Inawezekana Magufuli sio tatizo?

Inawezekana Magufuli sio tatizo?

Naamini tatizo sio muhimbili kama taasisi, tatizo kubwa ni population ya wakazi wa Dar ukilinganisha na idadi ya hospitali zilizopo.
Kwa sasa, hata uboreshe vipi muhimbili, temeke, amana na mwananyamala, bado huwezi ku accommodate wananchi wa jiji coz jiji limezidiwa katika mambo mengi.
Kama jiji lilikuwa designed kwa wakazi 2m na leo lina zaidi ya mara mbili ya watu, usitegemee kuwa kuna miundombinu itakayostahamili, sio barabara, maji wala afya.
Ijengwe hospitali nyingine pwani, yenye hadhi zaidi ya muhimbili ili kugawanya idadi ya wagonjwa wa jiji na wale wanaokuja kwa rufaa toka mikoa mingine. Otherwise tutafanya ziara za kushtukiza bila mafanikio yoyote.
 
Mkuu hili mbona tumelizungumza sana humu
lakini serikali imeweka pamba masikioni
hata foleni pia tatizo ni hili
lakini wanazidi kupanua barabara badala ya ku address hili tatizo
kila siku wanapanua Muhimbili
mara wanapanua bandari
mara wanapanua airport
utasema Dar ndo Tanzania
 
Yaani leo nimeshangazwa mno na sisi watanzania tulivyo

eti Magufuli anarudi pale pale kutoa ahadi ile ile na inakuwa ni 'new event'
yaani hata siku 100 hazijaisha....tushasahau

Wengine tulishasema hakuna jipya...ni more of the same.

Hivi hujawahi kuona baadhi ya hao viongozi wetu wakienda sehemu ati kuona na kujifunza kuhusu shida na matatizo yanayowakabili Watanzania?

Hivi kweli mtu anaweza kuamini kwamba huyo Magufuli alikuwa hajui matatizo yanayoikabili hiyo hospitali ya taifa na sekta ya afya kwa ujumla?

Hii hali ya wagonjwa kulala chini mbona sioni kilicho kipya.

Kuna picha nyingi tu miaka iliyopita ambazo zimekuwa zikizunguka kwenye mitandao zikionyesha hali halisi ya hospitali zetu.

Na kusema ukweli wala mtu huhitaji kuona picha ndo ushtuke kwamba kumbe kuna watu huwa wanalala chini mahospitalini.

Nenda tu mwenyewe hospitali na utajionea hilo.

Mimi mara kibao nimeshaona wagonjwa wakilala chini kwenye hospitali ya Somanda, Bariadi na hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Nakumbuka marehemu mzee wangu mwaka 1996 alipatwa na dharura ndogo akaenda Muhimbili na wakamlaza chini.

So what is new here?
 
Tatizo la Wagonjwa kushirikiana vitanda halisababishwi na uhaba wa vitanda, bali linasababishwa na uwingi wa wagonjwa na nafasi ni ndogo hivyo hakuna kitu Muhimbili wanaweza kufanya kwa maana hakuna nafasi sasa vitanda wataviweka wapi?

Changamoto kwenye sekta ya Afya kama kulivyo sehemu nyingine bado ni kubwa sana, ni lazima kwanza Hospitali zetu za Wilaya kama Amana, Temeke, Mwananyamala zote ziboreshwe na pia kujengwa nyingine zitakazoendana na idadi ya wakazi wa Dar, kumbuka Hospitali zote Dar zimejengwa wakati Dar ikiwa na wakazi chini ya milioni Moja leo hii tuko zaidi ya milioni 4.5 na kila mama anapata wastani wa watoto 2.6 Tanzania ambayo ni kasi kubwa sana!
Tatizo ni kuwaaminisha wananchi kuwamatatizo hayo yatatuliwa kirahisi na kesho yake unawaambia yametatuliwa kwa taarifa na kuweka picha magazetini! Ukichimbua rekodi za mkoloni utakuta kulikuwa na mipango ambayo ilikuwa ikizingatia kupanuka kwa MIJI yetu na kuongezeka kwa watu. Bahati mbaya sisi tuliachana na mipango tukaenenda bila dira na matokeo yake ni haya tunayoyaona kila sehemu.
 
Bossman,

Humu watu huwa tunapenda sana kumkejeli Lemutuz lakini kuna wakati aliwahi kusema kwamba 'viongozi wetu ni reflection yetu sisi wenyewe wananchi'.

