Inawezekana Magufuli sio tatizo?

Inawezekana Magufuli sio tatizo?

Vile vitanda na mashuka walishahamishia kwenye hospitali zao;
Hii nchi ni kama ya wenda wazimu, linazuka hapo hapo na kuzimika na kusahaulika,
Waandishi wa habari bila bahasha hawawezi kufanya kazi, nao ni majipu pia.
 
Muhimbili ni kubwa sana,ni ukweli kuwa vitanda vilipelekwa kwa amri ya raisi ila ile ilikuwa wodi ya Wagonjwa wa moi,na Moi ina wodi mpya ndiyo iliyopelekewa vitanda vipya na wagonjwa waliolala chini wakahamishwa kwenye vitanda vipya.Wodi ya wazazi ya jana nayo ni jengo la zamani kidogo ila wagonjwa wamekuwa wengi kadiri miaka inavyoenda na kuna upungufu wa vitanda.Kwa ujumla magazeti yalitoa ripoti ya ushabiki kuwa MNH haina shida ya vitanda wakati hali halisi vitanda bado vinahitajika kwa hospitali nzima ili wagonjwa walale vizuri.
 
kinachotuumiza tanzania ni kuendekeza usiasa watu bado wapo kwenye kampeni ila wamesahau muda unasonga watakapo jitambua watakosa la kuwaambia watanzania haiwezekani muhimbili muhimbili rais akikaa ikulu ataenda muhimbili na waandishi wa habari kibao kwenda kushitukiza sasa me binafsi sielewi anaenda ku record au kushitukiza na mambo yalivyo kuigizana utasikia naibu waziri amepiga suti mpya anaenda kushitukiza na na waandishi wa habari fuso mbili
 
Ukinisoma vizuri sibishi kuwa Muhimbili ina matatizo
na mengine ya mda mrefu
mimi ninachopinga ni watu waliotuambia sasa Muhimbili mambo safi
baada ya ziara ya kwanza ya Magufuli...na vile vitanda vilivyo changishwa wabunge....
napinga hii hali kuonekana mpya wakati hii hali ipo kila siku

Labda mambo safi kwa kutegemea hali ilivyokuwa awali. Mimi ninaamini kuwa matatizo ya Muhimbili hayawezi kutatuliwa 'overnight', ni juhudi shirikishi zinahitajika kutoka kila pembe. Waandishi/media wawe wanajiongeza kwa kurudi eneo la tukio kutupa habari za yanayojiri bila kuongozana na hao viongozi.
 
Je kungekuwa hakuna mgonjwa mashuhuri wa kwenda kumjulia hali hapo hospital pangeendelea kubaki hivyohivyo bila kumulikwa?


Nani atamulika?
Nadhani ni muda sasa Wananchi nao watimize wajibu wao wa kuwa watoa habari. Social Media ziko kibao na mchina ametuwezesha na simu za bei poa na zenye camera na video! Muwe mnatupia mapicha mpago huu utasaidia.
Wanahabari kazi yao ni kuingiza pesa kama hakuna pesa kwao hiyo siyo habari kuu.

Ni wakati sasa kama kweli Ikulu inatamani ushiki wa wananchi kuna haja iwe na akaunti kwenye social Media kama Facebook au twitter kwa masuala yoyote yanayohusu issue kama hizi za huduma mbovu. Utaratibu huu wa taarifa kuwa one way hauwezi kutujenga na badala yake ni urasifu wa kuhabarishana. Maisha hata habari mbaya ni maisha! Bila habari mbaya au tukio baya Dunia kusingekuwa maendeleo.


Mfano.
Ministry of Natural Resources and Tourism - Tanzania

Hakimiliki © 2014. Blogu Rasmi ya Ikulu. Haki zote zimehifadhiwa.
 
Muhimbili ilijengwa mkoloni. population sasa ni kubwa kwa secta ya afya na miundombinu yake hata ukifanya nini idadi ya watu haitapungua Muhimbili cha msingi ni kuhamisha vitengo na kuvijenga upya nje ya lile eneo hii itapunguza population. Na hospitali za wilaya zijengwe upya kigamboni na ubungo kwa ajili ya hizo wilaya mpya
 
Vitanda siyo tatizo tena hilo lilishatatuliwa na viko vya kutosha tu ila tatizo ni nafasi utaviweka wapi?
Sehemu kubwa ya Wagonjwa wanaokuja Muhimbili hawakupaswa hata kuja Muhimbili bali kwa hali ya kawaida walipaswa waende kwenye Hospitali zao za Wilaya kama M'mala, Amana, Temeke na zinginezo lkn hizi zote zimetelekezwa kwa miaka mingi sasa huwezi kutegemea miujiza leo hii, hii sekta ya Afya ina changamoto kubwa sana na ndiyo wengine tunapinga kutumia fedha nyingi kujenga daraja la Kigamboni ambao halina umuhimu mkubwa kwa wakazi wa Dar badala hizi fedha zingeelekezwa kwenye mambo ya jamii kama Afya nina Imani Kigamboni wangepata Hospitali ya hadhi ya Amana, Tegeta wangepata, Tabata wangepata hii ingesaidia sana lkn Watz wenyewe wanataka Daraja Kigamboni wakapige picha!
Mkuu uliona habari vema ama unakurupuka tu. Nafasi ilikuwa ya kutosha sana ila vitanda havikuwepo vya kutosha na hoja yao haikuwa kuongenzwa kwa jengo bali upungufu wa vijana.
 
Mkuu uliona habari vema ama unakurupuka tu. Nafasi ilikuwa ya kutosha sana ila vitanda havikuwepo vya kutosha na hoja yao haikuwa kuongenzwa kwa jengo bali upungufu wa vijana.


