Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,355
- 1,952
Mimi nafikiri matatizo ya nchi yetu ni makubwa kuliko tunavyofikiria. Yapo kila kona, si tu katika siasa. Kama daktari anaweza akamfanyia mtu upasuaji wa kichwa badala ya mguu, hivi jamani utasema hapo ni siasa tena? Very confusing! Hii dhana ya uwajiikaji itafika siku tutaielewa kweli katika nchi yetu? Yaani watu wamefanya kosa kama hili lakini bado Mkurugenzi yupo, wale madaktari wanaendelea na udaktari wao hivyohivyo!
Naomba wale wenye utaalamu wa mambo ya petition tuanzishe petition ya kutaka uongozi wa MOI na hawa madaktari waondoke haraka sana. Yes, this is more than ile issue ya Ukraine! Hebu na nyie someni hii habari, tafakari, usilie bali pendekeza hatua za kuchukua!
Aliyeumia mguu apasuliwa kichwa, wa kichwa apasuliwa mguu.
Na Jackson Odoyo
WAGONJWA wawili waliokuwa wamelazwa katika Taasisi ya Mifupa (MOI) Muhimbili wamefanyiwa upasuaji tofauti na matatizo yaliyokuwa yakiwasumbua.
Wagonjwa hao walifanyiwa upasuaji Novemba Mosi, mwaka huu kwa nyakati tofauti katika taasisi hiyo, ambapo aliyekuwa na matatizo ya mguu alipasuliwa kichwa na wa kichwa akapasuliwa mguu.
Mmoja wa wagonjwa hao Immanuel Didas, aliyeumia goti baada ya kupata ajali ya pikipiki hivi karibuni na kulazwa katika taasisi hiyo, alifanyiwa uchunguzi na madaktari kushauri kwamba afanyiwe upasuaji wa goti hilo.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida, wakati wa kumpatia huduma hiyo, madaktari waliohusika walimfanyia upasuaji wa kichwa badala ya goti.
Katika kile kinachoonekana kuchanganyikiwa kwa madaktari hao, mgonjwa mwingine, Immanuel Mgaya ambaye pia alilazwa MOI kwa matatizo ya kichwa na uchunguzi kubaini kuwa anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa kichwa, badala yake alifanyiwa upasuaji wa mguu.
Mwandishi wa Mwananchi alizungumza na ndugu wa wagonjwa hao kuhusiana na matatizo yaliyowafika ndugu zao wakati wanapatiwa huduma ya matibabu katika taasisi ambayo waliweka bayana magonywa yaliyokuwa yanawasumbua, lakini wakapata mshangao baada ya kutibiwa tofauti na matatizo yao.
Kaka wa Immanuel Didas, Sisti Marishay alisema mgonjwa wake alikwenda hospitalini hapo kwa matatizo ya goti baada ya kupata ajali ya pikipiki, lakini alipopigwa picha za x-ray hakuwa na matatizo katika mfupa ila kulikuwa na uvimbe kwa ndani ndipo madaktari wakashauri afanyiwe upasuaji ili kuuondoa.
Alisema katika hali ya kusikitisha madaktari hao walimfanyia upasuaji kichwani wakati alikuwa haumwi kichwa.
"Kilicho fanyika ni uzembe wa hali ya juu, kwa sababu mdogo wangu alikuwa anaumwa mguu na sio kichwa, wao wakamfanyia upasuaji wa kichwa na baada ya kutokea tatizo hilo, nilizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Profesa Laurent Museru ambaye alikiri kwamba kuna makosa yametokea hivyo wameamua kukaa na kuunda tume ya kuchunguza uzembe huo kisha watatoa taarifa baada ya wiki moja," alisema Marishay.
Marishay alisema kwa sasa hawawezi kuchukua hatua yoyote mpaka watakapo pata majibu ya tume iliyoundwa na taasisi hiyo kuchunguza suala hilo.
Ndugu mwingine wa Didas, Ludani Didas naye alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia uzembe huo uliofanywa na madaktari hao kwa sababu mpaka sasa mdogo wake amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU).
