Inawezekana matatizo ya nchi ni makubwa kuliko tunavyodhani: Immanuel Didas, apasuliwa kichwa badala ya mguu MOI

Hata kama haya makosa yanatokea kwa wenzetu atleast people are held responsible na hatua zinazotakiwa zinachukuliwa. Hawa wa huku kwetu wataunda tume and nothing will happen wataendelea kutesa watu tu. kumchukulia mtu hatua baada ya kufanya makosa makubwa kama haya kunawafanya hata wengine wawe makini zaidi kwa sababu wanajua wakikosea na tena kama ni uzembe adhabu ipo, lakini wengi wao wanajua hamna adhabu yeyote ile inayotolewa kwa hiyo they dont even make an effort kupunguza uzembe.

I think hawa wandugu wajaribu kutafuta legal advice na hawa wazembe wachuliwe hatua kali sana
 
Na hili ni ambalo limeripotiwa. Vipi kuhusu mamia ya kesi ambazo haziripotiwi? Mhhh mambo mengine nadhani hata shetani akiona watu tukiyafanya huwa anafumba macho kwa aibu!
 
Mimi nadhani hawa madaktari wamezidi kuwa walevi ndio maana wanafanya vitu vya ajabu, kuna umuhimu wawe wanapimwa kabla hawajafanya operations..ni watu wa kukesha vilabuni,mpaka na akili zao zinalewa.

sasa na huyo mkurugenzi anaunda tume ya nini wakati Facts zote ziko wazi?This country bwana!
 
Duh I have never seen such negligence nadhani hii imepita hata ile cheki ya Kikwete. Hivi ni kweli au mnatania jamani? Hii nigligence ni ya hali yajuu kweli kama ni matatizo tunayo sijui hii watu wa vyombo vya magharibi wakiikamata itakuwa je. Ndio maana wenzetu huwa wanatudharau tuko kama tunatumia sijui nini kufikiria. Mimi naona jamaa aliesema tuko less inteligent alikuwa sahihi na naamini angepatiwa Nobel prize ya pili. Yaani mtu unapasuliwa kichwa wakati huna tatizo la kichwa? Hawa ndio wasomi wetu je ambao hawajaenda shule watafanya nini?

Cheza na kila kitu lakini usicheze na mwili au maisha ya mtu. Hawa jamaa wanatakiwa wasimamishwe kazi mara moja wanyang'anywe lesseni zo na wapelekwe mahakamani kwa kosa la kujeruhi. Naamini maisha ya watanzania wengi yanatokana na uzembe wa madakitari wetu.Utaenda kupima ngoma wakuambie unayo kumbe huna, mke wako anaweza jifungua ukapewa mtoto wa wengine. Nimeogopa kabisa wakuu duh hii kali Haki ya Mungu tumekwisha maana kila pande inatugeuka nadhani tunamatatizo ambayo mizizi yake ni mirefu.

Binafsi sijawahi kutibiwa Muhimbili, kwa hiyo sijajua 'kunguni' wa pale wanafananaje. Ila hii hainifanyi nikadharau na kupuuzia hiki kilichoandikwa hapa. Huenda hali ni mbaya kweli.
 
Jamani Hii Nchi Yetu Inaenda Wapi Sasa????? Hivi Mambo Kama Haya Yakitokea Nchi Za Watu Kama Marekani Huwa Kwanza Kabisaaa Daktari Huyo Ananyang'anywa Leseni Kabisa, Asimtibu Haya Paka! Pili Kinachofuatia Hapo Huwa Ni Mgonjwa Au Ndugu Zake Kumshitaki Daktari Huyo...na Pesa Zitamtoka Hadi Afilisike (kwa Ma-lawyer, Na Pia Kumhudumia Mgonjwa Huyo Alomfanyia Viroja), Tatu Huwa Ni Kufikishwa Mbele Ya Vyombo Vya Dola, Na Daktari Huyo Anaweza Kufungwa, Mwisho Ni Hiyo Hospitali Pia Inashtakiwa Kwa Kuajiri Madaktari Wasostahili Na Kuachia Hayo Mambo Yatokee. Kila Mmoja Anawekwa Kuwa Responsible. Hivyo Bwana Kwenye Nchi Kama Marekani Na Za Ulaya, Madaktari Huwa Makini Sana, Na Hospitali Zonazowaajiri Huwa Makini Mara Mbili Zaidi Yao Ili Kuepuka Mambo Kama Haya!

