Inasikitisha jamani soma hii

Inasikitisha jamani soma hii

MNEKI

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
992
Reaction score
1,311
Baba na mama baada ya kurudi kazini pamoja wakakuta barua iko mezani sebuleni ikisema.

"Baba na mama, ni matumaini yangu kuwa mtasoma ujumbe wangu huu kwenye karatasi niliyoiweka juu ya meza, naomba msishtuke mana ni mambo ya kawaida kwenye maisha tunayoishi, najua mtaumia kwa vile bado nasoma na ndiyo nipo kidato cha kwanza."

Napenda kuwajulisha kwamba sasa hivi mnaposoma hii barua sipo nyumbani, nimetoroka mana nimegundua nina uwezo wa kujitegemea kwa sababu mi ni kijana mwenyewe umri wa miaka 14 na ninajua kipi chema na kipi kibaya.

Tangu mwezi mmoja uliopita nilikuwa na uhusiano nabinti mmoja aliyeitwa Rachel, mwenye umri wa miaka 27 na kwa sasa ndo naishi naye kwenyechumba alichopanga. Nilipokuwa nyumbani sikuwa napata (Inaendelea chini)
 
hela za kutosha ila sasa nimeanza kushika noti za shilingi 10,000...
Msichana niliyenaye ni mzuri sana wa umbo na ninampenda sana, amenifundisha njia za kutafuta hela. Amenipangia kazi ya kuuza madawa ya kulevya na yeye ikifika usiku anaenda kuuza mwili wake, basi kila siku tunapata hela ya kutosha, huyu mchumba wangu ni msichana mwenye bidii, kwa siku analala masaa 6 tu maana mwanaume yeyote akija lazima awe naye chumbani kwa muda wa
masaa 3. Msiwe na hofu, nipo salama kabisa na nimeamua kumwoa Rachel mana ni kila kitu kwangu. Pia amenunua gari la kubebea mbao kwahiyo biashara inaenda vizuri, Rachel ameenda kupima afya na amekutwa na upungufu wa kinga mwilini,mara nyingi namridhisha anapotaka kitu flani, iwe kufanya naye mazoezi ya viungo au kufanya naye mapenzi, si mnajua unapokuwa na mgonjwa
unakuwa naye karibu, ila mi pia sijihisi vizuri mana kila saa nakohoa tu na sina uhakika kama nimeathirika. Tumepanga baada ya miaka miwili tutawatembelea,nadhani mpaka miaka miwili iishe atakuwa ameshajifungua,na
 
ni furaha yangu mtamwona mjukuu wenu. Wazazi wangu sina la kuongeza kwaherini Mungu
akipenda tutaonana. NB: "Baba na mama, mi nipo chumbani kwangu najisomea,
mnachokisoma ni h/work ya mwalimu wa kiswahili alituambia tutunge hadithi fupi ya kusisimua, naomba muiangaliekama kuna makosa!"
 
Mkuu umenitoa roho yangu !! I am soulLess.
 
umeongeza chumvi sana ndo maana sijasikitika nikijua ni habari ya kuchongwa. Bora hata ungeishia pale mwanzo tu ningejiuliza huyu kijana atakuwa alienda wapi sasa na ningesikitika.
 
Wengi wenu hamjasoma hiyo hadithi mpaka mwisho. Hiyo ni Homework ya Mwanafunzi wa somo la kiswahili. Ndio maana nasema memba wa siku za hivi karibuni mnakurupuka tu. Fuatilieni jambo kwa makini. Ona sasa mnavyoonekana vilaza. Aibu tupu. Blali fuuu.
 
Mkuu umenitoa roho yangu !! I am soulLess.
Aisee hata mimi ilitaka kunitoa roho, fikiri sasa kama ni wazazi wa mtoto! Kabla ya kusoma mstari wa mwisho kuwa hiyo ni h/work baba na mama lazima wadondoke chini kwa pressure!!!
Sasa dogo anaweza akajikuta anapoteza wazazi kwa sababu ameitumia sanaa yake kwa kutumia ncha kali kwenye 'soft spot'!!!!!
 
hapo sasa..... duuh, na Dunia ya sasa basi !!!
well said..
 
kwanza makwenzi/.....pili mie na mwenza wangu tutakaa tujadiliane namna ya kujirekebisha manake toto limeandika kutokana na matukio ya home ya kunyimwa baadhi ya vitu na kuunganisha na mambo ayasikiayo kutoka kwa wenzie
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom