Inawezekana Mkoa wa Ruvuma una Viongozi Waandamizi wengi Serikalini maana unamiminiwa miradi kama yote

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,779
Mkoa wa Ruvuma kwa sasa ni kama huge construction site au work shop.

Kwa miaka ya hivi karibuni umekuwa unamiminiwa miradi ya kila aina tofauti na mikoa mingine kama Rukwa, Morogoro, Lindi, Singida, Kigoma nk.

Kwa mfano ndani ya miaka 7 iliyopita kumemiminiwa miradi kama ifuatavyo;

  • Barabara zote kuu zinazoingia/Kutoka zimejengwa na zinaendelea na ujenzi.
  • Barabara za mitaani mjini zimejengwa sana na za Tarura huko Mawilayani zinapasukiwa kama zote.
  • Imejengwa Hospital Mpya ya Mkoa achilia mbali Hospital za Wilaya zote.
  • Mradi mkubwa wa kusambaza Maji Songea wa zasii ya Bil.120 unaendelea.
  • Uwanja Mpya wa Ndege na kufungwa Taa kabisa.
  • Ujenzi wa New Campus z Vyuo Vikuu 2.
  • Ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia mazao(Mkoa huu ndio unaongoza Kwa Maghala mengi zaidi ya 16).
  • Mashule, Zahanati, Vituo vya Afya havihesabiki.
    -Ujenzi wa Bandari za Ndumbi na Mbamba Bay
    -Ujenzi wa Sgr ya Mbamba Bay -Mtwara Port
Screenshot 2023-07-03 100901.png


Ruvuma kwa sasa ni mkoa wa 3 kwa kuchangia pato la taifa Tanzania yaani GDP.(Taarifa zisizo Rasmi)

Screenshot 2023-07-03 101137.png

Mikoa ambayo haina watu wa connection haitakiwi kupata maendeleo?

Ili kuondoa huu upendeleo ni vyema tuwe na kanuni maalumu ya mgawanyo wa keki ya Taifa.

Screenshot 2023-07-03 101259.png


My Take
Mkoa wa Ruvuma ndio Chato ya Sasa?
 
SEKONDARI MPYA YA DKT SAMIA NAMTUMBO
Sekondari mpya ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyosajiriwa kwa jina la Dkt Samia Suluhu Hassan imejengwa Wilaya ya Namtumbo inatarajia kuanza kuchukua wanafunzi wa kidato cha tano Julai 2023.

Serikali ya Awamu ya Sita imetenga shilingi bilioni nne kupitia program ya kuboresha elimu ya sekondari nchini (SEQUIP) kutekeleza mradi huu ambapo hadi sasa zimetumika shilingi bilioni tatu na kazi inaendelea.

Sekondari hii ikikamilika kwa asilimia 100 itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi zaidi ya 1000.

Serikali imetoa shilingi bilioni 7.7 katika Mkoa wa Ruvuma kupitia program ya SEQUIP kujenga sekondari mpya 11 katika Halmashauri zote nane za Mkoa wa Ruvuma ikiwemo sekondari hii ya wasichana ya Mkoa wa Ruvuma iliyojengwa eneo la Migelegele Kata ya Rwinga Wilaya ya Namtumbo
 
Kutesa kwa zamu
Hakika naona ni zamu yenu Sasa
---

RAIS SAMIA KUIGEUZA MBAMBABAY KUWA KITOVU CHA UCHUMI TANZANIA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi bilioni 70 kuanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa bandari ya Mbambabay ziwa Nyasa mkoani Ruvuma.

Mradi wa ujenzi huo unatarajia kuanza Julai 2023 na kwamba bandari hiyo itakuwa na hadhi ya kimataifa pia itakuwa ndiyo bandari kubwa kuliko zote katika ziwa Nyasa na kuufanya mji wa Mbambabay kuwa kitovu cha uchumi Tanzania.
 
Mkoa wa tatu kuchangia pato la taifa halafu unataka wasiuboreshe huo mkoa?
Umekuwa Mkoa wa 3 Kwa sababu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali.

Kwa nini hawafanyi hivyo Mikoa yote?
---

SERIKALI YASAINI MKATABA UJENZI BARABARA YA LAMI LUMECHA RUVUMA-KIDATU MOROGORO
Serikali kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS)imesaini Mikataba saba ya ujenzi wa barabara itakayo tekelezwa kwa miaka minne yenye thamani ya shilingi Trillion 3.7 yenye urefu wa kilometa 2035 kwa kiwango cha lami.

Mikataba hiyo imehusisha Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Mpepo – Londo – Lumecha/ Ruvuma, Arusha – Kibaya – Kongwa Construction Of Handeni – Kiberashi – Kijingu – Njoro – Olboroti Mrijo Chini – Dalai – Chambalo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida Igawa .

