The Boss, samahani sana naomba ruhusa nitoe summary ya michango iliyotolewa na watetezi wa
hapa kazi tu kuhusu hali ya Hospitali Kuu ya Muhimbili. Kwa sasa hawa ndio wanawakilisha
think tank ya status quo ambayo ilimwezesha Magufuli kuingia madarakani na hivi sasa naambiwa kuna mpango wa kuwapa tuzo. Haya tuendelee...
- Nkasumuni: Muhimbili ilijengwa na mkoloni. population sasa ni kubwa kwa secta ya afya na miundombinu yake hata ukifanya nini idadi ya watu haitapungua.
- Eli79: Naamini tatizo sio muhimbili kama taasisi, tatizo kubwa ni population ya wakazi wa Dar ukilinganisha na idadi ya hospitali zilizopo. Kama jiji lilikuwa designed kwa wakazi 2m na leo lina zaidi ya mara mbili ya watu, usitegemee kuwa kuna miundombinu itakayostahamili, sio barabara, maji wala afya.
- Barbarosa: Tatizo la Wagonjwa kushirikiana vitanda halisababishwi na uhaba wa vitanda, bali linasababishwa na uwingi wa wagonjwa na nafasi ni ndogo hivyo hakuna kitu Muhimbili wanaweza kufanya kwa maana hakuna nafasi sasa vitanda wataviweka wapi? Vitanda siyo tatizo tena hilo lilishatatuliwa na viko vya kutosha tu ila tatizo ni nafasi utaviweka wapi?
- Ruttashobolwa: Vitanda vilinunuliwa kwa ajili ya ward ya kawaida haikuwa ya wazazi...kwa hiyo swala la ward ya wazazi ni case mpya ambayo inahitaji ufumbuzi!
- Queen Esther: ili kuweka kumbukumbu vizuri. Vile vitanda vilitolewa general ward. Hapo mtu Wa kwanza kuwajibika ni Head Wa idara husika, mgt ya Muhimbili na wizara husika. Pia hivi kujifungua tuu mtu hana shida kwanini anaenda referees hosp Muhimbili?? Hawa madaktari husika nao napata shida kidogo.
- Barbarosa: Hilo siyo suluhisho la matatizo ya TanZania hata kama Serikali ikihamia Dom bado idadi ya watu itaendela kuongezeka Dar kwa maana Dar ndiyo mji tajiri TZ na utabakia kuwa hivyo, suluhisho hapa ni population control basi, hakuna lingine ni lazima Serikali ije na mpango wa kudhibiti uzaaji hovyo wa bila mpango!
- Judy wa Kishua: Kuna vingi vimefanyika hapo Muhimbili ila wenye nongwa wamesubiri kuona mapungufu ndio waje kuporomosha lawama kama kawaida yao ila likifanyika zuri hautakaa uwaone wakipongeza na pia awapendi kuona tunaappreciate chochote kizuri toka kwa Magufuli.
- donbeny: Muhimbili ni kubwa sana,ni ukweli kuwa vitanda vilipelekwa kwa amri ya raisi ila ile ilikuwa wodi ya Wagonjwa wa Moi, na Moi ina wodi mpya ndiyo iliyopelekewa vitanda vipya na wagonjwa waliolala chini wakahamishwa kwenye vitanda vipya. Wodi ya wazazi ya jana nayo ni jengo la zamani kidogo ila wagonjwa wamekuwa wengi kadiri miaka inavyoenda na kuna upungufu wa vitanda.
- Barbarosa (akikana picha iliyopigwa jana): Wewe hauna akili kwanza hiyo picha ni ya lini? Hiyo picha ni kabla ya Utawala wa Raisi Magufuli, sasa nakupa changamoto kapige picha kama hiyo kwenye Hospitali hapa Dar halafu ulete tena!
- Barbarosa: lazima Uchumi wetu ukuwe kuzidi ongezeko la watu ili ilete maana na hili kwa hali ya kawaida na ngumu hakuna nchi waliowahi kufanikiwa na ndiyo njia pekee ni kupunguza ongezeko la watu kwa mfano iwekwe utaratibu mwisho watoto wawili ambao Serikali inawalipia kila kitu na kila mtoto wa tatu au nne unamlipia mwenyewe na kodi unayokatwa inaongezeka hii itasaidia vinginevyo hakuna kitu tutafanya!
- Phillipo Bukililo: Tatizo letu Watanzania ni kufikiri kwamba kuna mtu fulani sehemu fulani mwenye wajibu wa kuyashughulikia matatizo yetu kwa mapana yake!. Serikali ni mimi na wewe, ni wewe na yule, ni kila mtu. Anatazamwa Magufuli na wasaidizi wake kama vile ni watu wametoka sayari nyingine kuja kutuondolea maelfu ya matatizo yetu. Kila mtu atambue kuwa yeye ni serikali.
- twahil: Mkuu hao vijana wasikuumize kichwa...luwasa ameishatangaza kuwania urais 2020 sasa wameishaanza kampeni hao...ila wasichojua ni kuwa wanapambana na kivuli chao...Magufuli ni namba nyingine. Ni aibu kuona kampeni ndio zimeisha ila watu wanaendeleza siasa badala ya kazi...ukiona hivyo jua watu hao hawako sawa yaani ni punguani....
- Barbarosa: nchi zilizoendelea wote wanafanya population control sema mbinu tu ndiyo tofauti kwa mfano nchi tajiri zote watoto wa kike hupewa birth control pills au vidonge vya kuzuia ujazito sasa maana yake nini? Ukiangalia hiyo picha hapo chini utaona ninachoongelea, wapo wengi kama wangekuwa na vidonge vya kuzuia kupata mimba wengi wao wasingeamua kupata mimba!
- ...
The Boss, sidhani kama kuna haja ya kuendelea zaidi, huu ni mfano halisi wa jamvi letu pendwa lilivyoshuka hadhi na taswira ya tunakoelekea. Fikiria jibu unaloweza kuwapa hao watu wa aina hii hapo juu likatosheleza, hakuna. Hawa si wa kukimbizana nao, unaweza kuta watu wanashindwa kuona tofauti kati yako na wao. Hawa ndio wamemwagwa mtandaoni eti kuitetea serikali ya Magufuli na kwa majibu wanayoyatoa unaweza kuona taifa linakoelekea.