GE2025 INEC, NIDA wamkana Polepole

GE2025 INEC, NIDA wamkana Polepole

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumzia suala la kuanzisha mchakato wa uboreshaji wa Daftari mtandaoni, Bw. Kailima amesema Tume imejenga mfumo ujulikanao kama OVRS (Online Voters Registration System) utakaomwezesha mpiga kura anayeboresha taarifa zake kuanzisha mchakato mtandaoni na baadae kwenda kwenye kituo ili kukamilisha taratibu na kupata kadi yake ya mpiga kura.

“Uboreshaji wa taarifa kwa njia ya mtandao una masharti, kwa wale ambao wanataka kurekebisha taarifa zao ni lazima wawe na namba ya NIDA, lakini, mpiga kura anayehamisha taarifa zake hatalazimika kuwa na namba ya NIDA….,” amesema Bw. Kailima.

Amefafanua kuwa namba ya NIDA ni muhimu kwa ajili ya kufanya uhakiki wa taarifa za mpiga kura ambazo zinarekebishwa kwenye Daftari.

Uzuri internet ni maktaba kubwa sana

Rejea
 
2010 ulikuwa na umri gani mkuu?
Ulisikia malalamiko ya Dr. Slaa kwenye matokeo ya Urais.
Matokeo yanayotangazwa na tume yalikuwa tofauti na kwenye karatasi walizohesabia vituoni
Athari za kusoma kichwa cha habari nakukimbilia ku comment ndio hii sasa
 
Mkuu..nakuhakikishia daftari la wapiga kura..Lina majina mengi sana ya marehemu, wengine hata hawapo ndani ya nchi, wengine Wagonjwa ambao hata Kwenda kuboresha taarifa zao hawawezi...
Lakini kwakuwa daftari Lina chukua direct majina kutoka NIDA na kuyabandika...unaweza kukuta wewe jina lako lipo Bukoba na hukujiandikisha....
Hivi unaamini wapiga kura millioni 37 wamejiandikisha ?
Hili linahitaji uamini viongozi wako.
Unafkiri nani anaweza tawala hii nchi akajengewa hii hoja kama "Umeweka mifuko ya kuandikisha watu hewa" akaichomoa ?
 
As if this was a complete surprise to anybody, except you!

Which cave do you reside in; such that this was an unexpected revelation?

Naona bado unasubiri polisi wenye mabegi ya kura wakamatwe ili kuthibitisha uhusika wao kwenye matendo maovu wakati wa uchaguzi.

Nadhani akili yako inafanya kazi ki-CCM zaidi.
Umeelewa lakini nilichoandika au umekurupuka tu kunishambulia baada ya kilevi kukupa nafuu kurejea kwenye utambuzi wa mazingira yanayokuzunguka?

You are afflicted by pseudo-mentality, dude!!!!
 
Umeelewa lakini nilichoandika au umekurupuka tu kunishambulia baada ya kilevi kukupa nafuu kurejea kwenye utambuzi wa mazingira yanayokuzunguka?

You are afflicted by pseudo-mentality, dude!!!!
"...pseudo mentality..."? Is this a new disease! Never head of such a thing; and I am aware of the many "afflictions" that beset humans. Where did you pick up this "pseudo" thing?
 
Kauli ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kwamba mifumo ya Chama cha Mapinduzi (CCM) imeunganishwa na ile ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), imewaibua wakuu wa taasisi hizo na kukanusha madai hayo.

Wakuu hao wamebainisha kwamba hakuna mfumo wowote kwenye taasisi zao uliounganishwa na ya chama chochote cha siasa na kwamba jambo hilo si siri, na endapo lingekuwa hivyo lingekuwa tayari limejulikana.

Katika mazungumzo yake aliyoyafanya usiku wa kuamkia leo Agosti 22, 2025, Polepole amedai kwamba mifumo ambayo chama hichoimeijenga, inakiwezesha kupata ushindi hata kabla hawajakwenda kwenye uchaguzi.

INEC yakanusha

Akizungumzia tuhuma zilizoibuliwa na Polepole, Mwenyekiti wa INEC, Jaji Jacobs Mwambegele amesema hakuna mfumo wowote wa taasisi hiyo uliounganishwa na chama chochote cha siasa, hususani CCM.

“Hakuna. Sisi ni Tume huru na vitu kama mifumo kuunganisha si vitu vya siri, ukienda tu kitaalumu utajua, ni mfumo gani tuliounganisha na mtu mwingine,” amesema mwenyekiti huyo.

Jaji Mwambegele amesisitiza kwamba hata kama wangekuwa wameunganisha, hiyo inawahakikishiaje ushindi, kwani Tume hiyo inafanya kazi kwa mfumo wa dijitali? amehoji katika majibu yake.

“Kwa maana; je, kura zitapigwa kielekroniki? Kwa hiyo, hakuna kitu kama kuunganisha mifumo ya INEC na chama kingine, lakini nataka nimsikilize anavyozungumza huyo Polepole,” amesema Jaji Mwambegele.

Mwenyekiti huyo amesema mifumo yao haijaunganishwa na chama chochote cha siasa na hata Daftari la Kudumu la Wapigakura wameligawa kwa vyama vyote vya siasa, vinginevyo wangeweza kusema waunganishe katika mifumo yao ili waone.

“Lakini, daftari tumeligawa kwa vyama vyote vya siasa tangu Julai 27, 2025 kwa mfumo kidijitali na mfumo wa hardcopy (nakala ngumu),” amesema.

Jaji Mwambegele amesisitiza kwamba msimamo wa INEC, mjadala unaoendelea kuhusu kuunganisha mifumo, si wa kweli na wananchi hawapaswi kuamini hilo.

NIDA nayo yajitenga

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Nida, James Kaji pia amesema hakuna jambo kama hilo la kuunganisha mifumo, huku akisisitiza Polepole aeleze vizuri kama aliwahi kufanya kazi na mamlaka hiyo huko nyuma.

“Hakuna kitu kama hicho. Ni vema akawaelezea vizuri labda yeye anajua na kama ameshafanya kazi Nida,” ameeleza Kaji alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tuhuma zilizoibuliwa na Polepole kuhusu kuunganishwa kwa mifumo hiyo.

Chanzo: Mwananchi.
Well what did you expect from ccm scum burgs, in these offices,!?
Pole pole was senior ccm official, used to be one of the inner circle members of President JPM! The commander in chief,
For God sake!
 
Back
Top Bottom