Sasa Basi Tukirudi Kwenye Nchi Yetu Bongo.....mambo Hayo Yanatokea Kwa Sababu Hakuna Dedicatation, Na Standard Zetu Ni Za Chini Mno! Yaani Ina Maana Huyo Dk Hakusoma Hata Historia Ya Mgonjwa Kabla Kumtia Kisu Jamani?

Hiyo Petition Jamani Tufanye Na Tuisaini Ili Hawa Madaktari Wachukuliwe Hatua....and Please Lets Not Even Condider Hiyo "tume Ya Uchunguzi"...we All Know What The Outcome Is Going To Be...always The Same....no Problem. Wazungu Wana Msemo Wa Kutucheka Waafrika..."tia", Manake "this Is Africa"...anything Is Possible With Money! Let's Prove This Joke Wrong For Once!
 
Hali inatisha sana nchini kwetu.
Hivi mafaili ya wagonjwa huwa yanaachwa wodini wakati wa mtu kuwa operated?
NI kazi ya daktari kukariri matatizo ya mgonjwa wake?
Na je operation ilifanywa na daktari mmoja au madaktari tofauti?

Hiyo tume ya kuchunguza ilitakiwa kufanya kazi wakiwa ofisini au walipaswa kuwekwa pending kwanza?

Tunakoelekea hatukujui!
 
Naam, kama wengine walivyosema nami napigilia msumari kwamba lipo tatizo kubwa sehemu mbalimbali katika nchi yetu. Madaktari ni sehemu ndogo tu ndani ya mfumo wetu ingawa wao wanagusa moja kwa moja uhai wetu.

Turudi nyuma kidogo, utagundua kwamba hapo kabla madaktari walifungwa na professional zao zaidi kuliko personal gains. kumbuka kwamba hawa ndiyo wasomi waliobobea katka fani zao. uwiano mchafu wa kipato uliokuja baadaye hasa baada ya mfumo wa siasa za Azimio la Arusha kuisha, kulibadilisha kabisa ethics za wataalamu wetu, si mahospitalini peke yake, lakini wahasibu, wahandisi, maafisa kilimo, waalimu n.k wote wakabadilika kutoka kutoa huduma na kuwa wafanyabiashara.

Sababu kubwa ni kwamba, wakati wa transition ya mfumo athari zake kwa jamii hazikutiliwa maanani. ghafla tuliona wanasiasa wakipaa kwa utajiri wa kupindukia na kuwaacha wasomi wataalamu wetu wakiwa hohe hahe. kilichotokea kila mtu kwa nafasi yake akaamua ajianzishie miradi yake kando ya ile ya ofisi. Madaktari wakaanzisha hospitali zao, Wahandisi na wahasibu wakawa na zile consultant offices na wengine ndio hao unawaona kwenye siasa ili mradi kila mtu akatafuta uwiano wa kimapato kulingana na taaluma yake.

Athari zake zinaonekana, hakuna concetration. Daktari anafanya haraka ili amalize haraka awahi hospitali nyingine ambako pia anasubiriwa. Mwalimu anabrashia wanafunzi ili baadaye waende kwenye tuition yake n.k. Sote tunafahamu daktari mmoja bingwa kwa siku anaweza kuzunguka hospitali zaidi ya tano. ukitaka utibiwe vizuri labda uende kwenye kijiwe chake na huko utakoma mwenyewe kwa gharama yake.

Kazi ipo na ni pevu kuwarudisha wataalamu wetu kwenye ethics za taaluma zao. sawa na wanasiasa sasa hivi kuwaambia waache kununua Kura kutoka kwa wapiga kura. Sawa na kuwaambia wabunge wapunguze mishahara yao ili tuwe na uwiano sawa na wataalamu wetu.

Tukitibu ugonjwa wa kujitajirisha miongoni mwa wanasiasa wetu kwanza, nadhani pia itakuwa rahisi kutibu ugonjwa wa wataalamu wetu kajali fedha badala ya huduma.

This is my opinion.
 
Hii Hatari sana Jamani....Wazir Mkuu Tusaidie au upo Busy na Kumrudisha Mrema Kundini?
Hapa kama ingalikuwa ni viongozi wa serikali nafikiri Hii tume ingekuja baada ya hawa wazembe kufukuzwa.
Mie Nimekuwa najiuliza kwani ndugu wa hawa jamaa hawakushirikishwa na kutia sign kabla ya operations? lkn pia niungane na mwenzangu alieuliza huyu aliekuwa anaumwa Mguu hakujua nini kinafanyika?...Tuna kazi hadi tufike tunapokutaka.... au walidai RUSHWA kabla ya Operation? maana kila mmoja anataka utajiri wa FASTER FASTER? utajiri wa faster ndio unaofanya mtu aibe, apore, anyang'anye akabe, adhulumu mwisho AUE kabisaa...
 