Nyingine ni Songwe – Tunduma Masasi – Nachingwea – Liwale Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti River – Lalago – Maswa Construction Of Mafinga – Mtwango – Mgololo ambapo kila mkandarasi anayehusika na mradi mkubwa, atakua na timu nne za ujenzi katika kutekeleza Mradi.

Akizungumza kwenye hafla hiyo Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mnyaa Mbarawa ameeleza kuwa Barabara hizo zitajengwa Kwa kutumia utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).
Prof.Mbarawa ameeleza kuwa barabara zitakazojengwa zitapita katika Mikoa13 na kufafanua kuwa Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea yenye urefu wa kilometa 435.8 inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo.

“Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma; Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale,”amesema

Aidha amefafanua kuwa katika Mradi wa Barabara ya Igawa – Tunduma (km 218) ambao utajengwa kwa njia nne (4), imepangwa barabara hiyo ifanyiwe usanifu na ujenzi utakaowezesha kuifanya njia moja kuwa ya malori tu, na yatatumia njia hiyo kwa kulipia pia, itajengwa barabara ya mchepuo (ByPass) ambayo itapita Nje ya Jiji la Mbeya.
 
Umekuwa Mkoa wa 3 Kwa sababu ya uwekezaji mkubwa wa Serikali.

Kwa nini hawafanyi hivyo Mikoa yote?

Hapa naona uwekezaji wa sehemu mbali mbali iliogusa mikoa tofauti sioni tatizo au shida yako ni ruvuma tu? Mara ngapi mikoa mingne inakula keki ya taifa na ruvuma iliachwa muda mrefu walikuwa hawana umeme wa uhakika mpaka magu alipowapelekea gridi ya taifa wakawa na uhakika na umeme kuna sehemu mlisemea hili?
 
Hapa naona uwekezaji wa sehemu mbali mbali iliogusa mikoa tofauti sioni tatizo au shida yako ni ruvuma tu? Mara ngapi mikoa mingne inakula keki ya taifa na ruvuma iliachwa muda mrefu walikuwa hawana umeme wa uhakika mpaka magu alipowapelekea gridi ya taifa wakawa na uhakika na umeme kuna sehemu mlisemea hili?
Hapa naona uwekezaji wa sehemu mbali mbali iliogusa mikoa tofauti sioni tatizo au shida yako ni ruvuma tu? Mara ngapi mikoa mingne inakula keki ya taifa na ruvuma iliachwa muda mrefu walikuwa hawana umeme wa uhakika mpaka magu alipowapelekea gridi ya taifa wakawa na uhakika na umeme kuna sehemu mlisemea hili?
Wala sijasema Kuna ubaya ila upendeleo umezidi..
Kwenye hii ramani hapa Chini Barabara zote unazoziona kubwa zimejengwa Kwa lami,zinajengwa na zingine soon zinaanza tena hata sio Barabara kuu..
Screenshot_20230703-102158.jpg
 
Mkoa wa 3 kwa kuchangia pato la taifa alafu unataka isijengwe barabara? Sasa Hilo pato la taifa litawezaje kukusanywa bila barabara na miundombinu?

Halafu ujue kuna makaa ya mawe mengi sana kule,utabebaje hayo makaa bila barabara au reli?

Tena ujue,mikoa ya kusini ilitengwa sana huko nyuma, kuanzia miaka ya nyerere waliwatenga watu wa ruvuma. Hio reli ya tazara Ilibidi ipite mbeya songea hadi mtwara Ambayo ni njia fupi kama wazambia walivopendekeza,lakini nyerere akaipeleka huko Dar es salaam.

Leo hii songea ina mzigo mkubwa wa makaa na chuma ludewa, serikali hawana jinsi Bali imewalazimu kujenga barabara. Wasipojenga barabara na reli,hayo makaa ya mawe na chakula watakibebaji?

Na isitoshe, sion cha maana walichojenga huko. Hicho ki airport ni kidogo na hakuna cold rooms za kuhifadhia mazao, na kumbuka ruvuma ni mkoa wa kilimo.Hata hospitali ya rufaa ya serikali hakuna huko,wanategemea ya wamisheni.

Na hakuna barabara ya kuunganisha na Nchi ya Mozambique. Ni vumbi tupu. Na umbali wa songea hadi mpaka wa Mozambique nilisikia ni kilometa 120.Sasa jiulize kuna barabara ngapi za lami za kuunga kenya na Tanzania, halafu fananisha na huko kusini ndio utajua jinsi mikoa ya kusini ilivoachwa kwa makusudi toka miaka ya nyerere.
 
Back
Top Bottom