Hivi hakuna walioathiriwa na mgomo huo wanaoweza kufungua daawa mahakamani?!Mkuu wa Chuo Cha Usafirishaji kwa kauli aliyoitoa kwamba madereva warudi shuleni na hatimaye kusababisha mgomo katika sekta ya usafirishaji na matokeo ya mgomo huo kuleta hasara kubwa kwa taifa. Je; Mkuu huyo wa chuo anachukuliwa hatua gani baada ya serikali kusalimu amri kwa madereva?
Je; ni hasara kiasi gani iliyosababishwa na mgomo huo uliodumu kwa saa 9? Madhara ya mwananchi mmoja mmoja ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa kuchelewa/ kutofika kibaruani jana; wagonjwa kushindwa kufika hospitali kwa wakati n.k.
Je; Ni nani atakayeendelea kubeba mzigo huu pamoja na ule mgomo wa wafanyabiashara? Je; Nchi hii inaongozwa au inajiongoza?