INDIA: Wananchi wapanda miti Million 50 kwa masaa 24

MSEZA MKULU

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2011
Posts
3,821
Reaction score
5,825
Katika kupambana na Mabadiliko ya tabia nchi, wananchi 800,000 wa mji wa Uttar Pradesh walijitokeza mitaani na Kupanda miti Millioni 50 ndani ya masaa 24, Hii wamevunja record ya upandaji miti.

Kulingana na mabadiliko ya tabia nchi, tuna kitu cha kujifunza hapa.
 
sio kila siku tuwe tunakumbuka kuzaliana tu harafu tukayasahau mazingira hilo ni kosa.
ukienda maeneo ya usukumani, ni wagumu sana kupanda miti. Hiyo culture haipo kabisa. ukianzia igunga shuka hadi kahama, nenda hadi shinyanga na baadhi ya maeneo ya misungwi. Geita na maeneo ya sengerema wanajitahidi. Kagera karibu mkoa mzima wako vizuri. kuna umuhimu wa kuhamasaisha huu utamaduni maana mazingira ni uhai.
 
Hii ni njema sana.
Ilitakiwa ipitishwe sheria nchi nzima kila familia ipande miti 100 na miti iwekwe tayari na maeneo yatengwe.
 
watu wanaamini dhambi ni kuiba kuua mtu nk. lakini wanasahau kwamba kukata miti hovyo nayo ni dhambi kubwa. na kuna dini flani wao wanaamini ukipanda miti unabarikiwa hawa naipenda sana falsafa yao.
kama kweli wanaitekeleza kwa vitendo.
 
Nchi hii itakuwa kama bustani ya eden.
Badala ya kufukuza wakuu wa wilaya/mikoa kwa sababu ya njaa wafukuzwe kwa sababu wameshindwa kuhakikisha wananchi wamepanda miti.
Miti ni MVua, Miti ni Chakula, Miti ni utajiri na kichocheo cha afya
 
Na sasa hivi kuna deforestation ya hatari.
Kwanin kusiwe na re/aforestation ya hatari pia?
 
Upandaji miti una umuhimu sana. Mfano hali ya hewa Moshi ilianza kuwa ya joto lakini RC wa zamani wa Kilimanjaro Leonidas Gama alidhibiti ukataji miti na hivi sasa kuna matokeo mazuri.
Mkuu kwa Moshi naona bado,wananchi wake bado wanatakiwa kuongeza juhudi sana katika upandaji miti,hali ya hewa mpaka msimu wa jua wa mwaka jana ilikua hatari sana.
 
Nchi hii itakuwa kama bustani ya eden.
Badala ya kufukuza wakuu wa wilaya/mikoa kwa sababu ya njaa wafukuzwe kwa sababu wameshindwa kuhakikisha wananchi wamepanda miti.
Miti ni MVua, Miti ni Chakula, Miti ni utajiri na kichocheo cha afya
kuna mkuu wa wilaya wa Mbinga nasikia alianzisha nursery ya miti kwa gharama ya serikali. miti hiyo aliigawa bure kwa wananchi wapande. alisema serikali itapata mapato mbao zikianza kuuzwa. laiti tungerasmisha huo mpango tungekuwa mbali sana. pia tungeingia kwenye soko la carbon credit.
 
watu wanaamini dhambi ni kuiba kuua mtu nk. lakini wanasahau kwamba kukata miti hovyo nayo ni dhambi kubwa. na kuna dini flani wao wanaamini ukipanda miti unabarikiwa hawa naipenda sana falsafa yao.
kama kweli wanaitekeleza kwa vitendo.
MOLA atubariki tuachane na mikaa itokanayo na miti!
 
Hili wazo la kuhamasisha jamii kujua umuhimu wa kupanda miti ni mzuri sana,ila kwanza lidhibitiwe kama sio kuzuia kabisa ukataji wa mkaa.
images
upload_2016-7-20_13-0-10.jpeg
 
What a huge step.
In the long run this will ensure India food security, tourism, employment and trade.
But kupanda miti ni kitu kimoja; na kukuza miti ni kitu kingine.
Wajitahidi tu ikue maana miti 50 inahitaji uangalizi wa hali ya juu.
 
Wanasema 60% ya miti hiyo yote itaota kulingana na plan hadi kufikia mwaka 2030, watengeneze msitu wenye zaidi ya hekari Million 235.
 
Its a good plan lakini wanahitaji kuwekeza sana kwenye kukuza hiyo miti,
Kwasababu mimi nimeshudia tu MUFINDI kukuza miti ni kazi sanaa na inahitaji mtaji mkubwa.
 
Jamaa serikali yao imetenga trillion za kitanzania kama 13 kwa ajili ya upandaji wa miti nchi nzima
 
Kudadeki,
Narendra yuko serious sanaa na nchi yake. Wamejipanga.
Marekani kuna wanasiasa vichaa kama Al Gore wanahubiri kuwa Global Warming ni hoax.
 
Back
Top Bottom