"Mpaka dakika hii mdogo wangu hajitambui, hawezi kuzungumza chochote na yuko ICU, sasa mimi nitazungumza kitu gani, tusubiri nione hatima ya afya yake ndipo nitazungumzia uzembe huu wa wazi kabisa tena kwa wanyonge," alilalamika.
Naye mama mzazi wa Immanuel Mgaya aliyefanyiwa upasuaji wa mguu badala ya kichwa, Mary Mgina akiwa kwenye Wodi na 17, Sewahaji alimolazwa kijana wake, alisema alifika hospitalini hapo akitokea Njombe, mkoani Iringa wiki iliyopita.
"Tulikuja wiki iliyopita tukitokea Njombe katika Hospitali ya Kibena ambapo walituandikia barua kuja hapa kwa matibabu zaidi ya kichwa kilichoanza kumuuma ghafla siku chache baada ya kuanza mitihani ya kidato cha nne akiwa kwenye chumba cha mtihani," alisema Magina.
Alisema kutokana na tatizo hilo alishindwa kuendelea na mitihani kutokana na kuendelea kuumwa kichwa huku akianguka na kupoteza fahamu, ndipo akahamishiwa MOI ambako baada ya kumchunguza waliamua apasuliwe kichwa ila hawakumweleza ugonjwa unaomsumbua," alisema mama huyo.
Mjomba wa Mgaya, Dick Magina alisema baada ya kufanyiwa upasuaji huo walikabidhiwa mgonjwa aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa, lakini hakuwa ndugu yao na walipomkataa walianza kumtafuta na walipompata wakakuta amefanyiwa upasuaji wa mguu na si kichwa.
"Walinikabidhi mgonjwa mwingine tofauti na ndugu yangu nikawakatalia ndipo wakaanza kumtafuta na kumpata akiwa amepasuliwa mguu. Kilicho nishangaza zaidi ni kwamba tangu walipogundua kwamba wamefanya makosa hayo hawajafika kumuona mgonjwa ili wajue anaendeleaje," alisema Mgina na kuongeza;
"Kutokana na uzembe huo uliofanyika tunahitaji matibabu kwa mgonjwa wetu tena kwa gharama zao, pia nimehuzunishwa sana kutokana na makosa yaliyofanyika na hasa kwa wenzetu ambao mgonjwa wao amefanyiwa upasuaji wa kichwa badala ya mguu na hali yake ni mbaya," alisema.
Baadhi ya madaktari na wauguzi wa Muhimbili waliozungumza na mwandishi wa Mwananchi kwa njia ya simu kwa nyakati tofauti jana kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walidai kuwa uzembe kama huo ni wa kawaida hospitalini hapo.
Walidai kuwa madaktari wengine baada ya upasuaji wanaacha vipande vya pamba, nyembe na hata mikasi ndani ya mwili wa mgonjwa, lakini hufanywa kwa siri na mgonjwa anapofanyiwa upasuaji upya huwa haambiwi sababu ya kumpasua tena.
Baadhi ya wogonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo walidai kuwa uzembe kama huo ni wa kawaida kufanyika hospitalini hapo na kudokeza kwamba, hata akina mama wanaojifungua wengine hupewa watoto ambao si wao na wengine huambiwa uwongo kwamba mtoto amefariki muda mfupi baada ya kuzaliwa.
Naye Profesa Museru alikiri kuwepo kwa madai hayo na kusema kwamba, amesikitishwa na tukio hilo na kwamba aliamua kufikisha taarifa hizo wizarani.
Profesa Museru alisema pia wameunda tume ya kuchunguza madai hayo ambayo itaanza kazi leo na kutoa majibu kesho kutwa.
"Ni kweli kuna tukio la aina hiyo hapa hospitalini, lakini kuna taratibu nimeanza kuzichukuwa na sasa hivi ninapozungumza nawe nipo kwenye kikao cha kuunda tume ya kufuatilia na siwezi kukiri au kukataa kuwa ni uzembe, ndiyo maana tunaunda tume ya kuchunguza suala hilo na pia nimeishapeleka taarifa wizarani," alisema Profesa Museru.