Misunderstood
JF-Expert Member
- Aug 4, 2020
- 385
- 887
- Thread starter
- #21
Nimewahi kupitia unayopitia na ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuijua JF kwasababu katika kugoogle namna ya kusahau mtu nikaletwa huku JF
Nilikuwa natamani kulia lakini machozi hayaji
Appetite ikapotea
Nikapiga hata simu nyumbani kuomba kughairisha mwaka manake nilijiona hata darasani hakieleweki
Nikaweka uzi humu wa kuomba msaada wa namna ya kumsahau ambapo kimsingi nilipata mawazo kadhaa ambayo yalinisaidia kiasi chake
Kimsingi kilichonisaidia kupotezea ni baada ya kuweka mbele mambo ya msingi zaidi katika maisha yangu,nikaanza kutumia muda wangu mwingi kusoma sana kwasababu ndio kilinipeleka kule
Nikaanza kufikiria mtu nayempenda zaidi katika hii dunia ambaye ni baba yangu,nikaanza kuwasiliana nae sanaaaaaa
Nikaanza kwenda kanisani siku za jumapili na jumamosi kufanya usafi
Jitahidi kuwa busy na mambo yako,hayo unayopitia sasa hayatakuwa hivyo milele....pole,pambana
Oh asante mamy!