Hiyo kauli ina ukweli mwingi sana ndani yake.

Cc: Nguruvi3
Ina ukweli kwasababu leo wamesahau Magufuli alimuondoa Mkurugenzi ili mambo ya nyooke.
Sasa hatujui atamfukuza na huyo aliyemweka yeye mwenyewe

Inaeleza tulivyo kwasababu leo wananchi wanazungumzia Mhimbili, hawajui ni changa ili kuondoa mjadala wa kukimbia mabalozi ambao hawana jibu.

Wakatumbukiza kitu na watanzania wanaona ni kipya, wamesahau mabalozi walioitwa nyumbani, mwenye nyumba akaondoka!
 
Wodi ya wazazi leo
 
Attachments

  • 1455126991467.jpg
    1455126991467.jpg
    24.7 KB · Views: 29
  • 1455127012965.jpg
    1455127012965.jpg
    21.8 KB · Views: 36
Tatizo ni kuwaaminisha wananchi kuwamatatizo hayo yatatuliwa kirahisi na kesho yake unawaambia yametatuliwa kwa taarifa na kuweka picha magazetini!
Na media yetu nayo
ya ajabu mno
Media inatumika kumpamba mwanasiasa
na leo bila aibu inaripoti upya matatizo yale yale
 
Tatizo kubwa ni Media ambayo ilichukua hili swala kwa utashi wa kutaka kuuza (kasi ya awamu mpya) wakati wakitoa matumaini hewa kwa wananchi."Muhimbili ile ileee "..sababu hata CT scan iliyoletwa kumbe ilikuwa ni ya Morogoro wamefanya kuhamisha tu.
Na CCM ni ile ile. Tulionya mapema sana kuhusu haya mambo. Leo kila mmoja anatahamaki.
 
Na media yetu nayo
ya ajabu mno
Media inatumika kumpamba mwanasiasa
na leo bila aibu inaripoti upya matatizo yale yale
Wakati anaingia madarakani hakuwa na waziri wala katibu mkuu

#Hapakazi inatakiwa ionekane kwa mkurugenzi, waziri wa afya
Alimuondoa mkurugenzi kwa uzembe aliouona leo. Tusubiri kama #Hapakazi ni for real au ilikuwa bangusilo tu
 
Hakuna kitu Muhimbili watafanya, hakuna nafasi wamezidiwa na wagonjwa sasa hivyo vitanda wataviweka wapi? Hilo ndiyo swali!
Imefika wakati sasa tuanze kuliangalia swala la ongezeko la watu , tunazaliana sana matokeo yake ndiyo hayo kila huduma hazitoshi!

Wangalau sasa utaanza kujibu kwa nidhamu, toka lile sakata la mkulu kukimbia mabalozi na.huu ukweli unaoendelea kuwa hadharani utawafanya muache kusifia kila kitu kwa itikadi ya kiccm. Tulisema haya mambo hayahitaji kupenda sifa bali kuchunguza hasa ni nini matatizo yetu na jinsi ya kuyatatua na sio kuita camera kuongopea umma eti sasa tumepata kiongozi muarubaini wa matatizo yetu. Tuache kupenda sifa kwa ajili ya maksi za kisiasa kwani tatizo ni kibwa kuliko kupenda sifa za kisiasa.
 
Kama wewe ni mzalendo utakubaliana nami Muhimbili kuna shida ya ki uongozi zaidi ya tunavyofikiri. Pia baada ya Mhe. Rais kumaliza awamu ya kwanza ilibaki waziri na timu yake kujipanga!!!!

Nimemkumbuka Ag. CEO Dr. Kidantu na issue ya ST SCAN mashine na mbwembwe za mstaafu Prof Museru!!!

Pia nikusaidie uweke kumbukumbu vizuri. Vile vitanda vilitolewa general ward. Hapo mtu Wa kwanza kuwajibika ni Head Wa idara husika, mgt ya Muhimbili na waizara husika.

Pia hivi kujifungua tuu mtu hana shida kwanini anaenda referees hosp Muhimbili?? Hawa madaktari husika nao napata shida kidogo.

Queen Esther

Correction: Pombe alikwenda Muhimbili kumjulia hali sheikh wa Bakwata aliyelazwa hapo, akiwa aneo la hospital kinamama wakamsonga na kumuomba akajionee mateso wanayopata wodi ya wazazi na akakuta hayo aliyoyakuta.

