Inawezekanaje mke kumnyima mume wake unyumba?

King Jody

JF-Expert Member
Oct 8, 2022
914
1,704
Habarini wandugu,

Moja kwa moja kwenye mada yetu.

Rafiki yangu mmoja aliniuliza `Hivi King Jody umewahi kunyimwa unyumba na mke wako? Nikamjibu hapana, hata mara moja, nikamwambia nipo kwenye ndoa kwa zaidi ya mika 10 sijawahi nyimwa hata mara moja hata kama tumepishana kauli nikihitaji napewa na itakuwa sehemu ya kumaliza ugomvi kati yetu.

Jamaa akaniambia aisee una bahati sana, mimi huwa nanyimwa, sababu siijui na nikipewa ni kwa masharti,
nataka niachane na mke wangu, nioe mwingine.

Wanajamii nimshauri vp huyu rafiki yangu, wewe pia unaweza kumshauri, lakini swali langu ni je, haya mambo yapo kwenye ndoa? kama yapo nini huwa chanzo?

Je, wewe umewahi kukutana na tatizo kama hili?

Tujadiliane ili tupate kujifunza.

Asanteni.
 
Kama wataka ku kwepa mambo kama hayo oa wake wawili au watatu kihalali utateseka, wanawake wengi wanatumia kuadhibu, mwanaume kwa njia ya kumnyima unyumba ila ukiwa na plan "b" ambao ni rasmi hawezi kuthubutu. Hivi nyie mnaishi je na mke moja? Au mnazini tu, mgejua madhara yanao tokana na zuni ni makubwa kuliko kero za wake wawili.
 
Back
Top Bottom