India: Wanafunzi washambuliwa wakiwa katika sala

Msikilize Yesu mwenyewe anavyokuambia

Yeye hakupewa ujumbe wa utume kwa ajili ya watu wote wa kabila zote.

Bali yeye alikuwa Mtume kwa ajili ya wana wa Israeli tu.

Mwenyewe alijua mipaka ya utume wake. Kwahiyo alisema:

1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).

2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli.

“Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).

3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende,
wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 10:5-6).

4. Baadhi ya Wakristo wanadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe.

Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu. Yeye amesema kwamba: “Lakini watakapo wafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo
mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).

5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya
kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba: “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).

6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49.
pole sana
 
Back
Top Bottom