Je kungekuwa hakuna mgonjwa mashuhuri wa kwenda kumjulia hali hapo hospital pangeendelea kubaki hivyohivyo bila kumulikwa?

Yule waziri dr kilaza anayewahi asubuhi wizara ya afya na kufungia mageti wachelewaji yuko wapi?

Kinamama wanaolala chini hospital za huko Tandahimba watatuliwa tatizo lao baada ya nani kwenda hapo hospital au Pombe ni spiderman atakuwa anapaa hewani kukagua wodi zote tanzania?
 
Vitanda siyo tatizo tena hilo lilishatatuliwa na viko vya kutosha tu ila tatizo ni nafasi utaviweka wapi?
Sehemu kubwa ya Wagonjwa wanaokuja Muhimbili hawakupaswa hata kuja Muhimbili bali kwa hali ya kawaida walipaswa waende kwenye Hospitali zao za Wilaya kama M'mala, Amana, Temeke na zinginezo lkn hizi zote zimetelekezwa kwa miaka mingi sasa huwezi kutegemea miujiza leo hii, hii sekta ya Afya ina changamoto kubwa sana na ndiyo wengine tunapinga kutumia fedha nyingi kujenga daraja la Kigamboni ambao halina umuhimu mkubwa kwa wakazi wa Dar badala hizi fedha zingeelekezwa kwenye mambo ya jamii kama Afya nina Imani Kigamboni wangepata Hospitali ya hadhi ya Amana, Tegeta wangepata, Tabata wangepata hii ingesaidia sana lkn Watz wenyewe wanataka Daraja Kigamboni wakapige picha!
Unaposema hawakupaswa ulitaka waende wapi wakati hii ndiyo hospitali ya rufaa. Hata hao wanokwenda huko Mwananyamala, Amana na Temeke hawakupaswa kwenda huko, wangehudumiwa kwenye zahanati ambazo pia hazina vifaa wala wataalamu wa kuwatibu!
 
Tatizo ni kuwaaminisha wananchi kuwamatatizo hayo yatatuliwa kirahisi na kesho yake unawaambia yametatuliwa kwa taarifa na kuweka picha magazetini! Ukichimbua rekodi za mkoloni utakuta kulikuwa na mipango ambayo ilikuwa ikizingatia kupanuka kwa MIJI yetu na kuongezeka kwa watu. Bahati mbaya sisi tuliachana na mipango tukaenenda bila dira na matokeo yake ni haya tunayoyaona kila sehemu.

Ni nani amewaambia wananchi kwamba matatizo yametauliwa? Sijawahi kusikia mahali popote tangu Raisi magufuli aingie madarakani akisema kwamba matatizo ya Muhimbili au afya yametatuliwa hilo nalisikia kwako, nilichosikia ni kwamba hali imeboreshwa kulinganisha na ilivyokuwa hapo mwanzo kama ununuzi wa vitanda, mashine na upatikanaji wa dawa ktk MSD, lkn siyo kutatuliwa hilo sijawahi kulisikia!
 
Unaposema hawakupaswa ulitaka waende wapi wakati hii ndiyo hospitali ya rufaa. Hata haomwanokwenda huko Mwananyamala, Amana na Temeke hawakupaswa kwenda huk, wangehudumiwa kwenye zahanati ambazo pia hazina vifaa wala wataalamu wa kuwatibu!

Ninaposema hawakupaswa kwenda Muhimbili ina maana Muhimbili kama Hospitali ya Rufaa kwa hali ya kawaida inapswa kuhudumia wagonjwa tu wanaoletwa moja kwa moja ktk Hospitali nyingine kwa matibabu ya juu zaidi na siyo kila mama anayejifungua anakwenda Muhimbili au kila anayeteguka mkono anakwenda Muhimbili lkn kwa kuwa Hospt. zetu za Wilaya ziko chini ya kiwango basi tumaini pekee la wananchi lililobaki ni Muhimbili lkn haikupaswa kuwa hivyo!,
Ndiyo maana ya Hospitali kuitwa ya Rufaa yaani haunde mwenyewe bali daktari muhusika wa hospitali nyingine ndiyo alipaswa akupeleke Muhimbili kwa uchunguzi zaidi!
 
