Inashangaza Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) kuisemea Serikali

kwa kweli aliniacha hoi aliposema madereva oyeee utadhani anaomba kura za udiwani, nilicheka kwa kweli, huwa nakataa wanaposema kuishi kwingi ni kuona mengi ila ukweli ni kwamba kuishi tanzania ni kuona mengi

Tz patamu kama ukiwa na kitu mfukoni!!
utashangaa unapigiwa saluti na huku hata mgambo hujawahi pitia
 

aisee wanasiasa ni watu wabaya sana. yaani wanataka kumuangushia jumba bovu mhandisi mwenzangu Dr Mganilwa kienyeji-kienyeji tu hivi hivi??
Ajitokeze naye atueleze ya kwake, vinginevyo awajibishwe kwa usumbufu na hasara alizotusababishia, hata kama si leo au kesho.
 
kama mimi ni mkuu wa nit sikubali najitokeza kwenye media na makaratasi waliyosign, wasifanye baba watu aonekane ndo mbaya, itabidi jamaa ajisafishe
usicheze na system. Kabla ya kutoa nyaraka atapotezwa, mpaka muda huu atakuwa kisha pigwa biti kali
 
Serikali ilitakiwa ikanushe baada ya mkuu yule kutoa tamko lakini wamesubiri mpaka mgomo umetokea ndio wanamkana lakini hiyo ndiyo ilikua imetoka wasingeandamana na hii yaonyesha mambo mengi hufanywa na mtu mmoja tu watanzania tunafuata...ifikie mwisho sasa kuburuzwa!!
 
Kati ya wote aliyeniacha hoi ni kova tu....."Madereva oyee"Oyeeeee......alf akapiga kuanzia sasa hakuna toch....sasa sijui alifikiri kwanza kabla ya kuongea au alijilopokea tu.. .dah! Duniani humu....
 
Kati ya wote aliyeniacha hoi ni kova tu....."Madereva oyee"Oyeeeee......alf akapiga kuanzia sasa hakuna toch....sasa sijui alifikiri kwanza kabla ya kuongea au alijilopokea tu.. .dah! Duniani humu....

Hakuna tochi tena!? Usintanie mkuu! Uhuuuu! Oya tingo toa fyuz tutiririke mwendo wa basi mwanangu, leo hiihii tukalalie kobelo!
 
Kova naye " Waheshimiwa madereva nendeni na hakuna tochi na msibughudhiwe. MADEREVA HOYEE" wakati jana yake alitamba ya kuwa hakuna mgomo kwa sababu vinara alikuwa amewakamata.

Inaonekana viongozi wetu wanaongoza kufuata upepo badala ya sheria na taratibu za nchi. Inatakiwa Kova naye ahojiwe atoe ufafanuzi juu ya kauli yake, serikali imenunua vifaa yeye anasema visitumike mbaya zaidi anaongea hivyo mbele ya waziri. Nchi ngumu hii.
 
Nlisikia kuwa jana madereva waliambiwa wakanyage tu hakuna cha tochi wala kibatali njian, kumetokea ajali ngapi jana kutokana na mwendo kasi wa mabasi?
 
Hamna kitu kama hicho mkuu, japo serikiali iko kwenye AUTO PILOT, Lakini si kweli kuwa mkuu wa chuo cha NIT, angeweza kufanya hivyo, wao wameona ngoma imekuwa nzito acha wamuangushie jumba bovu tu, ili serikali ijisafishe kuwa sio wao!!! kama ni kweli hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake, kwani hasara na usumbufu uliojitokeza leo kwa wananchi ni mkubwa sana. Hiyo ni danganya toto tu, Sumatra, polisi wote walikuwa wanalijua hili mbona hawakuliona kuwa lingeleta mtafaruku?!! Yeye kova ni mtu wa kukurupuka tu na kutoa vitisho, bila kuangalia madhara, na ja ajabu huwa hawajifunzi kuwa siku hizi vitisho havisaidii tena kwa watu wanaokuwa na umoja na wako kwenye haki.Wakati wa mzozo leo pale ubungo madreva wengi walikuwa wanakunywa viroba muda wote walipo kuwa wanangojea hatima yao, cha ajabu walipofikia mwafaka baada ya serikali KUUFYATA, ni kuwaruhusu kuanza safari mala moja!!ki usalama bora mabasi yangeanza safari kesho tu. KOVA wakati mwingine uwe unachanganya na zako heeee!!!
Mchawi mweupe hakika ume hit the point.Siyo rahisi kwa Mkuu wa Chuo kutoa maamzi kama yale pasipo kuelekezwa.
Hiyo ilikuwa ni deal sema Mdereva wamekuwa Wajanja na hivyo limewakurupusha wahusika.Tunaenda kwenye gurio la kura mwezi wa kumi hivyo kila Mteja yuko busy kutafuta purchasing power.
 

aisee wanasiasa ni watu wabaya sana. yaani wanataka kumuangushia jumba bovu mhandisi mwenzangu Dr Mganilwa kienyeji-kienyeji tu hivi hivi??

Hiyo ilikuwa vunga tu.Mkuu wa chuo hicho alikuwa na ubavu gani wa kutangaza hilo jambo;ni serikali isipokuwa walitaka wasijulikane;wakaona imekuwa issue,mbona hawakusema watachukua hatua dhidu yake?ACHANA na SIRIKALI waliona itakuwa NOMA kwao.Hilo lilikuwa tamko lao,wamefyata,WANGESEMAJE?Kumbuka uchaguzi umekaribia,WALIKUWA WANAJIKOSHA.Msiwe wageni nchini kwenu
 
Mkuu wa Chuo Cha Usafirishaji kwa kauli aliyoitoa kwamba madereva warudi shuleni na hatimaye kusababisha mgomo katika sekta ya usafirishaji na matokeo ya mgomo huo kuleta hasara kubwa kwa taifa. Je; Mkuu huyo wa chuo anachukuliwa hatua gani baada ya serikali kusalimu amri kwa madereva?

Je; ni hasara kiasi gani iliyosababishwa na mgomo huo uliodumu kwa saa 9? Madhara ya mwananchi mmoja mmoja ni pamoja na kufukuzwa kazi kwa kuchelewa/ kutofika kibaruani jana; wagonjwa kushindwa kufika hospitali kwa wakati n.k.

Je; Ni nani atakayeendelea kubeba mzigo huu pamoja na ule mgomo wa wafanyabiashara? Je; Nchi hii inaongozwa au inajiongoza?
 
Sipati picha mapato yangeyopatikana endapo Chuo kingefanikiwa hiyo issue.
We chukua madereva wote nchi nzima waende kusoma Pale.Wengine naona kazi wangeacha

Kila miaka mitatu,kwa maana hiyo kila mwaka chuo kingekuwa full mtete.

Ada Tsh:580,000 x malaki ya madereva,kila mwaka fungu kuuuubwwaa.
Aisee hapa chuo kingetusua kweli.Lakini issue imebuma.
Ngoja tujipange upya.
 
Back
Top Bottom