Attachments

  • Mrema.jpg
    Mrema.jpg
    83 KB · Views: 38
Sasa jamani hii bodi ya madaktari inafanya kazi gani?au inawaorodhesha tu kujua idadi yao basi?Hili ni kosa la kiufundi moja kwa moja,kilichotakiwa hapa,hao madakitari wawe wamesimamishwa mara moja.Halafu na hizo tume ndio zifanye kazi.Pia naomba wanasheria watuelimishe haki zetu katika mambo hayo.Hili ni moja tumelisikia,lakini yako mengi sana ya kusikitisha yanatokea sehemu mbali mbali za nchi yetu.Ikitokea sana sana utasikia watu wakisema ingekuwa Ulaya lazima hatua fulani ingechukuliwa,kama kama vile fidia kwa muathirika n.k.
 
Hili lingetoke huku Majuu haya yangeshafanyika

1. Hospitali husika ingeamuriwa kusimamisha huduma za upasuaji with immediate effect.

2. Kikosi chenye mchanganyiko wa watafiti, watawala, wafanyakazi wengine wa umma kingetumwa kutoka wizara ya afya, bodi ya madaktari na hospitali nyingine bingwa kukagua taratibu zinazofuatwa katika huduma za upasuaji, ikiwa ni pamoja na kungalia makosa yalitokea wapi.

3. Baada ya uchunguzi wao wangewakisha ripoti yao kwa waziri wa afya na bodi ya madaktari. Ndani ya hiyo ripoti kungekuwa pamoja picha kamili ya nini kilitokea na nini kifanyike kuzuia makosa kurudiwa.

4. Then, waziri kwa kushirikiana na bodi ya madaktari wangeweka kwenye mizani mapendekezo ya bodi na kufuatilia/kusimamia utekelezaji wake.


Kwa Tanzania kilichofanyia ni Mkurugenzi kusema wanafanya uchunguzi...
 
Makosa kama hayo ni ya kawaida sana mahospitalini worldwide, hasa pale kunapokosekana protocol ya kueleweka ya jinsi gani mambo yafanyike.
Mwaka jana mwezi kama huu ktk hospitali ya Milford, Massachussetts, a small town maili chache nje ya Boston... mama mmoja ilikuwa afanyiwe cholecystectomy tena laparascopic (yaani operation ya kuondoa gallbladder kwa kutumia kamera). Badala yake surgeon akapasua na kuondoa Kidney, yaani surgeon akajagundua hilo kosa baada ya kupata phone call toka kwa pathologist, kwamba "hizi tissues ulonitumia mbona kama za kidney??," Ndio ikawa toba............doctor alikuwa suspend wakti wa investigation, latest ni kwamba anafanyakazi ya upasuaji lakini under supervision.
Huku protocol ni kwamba kunakuwa na checks, double checks na crosschecks over and over again kabla ya surgery au hata nurse kugawa dawa wodini. Lakini haina maana kwamba hakuna makosa!!, ila inasaidia sana kwani ni machache na kama yakitokea basi ni uzembe wa hali ya juu!!. Yani hawa jamaa inafikia point baadhi ya hospitali utakuta sehemu ambayo itafanyiwa upasuaji imechorwa/kuandikwa na marker pen kwamba "this is the right arm, leg or whatever." Cha muhimu sana ni protocols, ambazo lazima zifuatwe na atakaye shindwa au kupuuza basi out of the door he/she goes!!!.


i) unalinganisha pua na miguu, wapi na wapi? Huyu alitakiwa afanyiwe operation ya mguu akafanyiwa ya kichwa, yaani bado wewe unaona akili ipo? Mguu na kichwa unalinganisha na kukosea kati ya kidney na gallbladder au biology yako namna gani?

ii) muhimu zaidi: hatuwezi kuhalalisha ushenzi kwa sababu eti ushenzi huo umewahi pia kufanyika America, huu uwendawazimu tulishaukataa humu sana. Naomba jamani tuache kabisa hii tabia ya kuhalalisha makosa yanayofanyika katika nchi yetu kwa kigezo kwamba makosa kama yaliwahi kufanyika America au nchi zingine zilizoendelea, huo pia ni uzembe na ufisadi wa aina yake, tena tukome kabisa!
 