Hakuna kitu Muhimbili watafanya, hakuna nafasi wamezidiwa na wagonjwa sasa hivyo vitanda wataviweka wapi? Hilo ndiyo swali!
Imefika wakati sasa tuanze kuliangalia swala la ongezeko la watu , tunazaliana sana matokeo yake ndiyo hayo kila huduma hazitoshi![/QUO
Wangalau sasa utaanza kujibu kwa nidhamu, toka lile sakata la mkulu kukimbia mabalozi na.huu ukweli unaoendelea kuwa hadharani utawafanya muache kusifia kila kitu kwa itikadi ya kiccm. Tulisema haya mambo hayahitaji kupenda sifa bali kuchunguza hasa ni nini matatizo yetu na jinsi ya kuyatatua na sio kuita camera kuongopea umma eti sasa tumepata kiongozi muarubaini wa matatizo yetu. Tuache kupenda sifa kwa ajili ya maksi za kisiasa kwani tatizo ni kibwa kuliko kupenda sifa za kisiasa.
Mkuu hili mbona tumelizungumza sana humu
lakini serikali imeweka pamba masikioni
hata foleni pia tatizo ni hili
lakini wanazidi kupanua barabara badala ya ku address hili tatizo
kila siku wanapanua Muhimbili
mara wanapanua bandari
mara wanapanua airport
utasema Dar ndo Tanzania

Ni kweli ndigu, viongozo wetu wote wamekuwa kama wamelogwa huki wakijofanya wasomi.
Mkuu hili mbona tumelizungumza sana humu
lakini serikali imeweka pamba masikioni
hata foleni pia tatizo ni hili
lakini wanazidi kupanua barabara badala ya ku address hili tatizo
kila siku wanapanua Muhimbili
mara wanapanua bandari
mara wanapanua airport
utasema Dar ndo Tanzania

viongozi wamefikia mwisho wa kufikiri. wao wanaamini kila kitu ni Dar. Hamoshia serekali dodoma utaona jinsi gani jiji litaacha nafasi. ukiuliza kisa cha kitokuhamoa dodoma kwa serekali hakuna bali ni porojo tu
 
Wangalau sasa utaanza kujibu kwa nidhamu, toka lile sakata la mkulu kukimbia mabalozi na.huu ukweli unaoendelea kuwa hadharani utawafanya muache kusifia kila kitu kwa itikadi ya kiccm. Tulisema haya mambo hayahitaji kupenda sifa bali kuchunguza hasa ni nini matatizo yetu na jinsi ya kuyatatua na sio kuita camera kuongopea umma eti sasa tumepata kiongozi muarubaini wa matatizo yetu. Tuache kupenda sifa kwa ajili ya maksi za kisiasa kwani tatizo ni kibwa kuliko kupenda sifa za kisiasa.

Sielewi hata unachokiongea Raisi Magufuli bado mpaka sasa hivi anajaribu sana kutatua matatizo yaliyopo lkn peke yake hawezi anahitaji ushirikiano wetu sasa kama watu kama ninyi mmekaa na kutegea kusubiri wapi atateleza ili muanze kumuattack mnakosea sana na kama lengo lilikuwa kuingia madarakani kwa staili hiyo poleni sana kwani hamtafanikiwa kwa sababu Wananchi wote wanaona kwamba Raisi anajitahidi ingawaje ana kazi ngumu lkn anajitahidi na watampa ushirikiano!
 
Kama wewe ni mzalendo utakubaliana nami Muhimbili kuna shida ya ki uongozi zaidi ya tunavyofikiri. Pia baada ya Mhe. Rais kumaliza awamu ya kwanza ilibaki waziri na timu yake kujipanga!!!!

Nimemkumbuka Ag. CEO Dr. Kidantu na issue ya ST SCAN mashine na mbwembwe za mstaafu Prof Museru!!!

Pia nikusaidie uweke kumbukumbu vizuri. Vile vitanda vilitolewa general ward. Hapo mtu Wa kwanza kuwajibika ni Head Wa idara husika, mgt ya Muhimbili na waizara husika.

Pia hivi kujifungua tuu mtu hana shida kwanini anaenda referees hosp Muhimbili?? Hawa madaktari husika nao napata shida kidogo.

Queen Esther
natamani ungekua mke wangu na kipindi unataka kujifungua ningekupeleka muhimbili ili ujioneee ari alisi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom