama vyote vya siasa, vinginevyo wangeweza kusema waunganishe katika mifumo yao ili waone.
“Lakini, daftari tumeligawa kwa vyama vyote vya siasa tangu Julai 27, 2025 kwa mfumo kidijitali na mfumo wa hardcopy (nakala ngumu),” amesema.
Jaji Mwambegele amesisitiza kwamba msimamo wa INEC, mjadala unaoendelea kuhusu kuunganisha mifumo, si wa kweli na wananchi hawapaswi kuamini hilo.
NIDA nayo yajitenga
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Nida, James Kaji pia amesema hakuna jambo kama hilo la kuunganisha mifumo, huku akisisitiza Polepole aeleze vizuri kama aliwahi kufanya kazi na mamlaka hiyo huko nyuma.
“Hakuna kitu kama hicho. Ni vema akawaelezea vizuri labda yeye anajua na kama ameshafanya kazi Nida,” ameeleza Kaji alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na Polepole kuhusu kuunganishwa kwa mifumo hiyo.
Chanzo: Mwananchi.
ccm wanahaha kujibu jibu chawa wanakomaa kusaka Uteuzi kupitia humo humo lakini wenye Akili Timamu wapo na polepole hawateterekiNi muda wa polepole kuja kudadavua vizuri maana bado wameweka pamba masikioni
Tanzania hakuna uchaguzi kuna Maigizo tu kwani ccm walishapiga kura mapema wanasubiria kutangazwa tuSasa kwanini tumeccm inataka mawakala wasipewe matokeo na cm wasiende nazo vituoni? Huo sio uchaguzi
Uzuri sasa watu wengi hawana imani na ccm hata wajieleze vipi hakuna wa kuwaamini tenaUkweli ukifika wakati wake huwezi kuuzuia kamwe!!
TUME HURU YA UCHAGUZI ❎❎❎Huyo Mwambegele kachaguliwa na nani kukaa hapo? Kifupi hana jipya.
Juzi nilihudhuria mkutano na Tume huru na Waandishi wa Habari aliambiwa ukweli kuwa Tume haikubaliwi na haitakiwi na Wananchi...huyu Jaji aliwaka utadhani mwehu.
Wewe ndiyo una IQ ndogo zaidi kwa kuamini kukariri Maovu ujinga wote wa ccm na kukataa ccm isikosolewe, hakuna kitu kibaya kama kujiona upo sawa kwa kila kitu na hupaswi ukosolewe mileleNilikuwa nabisha wakenya wakisema watanzania tuna IQ ndogo.
Hili la polepole limefanya niamini kweli watanzania tunashida ya kufkiria.
Mtu kwakuwa aliongea ni mtu anae muamini basi yeye anachukuwa tu km lilivyo nae kuliamini.
Sasa Akili ya kwaida tu ujiulize, access ya NIDA inakusaidia vipi kupata kura kupitia mfumo ?
ccm ya sasa haina chawa wa kujibu hoja bali wapo chawa wa kusaka Uteuzi ndiyo hujiandikia andikia hovyo tu pasipo kutafakari kablaWamemjibu kiwepesi Sana aisee!
MSEMAJI MKUU WA RAIA NA UJUMBE KWA WATAWALA NA VYOMBO VYAO INEC NIDA
View: https://m.youtube.com/shorts/xGgdxpxWyYs
Wenye Akili Timamu wapo na polepole wenye uzezeta wapo na ujinga wa ccmJiulize kwanini mawakala hawaruhusiwi kupatiwa nakala za matokeo