Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,713
Kuna system ikiwekwa ingesaidia sana...kutoa mimba au kuweka mimba ni chaguo la mtu!mfano serekali imeweka katiba marufuku kwa utoaji mimba...je unaona inasaidia wakati kila kukicha watoto wanatupwa majalalani!Hio bado haitoshi watu wanatoa mimba kwa njia zisizo sahihi mpaka kupelekea kifo au kuharibikiwa kwa viungo vya uzazi!unadhani wanawake/wasichana wangefundishwa njia za uzazi wa mpango hayo yote yangetokea?Kwani wakati "asumani jicho moja" anachokora kule maeneo, huo umaskini ulikuwa hauonekani au ghafla bin vuu hawa mabinti hutoka katika hali ya utajiri kwenda kuwa masikini???
Lazima tutambue kuwa kila jambo lina mwanzo wake, huo ujauzito haukutokea kwa nguvu za miujiza bali kuna mtu aliyepanga kwenda kudinyana bila kufikiria mwisho wa dahari...