Mimi ni mmoja wa wahanga ambao watoto wao walidhalilishwa na kufedheheshwa na Serikali ya John Pombe Magufuli kwa kufukuzwa UDOM; yaani mwanangu ni 'kilaza' kwa mujibu wa Rais JPM.
Kabla ya kuitwa na Serikali ya Rais msikivu Jakaya Mrisho Kikwete kwenda kujiunga UDOM, kama mzazi nilikuwa tayari nimeishamfanyia mipango ya kuendelea na masomo katika fani nyingine kwenye chuo kingine.
Hata hivyo kwa kuzingatia Uzalendo, tulijadiliana na kijana wangu kuhusu suala hilo. Bahati nzuri kijana wangu naye ana uzalendo na nchi yake (like father like son) alikubali kwenda UDOM ili akitoka huko aje kusaidia kuimarisha sekta ya Elimu nchini hasa katika upande wa masomo ya Sayansi.
Sasa ndo hivyo Rais anayejinadi kuwatumikia wananchi masikini, kavuruga ndoto za kijana wangu.
Kuna baadhi ya ndugu zangu walinishauri nisimruhusu kijana kwenda UDOM kwa kile walichoita ukigeugeu wa Serikali hasa kiongozi mmoja anapoingia madarakani kuhakikisha anafuta nyayo za mtangulizi wake; mimi na kijana hatukulizingatia hilo.
Hoja yangu; Je?, naweza kuishitaki Serikali Mahakamani kwa kadhia hii?.
Nishaurini kwa hoja za kiweledi badala ya siasa.........Nawategemea zaidi Wanasheria.