Kibaya zaidi sio wahusika hawatochuliwa hatua bali hata ile kusema samahani hawatofanya as if nothing wrong has happened and business as usual, at best wahusika "watahamishiwa" wizarani kwenye ulaji zaidi
 
Jamani makosa ya namna hiyo yanatokea, siyo Tanzania tu bali hata huku majuu. Mojawapo ya makosa ya namna hiyo ni yale yanayotokana na kuangalia vibaya X-ray.. ndiyo maana kwenye hospitali nyingi hapa siku hizi ile exray yenyewe inaoneshwa upi ni upande wa kushoto na upi ni wa kulia, (au juu na chini).

Nimeweka hapa chini document inayohusu medical errors: na pia unaweza kujisomea hapa chini kuelewa kuwa makosa ya namna hii hutokea hata katika nchi zilizoendelea sana na ambazo tunaweza kusema hazistahili makosa ya namna hii. Kwa upande wetu nadhani makosa ya naman hii (sijui kama kuna takwimu inayofuatilia) si mengi sana kwani bado tunategemea wanadamu zaidi kuliko mashine!

MAKOSA YA KITABIBU
 

Attachments

  • common_medical_errors.pdf
    178.7 KB · Views: 39
Jamani makosa ya namna hiyo yanatokea, siyo Tanzania tu bali hata huku majuu. Mojawapo ya makosa ya namna hiyo ni yale yanayotokana na kuangalia vibaya X-ray.. ndiyo maana kwenye hospitali nyingi hapa siku hizi ile exray yenyewe inaoneshwa upi ni upande wa kushoto na upi ni wa kulia, (au juu na chini).

Nimeweka hapa chini document inayohusu medical errors: na pia unaweza kujisomea hapa chini kuelewa kuwa makosa ya namna hii hutokea hata katika nchi zilizoendelea sana na ambazo tunaweza kusema hazistahili makosa ya namna hii. Kwa upande wetu nadhani makosa ya naman hii (sijui kama kuna takwimu inayofuatilia) si mengi sana kwani bado tunategemea wanadamu zaidi kuliko mashine!

MAKOSA YA KITABIBU


Mzee Mwanakijiji

Umesoma hoja ya Kitila hapo juu?
X-Ray ya kichwa ichanganywe na X-ray ya mguu??!!!..Upande wa kushoto na wa kulia, au wangechanganya mguu wa kushoto na kulia...lakini kichwa na mguu.

Halafu, huoni kama matatizo kama hayo yameshatokea sehemu nyingine duniani ingekuwa ni fundisho huku kwetu yasitokee kabisa?
 
....walipe tuu au waende jela,mambo kama haya wenzetu waliyaona zamani ndio maana Dr kufanya kazi huku lazima uwe na insurance na hapo inakufanya uwe makini zaidi na upuuzi kama huu unalipwa na insurance ukishinda kesi na Dr ukiwa mzembe mzembe nobody is goin to insure you that means no no insurance no job.
 
Jamani makosa ya namna hiyo yanatokea, siyo Tanzania tu bali hata huku majuu. Mojawapo ya makosa ya namna hiyo ni yale yanayotokana na kuangalia vibaya X-ray.. ndiyo maana kwenye hospitali nyingi hapa siku hizi ile exray yenyewe inaoneshwa upi ni upande wa kushoto na upi ni wa kulia, (au juu na chini).

Nimeweka hapa chini document inayohusu medical errors: na pia unaweza kujisomea hapa chini kuelewa kuwa makosa ya namna hii hutokea hata katika nchi zilizoendelea sana na ambazo tunaweza kusema hazistahili makosa ya namna hii. Kwa upande wetu nadhani makosa ya naman hii (sijui kama kuna takwimu inayofuatilia) si mengi sana kwani bado tunategemea wanadamu zaidi kuliko mashine!

MAKOSA YA KITABIBU

Sawa, ajali hutokea lakini hazikubaliki. Tena zile zinazowezekana kuzuilika kiurahisi. Na hata kama zinatokea majuu hiyo haihalalishi kutokea sehemu zingine. Hata huko majuu zinazotokea si kwamba zinakubalika kwani watu huwajibishwa!!!
 
Serikali yaingilia kati upasuaji wa ajabu hospitali kuu Tanzania
Na Jackson Odoyo (Mwananchi)

SERIKALI imeiagiza tume iliyoundwa kwa ajili ya kuchunguza tukio la wagonjwa wawili kufanyiwa upasuaji tofauti na matatizo yao katika Taasisi ya Mifupa (MOI).


