India yaipiku China kwa idadi ya watu

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
7,224
12,946
Nchi ya India imeipiku nchi ya China kwa population.


Population:

1. India 1,426,409,584
2. China 1,425,731,257
3. USA 339,688,556
4. Indonesia 277,148,717
5. Pakistan 239,693,115
6. Nigeria 222,914,017
7. Brazil 216,214,106
8. Bangladesh 172,659,039
9. Russia 144,528,119
10. Mexico 128,297,060
.
12. Japan 123,405,307
18. Turkey 85,740,393
19. Germany 83,300,994
21. UK 67,698,634
23. France 64,735,380
24. South Africa 60,322,787
25. Italy 58,899,388
29. South Korea 51,790,420
33. Argentina 45,725,645
38. Canada 38,726,161
55. Australia 26,395,113
72. Netherlands 17,609,287
87. Sweden 10,601,484
96. UAE 9,504,149
100. Austria 8,955,779
101. Switzerland 8,787,128
114. Singapore 6,008,362
115. Denmark 5,906,142
119. Norway 5,467,469
168. Luxemburg 653,708
179. Iceland 374,788
197. Seychelles 107,660
217. Monaco 36,297
227. Tuvalu 11,396
234. Vatican 518


Screenshot_2023-05-01-15-46-23-46_f4b68248098991d824f647422fc8e6e2.jpg
 
Huenda mila, dini na tamaduni za kihindi zinachangia ?....kama vipi waanzishe sera kali kama China kudhibiti ongezeko hilo la kutisha kwa miaka kadhaa.

imhotep Yoda T14 Armata
Kudhibiti ili iweje? Waafrika mnadanganywa na wazungu eti population inaharibu mazingira na nyie mnadanganyika mnaacha kuzaana matokeo yake mnaenda kuisha duniani. Wahindi na wachina wana akili wanakataa huo ujinga maana wanajua population ni nguvu ya superiority. Mataifa yenye watu wengi ndo yanakuja kuwa na nguvu sana kiuchumi.
 
Kudhibiti ili iweje? Waafrika mnadanganywa na wazungu eti population inaharibu mazingira na nyie mnadanganyika mnaacha kuzaana matokeo yake mnaenda kuisha duniani. Wahindi na wachina wana akili wanakataa huo ujinga maana wanajua population ni nguvu ya superiority. Mataifa yenye watu wengi ndo yanakuja kuwa na nguvu sana kiuchumi.
Population kubwa kuharibu mazingira huo ni ukweli kabisa........kuhusu kuwa na watu wengi ni nguvu kubwa kiuchumi sijui sana.
 
Huenda mila, dini na tamaduni za kihindi zinachangia ?....kama vipi waanzishe sera kali kama China kudhibiti ongezeko hilo la kutisha kwa miaka kadhaa.

imhotep Yoda T14 Armata
India hawajafikia level ya kiuchumi ya China kuacha kupungua kuzaana, hata China ilikuwa mbali na level za South Korea na mbali zaidi na level za Japan kijamii.

Japan ukizaliwa unakuta kuna namna ya kuishi imepangwa na jamii nzima inakutarajia ufanye hivyo, kinyume chake wanakusimanga. Umri wa kuwa chuo unajulikana kwenye miaka 18-21, umri wa kumiliki assets au kazi au kitu chochote cha maisha unajulikana. Mwishowe Wajapani wanapambana mno na kujisahau kuanzisha familia au kuwa serious na mapenzi. Wako lonely na wana suicide rate ya juu. Wako workaholic

China ukuaji wa uchumi unaleta impacts kijamii, miji inakua changamoto za maisha zinakuwa nyingi, watu wako preoccupied na kazi, foleni, kujiendeleza kusoma, n.k hivyo hawazai sana. India wao tamaduni zao zitawafanya wazaane kwelikweli labda kampeni za miongo kadhaa iliyopita zirudiwe.
 
Ina maana wanaosema Waafrica tunazaa sana wanatuonea ?.....labda tutakuja kuwapiku hao jamaa mbeleni

Waafrika bado Sana.
Tatizo la waafrika ni kudandia mambo ya watu.
Bora Wasukuma Kwa hapa Tanzania wameamua kuendelea kukiwasha, nafikiri miaka 20 ijayo wakiendelea hivi alafu baadhi Yao wakasomeshwa vizuri wanaweza kuitawala Tanzania watakavyo
 
Back
Top Bottom