Inauma sana lakini Lakuvunda halina ubani

Inauma sana lakini Lakuvunda halina ubani

Mommadou Keita

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2013
Posts
230
Reaction score
238
Baada ya jitihada za kumtafuta kwa muda mrefu, leo ndiyo tumebaini kwamba shemeji yangu amefariki dunia kwa kupigwa na mawe na watu wenye hasira kali hadi kufariki dunia.
Mara kadhaa nilijitahidi kuokoa maisha ya shemeji yangu huyo ambaye nimemuolea dada yake kwa kumpa mwongozo wa maisha lakini hakutaka kunielewa...
Mwanzoni mwa miaka ya 2000, nilimpeleke katika chuo cha TAMECO pale Keko, jijini Dar ili akasomee ufundi, nililipa ada kwa miesi sita tu lakini alifanya mahudhurio kwa miezi miwili au mitatu akaacha kuendelea na masomo, akarudi mtaani kujiunga na makundi ya kihuni.
Baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Magomeni kwa muda mrefu, hatimaye alitorokea Afrika Kusini, kwa kuwa alikuwa akisakwa na maaskari jina lake lilikuwa midomoni mwa mapolisi. nilijitahidi kuzungumza naye baada ya kukwama Malawi na kurudishwa nchini huku akiwa hana fedha za nauli, wenye basi wakazuia hati yake na mwenzake, nikalipa fedha na nikazuia hati yake ya kusafiria, ilikuwa ni kazi bure.
Mke wangu akaniambia nimpe hati yake ya kusafiria nikafanya hivyo huku nikimsihi atafute ujuzi wake binafsi ambao ungeweza kumsaidia huko Afrika Kusini lakini hakunielewa.
Baada ya muda nikasikia kuwa ametorokea tena kwenda, Afrika Kusini akiwa na mwenzake, huko kazi yake ilikuwa ni kuishi geto na kujihusisha na biashara ya kuuza madawa ya kulevya.
Mara moja moja alikuwa akipiga simu kwa dada yake na kumwambia: "Mwambie shemeji nitamletea gari ya kutembelea..." nilihuzunika sana lakini sikuwa na la kufanya kwa kuwa maji yalishamwagika, nilijua alikuwa akitoa ndoto za mchana.
Mwaka 2010, mama yake mzazi alifariki dunia, nikamwambia arudi nchini lakini wapi, aligoma aliendelea kupiga simu huku akiwa na wasichana wa Wakihindi na Wakizulu. Maisha yakaendelea kwa kasi sana... hatimaye akarudi nchini akiwa ameumia mguu baada ya kupigwa risasi ya mguu.
Aliporudi nilimwambia jinsi ya kijana mwenzake aliyekuwa naye kwenye kundi moja hapa nchini jinsi alivyouawa kwa kukanywanyakanyagwa na pikipiki na madereva wa bodaboda.... akajuta sana, akasema hatataka tena kujiingiza kwenye uhalifu.
Mwaka jana mimi na mke wangu tukampeleka Kigoma akaenda kusomea udereva katika chuo cha VETA, hatukutaka akae Dar es Salaam kwa sababu ya makundi yalikuwa yakimharibu sana, kweli alienda, nikajua amebadilika... akafanya vizuri kwenye chuo hicho hadi akasifiwa kwa uwezo wake wa akili.
Hatimaye akarejea Dar baada ya kupatikana kazi ya udereva katika kampuni moja kubwa tu, kila kitu kilikuwa vzr alitakiwa kuanza kazi, la kuvunda halina ubani... alienda siku moja tu kazini baada ya hapo akarejea tena kwenye kundi lake la wizi wa bodaboda.
Hata mwezi haujafika akanifuata nyumbani na kuniomba akae kwenye nyumba yangu mpya ambayo bado sijahamia kwa kuwa alikuwa hataki kukaa ukweni ( ndiyo alishaoa na kujaliwa kupata watoto wawili, mmoja hata mwaka hajatimiza na mwingine ni wa miaka minne au mitano) ili ajipange kabla ya kuhamia kwenye nyumba yake aliyokuwa akiijenga huko Mbande kutokana na fedha alizokuwa akimtumia mkewe akiwa Afrika Kusini.
Nikampa masharti ya kuacha wizi, akakubali kwa kuwa alikuwa na ujuzi, nikamwambia kama hataki kuwa dereva, basi akafanye hata kazi halali za kutuimia nguvu... akasema:
" Shemeji hata mimi sipendi kufanya wizi..."
Nikamruhusu kwenda kukaa katika mjengo wangu bila kinyongo.
Ni juzi tu nilipoambiwa na mke wangu kwamba shemeji yangu hajarudi nyumbani kwa siku tatu na mkewe analalamika, tukaanza kuwasiliana na masela wenzake.
Hakuna aliyekuwa akizungumza ukweli, wote walikuwa wakificha, mmoja akasema kwamba walikuwa naye Maisha Club, akakodi pikipiki huku akiwa amelewa na aliwapita eneo shule ya Oysterbay.
Jitihada za kumsaka zikaanza rasmi leo Jumapili, nikatoa gari langu kuanza kumtafuta, sehemu ya kwanza ilikuwa ni Segerea... hakuwepo, Keko, pia hakuwepo.... gari likaenda kusimama Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, pia hakuwepo.... mwisho wazo likasema gari liende Mwananyamala Hospitali.... alikuwa amejaa tele akiwa amelala katika wodi namba 0.... yaani chumba cha maiti, maisha yake yakiwa yameishia hapo...
Nikapata namba ya simu ya askari wa doria wa Oysterbay ambaye ndiye aliyeifikisha maiti yake hospitalini hapo...
Askari: Hebu niambie amekutwa wapi... Oysterbay Beach au...
Mimi: Oysterbay Beach
Askari: Aaaah! huyo alikuwa akijaribu kuiba pikipiki aina ya boxer, alikuwa na wenzake ambao walifanikiwa kukimbia kwa kutumia gari aina ya Noah, tulimkuta akivuta pumzi zake za mwisho.
Nilihudhunika sana, nililia kwa uchungu.. siwezi kuamini kwamba Mungu alipanga maisha yake yakatike mapema hivi... shemeji amefariki kutokana na maisha aliyoyachagua, ameaga dunia akiwa bado kijana mdogo... sidhani kama amefikisha hata miaks 25.
Inauma sana... uncle wake (mwanangu kuna siku ataniuliza) : Daddy Uncle..... yuko wapi? sijui hata nitamjibu nini.
Aaaah wadau acheni niende kwenye kikao cha mazishi, tunatarajia kumzika kesho (Jumatatu)... INAUMA SANA LAKINI.... LAKUVUNDA HALINA UBANI, ASANTENI.
 