Hatua hiyo inalenga kuiwezesha kuchukua hatua zinazotakiwa kama kuna watu watabainika kuhusika na tukio hilo ambalo siyo la kawaida.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi ofisini kwake jijini Dar es Salaam jana, Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa alisema serikali haiwezi kupuuza tukio hilo ndiyo maana inahitaji kufahamu ukweli.


Dk Mtasiwa alifafanua kwamba, wananchi wanahitaji kufahamu ukweli juu ya tukio hilo ili waweze kuwa na imani na madaktari wa taasisi hiyo mbalimbali hapa nchini hivyo ni lazima hatua za dharura zichukuliwe ili kuharakisha utoaji wa majibu ya uchunguzi huo.


"Tunaitaka tume ifanye kazi hiyo haraka na kutuletea majibu kisha tutatoa tamko mara moja iwezekanavyo," alisema Dk Mtasiwa.


Alisema kuna kanuni zilizowekwa kitaalam kabla ya kumfanyia mgonjwa upasuaji, lakini siku hizi watu wamezoea kufuata njia za mkato badala ya kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa kitaalam, kwa ajili ya upasuaji ama matibabu mengine.


"Siku hizi watu wamezoea kufanya kazi kwa mazoea badala ya kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa kitaalam kwa ajili ya upasuaji kabla na baada na wakati mwingine hata kwa matibabu ya kawaida," aliongeza.


Hata hivyo, alisema inapotokea tatizo lolote kwa upande wa afya, kuna njia tatu ambazo wasimamizi wa vitengo na vituo vya afya wanatakiwa kufuata kabla ya kuchukua hatua yoyote, ikiwemo ya kutoa taarifa wizarani.


Dk Mtasiwa aliongeza kuwa njia ya pili ni kuwasilisha taarifa yao baada ya kufanya uchunguzi wa tatizo hilo na bodi yao ya wakurugenzi ndiyo itakayopeleka taarifa hiyo wizarani kisha wao watakaa na kuamua hatua za kuchukua.


Alisema kwamba hatua ya tatu ni baraza la madaktari, ambalo pia litakaa na kutoa taarifa yake kutokana na uzito wa tukio sanjari na sababu zilizochangia tukio hilo.


Aliwaomba wananchi pamoja na ndugu wa wagonjwa hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho inashugulikia suala hilo kwa karibu zaidi hata hivyo hakutaka kuweka wazi hatua zipi watachuwa.


Mbali na serikali kutoa tamko hilo, baadhi ya madaktari bingwa nao wameonyesha kushangazwa na sakata hilo na kuhoji usimamizi wa kanuni za kitaalamu baada ya kutokea matukio kama hayo.


Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Profesa Leonard Lema, aliwataka wakuu wa idara zote za afya hapa nchini kuwa makini wakati wa kuhudumia wagonjwa kwa sababu wanafanya kazi ya kuokoa maisha ya binadamu.


"Napenda kuwaagiza wakuu wa idara zote za afya hapa nchini kuwa makini wakati wa kutoa matibabu ya aina yoyote kwa wagonjwa, vinginevyo watakutana matatizo kama haya kila wakati," alisema Profesa Lema.


Naye Kaimu Afisa wa Uhusiano wa MOI Mary Ochieng, alisema tume hiyo iliyoundwa ni ya watu sita na inategemewa kufanya kazi yao haraka na kutoa majibu ya uchunguzi huo.


Ochieng alisema wagonjwa hao hawataweza kufanyiwa upasuaji wa matatizo yao kwa sasa kwani bado wana uguza majeraha walinayo na kuongeza kwamba, hata watakapofanyiwa upasuaji tena hawatagharamia.


"Tume ni ya watu sita na wameshaanza kazi ya kuchunguza tukio hilo na hata wagonjwa hao pia hawataweza kufanyiwa upasuaji wa matatizo yao kwa sasa kwani bado wanauguza majeraha, hata watakapopona MOI itagharamia matibabu yao,"alisema Ochieng.


Hata hivyo, mwandishi wa habari hizi pia alizungumza na baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji kutoka MOI na MNH ambao waliomba majina yao yasindikwe gazetini.


Wataalam hao walisema madaktari waliohusika katika tukio hilo ni kati ya madaktari bingwa wa upasuaji walipo katika taasisi hiyo ambao pia ni wa siku nyingi, lakini hawaelewi mazingira ya tukio hilo.


