Kuna ngazi ya maendeleo ambayo nchi hufikia ambapo sasa wananchi wenyewe wanaweza kujicontrol kama zilipofikia nchi zilizoendelea lkn hii ni hatua ya mbele kabisa!
Lkn asikudanganye mtu nchi zilizoendelea wote wanafanya population control sema mbinu tu ndiyo tofauti
kwa mfano nchi tajiri zote watoto wa kike hupewa birth control pills au vidonge vya kuzuia ujazito sasa maana yake nini?
Ni kwamba mtoto wa kike wa Ulaya, Marekani, Japani au nchi tajiri yoyote
hawezi kupata mimba ya bila kutarajia yaani kama atapata mimba ni kwamba ameamua kupata mimba na siyo bahati mbaya sisi kwetu hakuna hilo ina maana msichana yoyote yule anayelala na mwanaume ana hatari ya kupata mimba wakati wowote ule na ukiangalia takwimu za serikali wasichana wanaopata mimba bila ya kupanga yaani kuwa tayari kuwa na mtoto ni wengi sana jaribu kuangalia tu mtaani na hesabu wasichana waliozaa kabla ya wao kuwa tayari kuwa na familia au kijijni ukienda, sasa hii maana yake nini?
Ina maana huyu msichana kwanza hana elimu ya kumuwezesha kupata ajira yaani yeye mwenyewe bado hajaweza kujisimamia halafu tayari tena ana kiumbe ambacho anapaswa akihudumie sasa Umaskini utawezaje kuisha au kupungua hapo?!
Hivyo basi kwa kuwa sisi hatuna uwezo wa kuwapa wasichana wetu vidonge vya kuzuia mimba hatuna budi kutafuta njia mbadala, ili mtoto azaliwe tu na yule mwenye uwezo wa kumuhudumia na si vinginevyo!
Ukiangalia hiyo picha hapo chini utaona ninachoongelea, wapo wengi kama wangekuwa na vidonge vya kuzuia kupata mimba wengi wao wasingeamua kupata mimba!