Kweli inauma sana... vijana wengi wa siku hizi hawataki kuwasikiliza wakubwa zao.
 
Mkuu POLE SANA na MUNGU aiweke roho ya Shemeji yako panapostahili! You played your part; Usijilaumu kwani kama ulivyosema katika tittle ya uzi-Lakuvunda.........
 
Pole sn. Mungu atakupeni nguvu kwa mtihani huo. Amin
 
Pole Sana but that's kind of life he choose to live
 
pole mkuu...hawa wadogo zetu hawasikii kabisa...RIP Uncle
 
pole meku....ukichagua kazi hiyo si tu hujui mwisho wake hapana...unajua kabisa na lini itakua mwisho wako,trust me umefanya ulilotakiwa kufanya....
 
Mi nadhani kuna watu huzaliwa hivyo, hata ujitahidi vipi kumuusia hawasikii. Pole kamanda.
 
Poleni sana;
Vijana wamekuwa wavivu sana
Wanataka kupata pesa kwa njia za mkato mkato

R.I.P. Kijana wetu.
 
Pole sana;

Ulijitahidi kumrekebisha lakini LAKUVUNDA........


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
ajali kazini si umeona wengine walikimbia anyway, RIP
 
ndo baaasi tenaaaa....!mkuu tabia za wizi mara nyingine ni za kurithi...fanya uchunguzi upande wa wazaa chema wako...R.I.P mpigaji....napita mkuu
 
ndo baaasi tenaaaa....!mkuu tabia za wizi mara nyingine ni za kurithi...fanya uchunguzi upande wa wazaa chema wako...inaweza ikatokea mwanao(mpwa wa marehemu)naye akapita njia hizo hizo...CHUKUA HATUA...by the way R.I.P mpigaji....napita mkuu
 
Back
Top Bottom