Kwa sababu kanuni za upasuaji ziko wazi na baadhi ya kanuni hizo zinasema kwamba, ili mgonjwa afanyiwe upasuaji kuna hatua tatu ambazo zinapitiwa na watu sita.


Hatua ya kwanza, ni kuanzia wodini ambako mgonjwa anatolewa kwenda wodi ya upasuaji akiwa na wauguzi wawili, jalada lake na picha ya x-ray inayoonyesha tatizo linalo msumbua.


Hatua ya pili, ni kumkabidhi mgonjwa katika chumba cha upasuaji ambapo pia kuna wauguzi wawili ambao wanahakikisha kwamba mgonjwa huyo ameambatana na vibali vyake vyote na kuhakikisha kwamba ndiye anatefanyiwa upasuaji huo.


Tatu, ni kukabidhiwa kwa madaktari wawili waliopo katika chumba cha upasuaji ambapo mmoja ni daktari wa kumchoma mgonjwa sindano ya usingizi na daktari ambaye atafanyakazi ya kumpasua baada ya kuhakikisha kwamba huyo ndiye mgonjwa wake.


"Kwa kufuata baadhi kanuni hizi huwezi kufanya kosa kubwa kama hilo, sisi tuna maswali ya kujiuliza kwamba kwanini tukio kubwa kama hili litokea kama kweli watu wote hawa walifuata hatua hizo," alisema mmoja wao.


Sakata hilo la upasuaji wa aina yake uliofanyika Novemba mosi katika MOI, umefanywa kwa wagonjwa Emmanuel Didasi na Emmanuel Mgaya.


Kati ya wagonjwa hao, Didasi alipata ajali ya pikipiki na kutakiwa kufanyiwa upasuaji wa goti lakini akafanyiwa upasuaji wa kichwa na Mgaya aliyetakiwa kupasuliwa kichwa alipasuliwa goti.


Mpaka sasa aliyepasuliwa kichwa hali yake si nzuri kwa hajitambua na amelazwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)
 
i) unalinganisha pua na miguu, wapi na wapi? Huyu alitakiwa afanyiwe operation ya mguu akafanyiwa ya kichwa, yaani bado wewe unaona akili ipo? Mguu na kichwa unalinganisha na kukosea kati ya kidney na gallbladder au biology yako namna gani?

ii) muhimu zaidi: hatuwezi kuhalalisha ushenzi kwa sababu eti ushenzi huo umewahi pia kufanyika America, huu uwendawazimu tulishaukataa humu sana. Naomba jamani tuache kabisa hii tabia ya kuhalalisha makosa yanayofanyika katika nchi yetu kwa kigezo kwamba makosa kama yaliwahi kufanyika America au nchi zingine zilizoendelea, huo pia ni uzembe na ufisadi wa aina yake, tena tukome kabisa!

Wewe jamaa bwana,
Unani criticise kitu gani sasa? soma nilichoandika vizuri na uelewa......dizaini yako ndio watu mnaokatisha watu tamaa hapa hata kuchangia mawazo yao.
Its very clear kwamba hukuelewa post yangu na umekurupuka tu ku-criticise kwa masifa!!.
 

Mzee Mwanakijiji

Umesoma hoja ya Kitila hapo juu?
X-Ray ya kichwa ichanganywe na X-ray ya mguu??!!!..Upande wa kushoto na wa kulia, au wangechanganya mguu wa kushoto na kulia...lakini kichwa na mguu.

Halafu, huoni kama matatizo kama hayo yameshatokea sehemu nyingine duniani ingekuwa ni fundisho huku kwetu yasitokee kabisa?

Msee Yebo na Kitila,
Yaani mnaangalia issue complex kama hii ki-layman mpaka naona aibu yaani.........i wish mngekaa kimya. Kwa kifupi sio kama mnavyofikiria, ungepata bahati ya ku-spend few hrs in OR labda ungeelewa!!!.
 
Msee Yebo na Kitila,
Yaani mnaangalia issue complex kama hii ki-layman mpaka naona aibu yaani.........i wish mngekaa kimya. Kwa kifupi sio kama mnavyofikiria, ungepata bahati ya ku-spend few hrs in OR labda ungeelewa!!!.

...ebwana vipi game ya jana...? yaani nilifurahi ile kichizi...sasa hivi naona hamna atakayewasimamisha
 
Back
Top Bottom