Hilo ni swala la common sense tu hauhitaki kuona habari kujua kwamba tatizo la wagonjwa kulala chini Muhimbili halisababishwi na upungufu wa vitanda bali kuzidiwa kwa wagonjwa yaani kuna wagonjwa wengi kuliko uwezo wa Hospitali hiyo ndiyo sababu na siyo lazima uangalie TV ili ulishwe habari hii!
 
mtanichukia tu hii nchi ilikuwa inahitaji shuffle ya nguvu ndomana na sema Lowassa alistahilikuwa raisi wa hii nchi,samahani lakini kama ntakuwa nje ya mada..!!!Bado tunaongozwa na mihemko,mizuka yaani kwa mwanasiasa mjanja nikutengeneza awareness tu kwa wananchi wataacha kujadili yote ya maana watakimbila kudiscuss issue yako
 
Hizo hela za kurudia uchaguzi uliokuwa huru na wa haki bora wajenge hospitali kubwa nyingine.
 
Wewe hauna akili kwanza hiyo picha ni ya lini? Hiyo picha ni kabla ya Utawala wa Raisi Magufuli, sasa nakupa changamoto kapige picha kama hiyo kwenye Hospitali hapa Dar halafu ulete tena!
Ha haaa km watu wanaomsifia magufuli ni wa aina yako,nna uhakika tumepoteza tena fursa ya kuwa na kiongozi bora kwa miaka mingine 5. Yaani hata picha za jana unapingana nazo?? Yaani nyie mkwere ndiyo aliwaombea mfikiriwe??
 
tatizo majengo muhimbili ni machache,madaktari bigwa wote wanapelekwa muhimbili.kinacho takiwa kufanya na serikali ya CCM iwezeshe mazingira ya hospitali za wilaya na mikoa kwa kujenga hodi za kutosha na kusambaza madaktari bingwa wilayani
 
Basi waandishi msituwekee picha za nesi au paka kalalia kitanda wakati watu wagonjwa wawili wanalalia kitanda kimoja mbona hzo hamtuwekei magazetini?
 
Nimeona Azam two tv Magufuli mwenyewe kauliza kwa mshangao watu watano?
wakamjibu ndio
Fahamu kuwa vitanda katika hospitali zetu sio vya kulalia kama tunavyofanya sehemu nyingine, bali ni kujipumzisha au kukalia na mgonjwa akichoka analala chini.
 
Mimi kwa kweli sijawahi kuona serikali au viongozi wetu wanatatua tatizo likaisha sijui tatizo ni nini. Hata vitu vidogo vinawashinda uchafu tu unawashinda kusimamia.watajifanya wakali na vifaini siku mbili tatu uchafu upo palepale hakuna anayejali nao wanapita kila siku na wanaona.ukienda kwenye elimu shida watoto bado wana kaa chini hadi leo kuna shule za serikali mikoani hazina hata paa. Ukija ktk afya matatizo ni yale yale maisha yote.foleni maji ujambazi ufisadi hakuna kitu tunaweza kusema jamani hiki serikali imebadilisha na si tatizo tena.
Sasa ni nini kila kitu hawajawahi kuweza.


siku zote wanafanya zimamoto
hawamalizi tatizo
lakini team ya propaganda ya Magufuli mtandaoni waliaminisha watu
kuwa Muhimbili matatizo yamekwisha hadi jana walivyo umbuka
 
Matatizo katika sekta ya afya hayataisha kwa "ziara za kushtukiza" na maagizo au matamko ya wanasiasa hata siku moja!! Kama kweli tunataka mabadiliko yenye tija na ya kudumu katika hii sekta, kuna vitu vingi sana tunatakiwa kufanya!!
Haya mambo ya maagizo na ziara za ghafla zita achieve only a partial and superficial effect. Na muhimbili specifically, matatizo yake ni deep-seated. Tatizo sasa hivi ukiongea katika muktadha huo unaonekana mchawi tuu, kila mtu yuko "super-excited"The Boss

Hii ya kujitoa ufahamu na kujifanbya kila anachofanya Magufuli ndo muarobaini wa tatizo
slowly imeanza kutoweka.....very soon wtaanza kulialia hata wapambe
maigizo yanaanza kuwaishia now
 
Labda mambo safi kwa kutegemea hali ilivyokuwa awali. Mimi ninaamini kuwa matatizo ya Muhimbili hayawezi kutatuliwa 'overnight', ni juhudi shirikishi zinahitajika kutoka kila pembe. Waandishi/media wawe wanajiongeza kwa kurudi eneo la tukio kutupa habari za yanayojiri bila kuongozana na hao viongozi.

Waandishi wa Tanzania bila bahasha hawaandiki chochote
tungekuwa na waandishi wa kweli mbona haya yangekuwa all over news mapema
 
Ni nani amewaambia wananchi kwamba matatizo yametauliwa? Sijawahi kusikia mahali popote tangu Raisi magufuli aingie madarakani akisema kwamba matatizo ya Muhimbili au afya yametatuliwa hilo nalisikia kwako, nilichosikia ni kwamba hali imeboreshwa kulinganisha na ilivyokuwa hapo mwanzo kama ununuzi wa vitanda, mashine na upatikanaji wa dawa ktk MSD, lkn siyo kutatuliwa hilo sijawahi kulisikia!
Unacheza na maneno. Hayo uliyoandika ni sawa na kuwaambia matatizo yametatuliwa. Ukisoma taarifa zinazotolewa mwelekeo ni huo wa kuwaaminisha hivyo. Soma uhuru na habarileo la leo utaona ilivyoripotiwa ziara ya Mh Rais jana wodi ya wazazi utajua ninalolisema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom