Nimpe moyo kwakipi?
Kwanini hakudai kupewa moyo kabla sijazaliwa?
Kuchagua kunilea ni hisani?
Unajua maana ya hisani wewe?
Hicho kibaya wangenifabnyia na wala isingekuwa kitu kwangu na wangeenda kujibu tu
Siwezi kumshukuru mtu kutimiza wajibu wake
Yaani wewe uwashwe umtongoze mwanamke na umtie mimba bila kuomba ushauri wowote ule halafu eti uje udai ushukuriwe kwa hicho ulichokifanya .....!!!!!!!!!!!
Khaaaaa!!!!!!!!!
Napita...
Na wasingenilea wangekiona cha motoHahahhh kwani wewe uliwekeana mkataba na wazazi wako kwamba wakulee.?.
Unadhani kujua chochote kunanifaidisha nini mimi?Na ungewezaje kujua chochote kabla hujazaliwa!?
Kwanini wasinilee?Hahahahh utaombaje ushauri kwenye mambo ya kutongoza..
Na mfano wasinge kulea ungekuwa hivyo ulivyo?
Nimezaliwa kwa sababu kuna mtu ambae alifikiri hivyoAu mkuu we Hujazaliwa umezuka au?.
Ngumu kuelewa nini?Maana mgumu kweli kuelewa, au ndo kuelewa sana huko.
Na wasingenilea wangekiona cha moto
Unadhani kujua chochote kunanifaidisha nini mimi?
Kwanini wasinilee?
Nimezaliwa kwa sababu kuna mtu ambae alifikiri hivyo
Na alijua hiki anachokifanya ni lazima akilee
Na kukilea sio hisani ni lazima
Na hatakiwi kushukuriwa
Ngumu kuelewa nini?
Nimesema hivyo ili ionekane kuwa wanahitaji hisani yangu kwenye malezi yao kwanguKwahiyo unamaanisha nini kusema hawakukushirikisha wakati wanapanga kukuzaa!?
Kipi hujaelewa?Maana hueleweki msimamo wako ni upi.
Kwafano wasingekulea kwani ungewafanya nini..?
Nimesema hivyo ili ionekane kuwa wanahitaji hisani yangu kwenye malezi yao kwangu
Lakini hawajafanya hivyo
Kwanini unafikiri wanahitaji hisani yangu?
Hapo ndipo kwenye tatizoHee hisani yako kwao! Kwani wewe unawafanyia hisani ipi wazazi wako..
Mimi sijaongelea hicho..ndiomaana nasema hujanielewa..
Nilichoongea ni kuhusu KUHESHIMU, KUWAPENDA NA KUWATII wazazi..
Na pia KUSHUKURU kwa mema waliyokutendea.
sawa Eiyer
Ambae angewafanya kinachowastahili sio mimi ni Mungu
Hata wewe usijidanganye kuwa kuwalea wanao [kama wapo] ni hisani
Ukiacha utaenda kula kibano tu
Kama hutaki kulea ni bora usizae!
Hapo ndipo kwenye tatizo
Mema gani?
Kwanini niwashukuru?
Wale waliopandwa kama mchicha hapa hapawahusu.
Hivi hujawahi kukaa na kufikiria kidogo kuhusu wazazi wako?
Kila wanachokifanya kukuhusu wewe ni kwaajili yako.
Na hata kama kuna mahali wanakukosea au wanakosea bila kujua, kuna haja yoyote ya kuchukia au kuwa na kinyongo?!!
hakuna haja ya kuchukia au kuweka moyoni.
Cha muhimu ni kuweka mambo sawa, kuwaambia kwa uwazi nini unapendelea nini hupendi.
Kwasababu yote hayo wayafanyayo wanayafanya kwaajili ya kujitahidi uwe na amani na furaha na maisha mazuri.
Sikatai kuna wazazi wanatumia nguvu au ubabe au mamlaka waliyo nayo kuwakandamiza watoto wao, lakini wewe kama mwanawao unaweza kufanya kitu kurekebisha.. Hata ikibidi kushirikisha wana familia au ndugu wa ukoo kuhusu hilo. Pia kuna taasisi mbalimbali zinazo husiana jamii na mambo kama hayo zinazo weza kusaidia.
Kwahiyo wewe kama unajitambua unaelewa kabisa kila binadamu ameumbwa na MUNGU na kuwekwa hapa duniani kwa sababu Maalum.
Na kinacho takiwa kufanya ni Kuwaheshimu,kuwapenda na kuwatii wazazi/walezi wako, ili kumpendeza MUNGU.
Na sio wazazi tu au walezi,kila mtu ni vizuri kumheshimu na kuwa na amani naye.
** Hebu tulia na ufikirie kidogo kuhusu hilo.**
‪#‎NAWAPENDA‬ sana wazazi wangu, MUNGU awabariki..
#Nawapenda pia marafiki na ndugu zangu, MUNGU awabariki.
Wote kwa pamoja nawatakia Maisha mema.