Inashangaza Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Tanzania (NIT) kuisemea Serikali

tamimusalim

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
1,822
494
Katika hali ya kushangaza kabisa, kufuatia mgomo wa madereva ulianza leo na kumalizika mchana bahada ya waziri wa kazi bi, Gaudensia Kabaka kutoa tamko.

Ilinifanya nifuatilie chini chini kujua nani alitoa tamko ambalo lilisababisha madereva kugoma kuanzia bodaboda mpaka mabasi ya abiria na kusababisha usumbufu kwa abiria lakini kuikosesha mapato serikali yetu, nikagundua tamko halikuwa la serikali bali lilikuwa tamko la mkuu wa chuo.

Ukweli hii imenisikitisha sana mkuu wa chuo amekuwa na nguvu kiasi gani mpaka kutoa tamko kama lile bila woga na kutaka kuleta uvunjifu wa amani licha ya hasara serikali ambayo imeipata.

Kuthibitisha hilo leo waziri wa ajira amethibitisha kwamba tamko hilo halikuwa la serikali lilikuwa na mkuu wa chuo hicho (N.I.T).

Sasa kama serikali inakosa msemaji mpaka mkuu wa chuo anaropoka tu hii ni aibu kubwa.

Huyu mkuu wa chuo akamatwe na afunguliwe mashitaka, leo yeye kesho mkuu wa shule ataisemea serikali.

Hii ni aibu kubwa kwa serikali yetu, it is horrible!!!!
 
Yaani huu ndiyo udhaifu dhahiri wa serikali yetu.. Hivi inatokeaje mtu mmoja akajitangazia mambo ambayo kiuhalisia hayatekelezeki..

Hapa kuna uonevu mkubwa sana juu ya madereva.. Udereva ni fani kama fani zingine.. Mbona hawajatangaza madaktari nao warudi vyuoni kwa sababu vifo vya wagonjwa vimeongezeka??

Mbona haiwambii walimu warudi vyuoni kwa sababu ufaulu kila siku unashuka..

Mbona haiwaambii wachumi warudi vyuoni kwa sababu uchumi kila siku unadorora??

Tuwe wakweli.. huu ni uonevu wa dhahiri.. Yaan Serikalini kila mtu anatafuta deal la kufanya ili apate fedha..

This is shame!!!
 
Hamna kitu kama hicho mkuu, japo serikiali iko kwenye AUTO PILOT, Lakini si kweli kuwa mkuu wa chuo cha NIT, angeweza kufanya hivyo, wao wameona ngoma imekuwa nzito acha wamuangushie jumba bovu tu, ili serikali ijisafishe kuwa sio wao!!! kama ni kweli hatua stahiki zichukuliwe dhidi yake, kwani hasara na usumbufu uliojitokeza leo kwa wananchi ni mkubwa sana. Hiyo ni danganya toto tu, Sumatra, polisi wote walikuwa wanalijua hili mbona hawakuliona kuwa lingeleta mtafaruku?!! Yeye kova ni mtu wa kukurupuka tu na kutoa vitisho, bila kuangalia madhara, na ja ajabu huwa hawajifunzi kuwa siku hizi vitisho havisaidii tena kwa watu wanaokuwa na umoja na wako kwenye haki.Wakati wa mzozo leo pale ubungo madreva wengi walikuwa wanakunywa viroba muda wote walipo kuwa wanangojea hatima yao, cha ajabu walipofikia mwafaka baada ya serikali KUUFYATA, ni kuwaruhusu kuanza safari mala moja!!ki usalama bora mabasi yangeanza safari kesho tu. KOVA wakati mwingine uwe unachanganya na zako heeee!!!
 
Huyo Mkuu wa Chuo ni kweli anatakiwa ashtakiwe kwa kuingilia majukumu ambayo si ya kwake. Licha ya hilo Kova nae nimeona akisema tochi hakuna, ametoa tamko hilo akiwa kama nani?
 
huyo mkuu wa chuo katumwa na hiyo hiyo serikali ajashauriwa na mkewe ndio maana serikali haikukana hilo tamko na hata madereva walipotangaza mgomo siku 7 nyuma serikali haikuweka mambo sawa kwa kusema sio tamko lao

#Zitto
 
Yaani huu ndiyo udhaifu dhahiri wa serikali yetu.. Hivi inatokeaje mtu mmoja akajitangazia mambo ambayo kiuhalisia hayatekelezeki..

Hapa kuna uonevu mkubwa sana juu ya madereva.. Udereva ni fani kama fani zingine.. Mbona hawajatangaza madaktari nao warudi vyuoni kwa sababu vifo vya wagonjwa vimeongezeka??

Mbona haiwambii walimu warudi vyuoni kwa sababu ufaulu kila siku unashuka..

Mbona haiwaambii wachumi warudi vyuoni kwa sababu uchumi kila siku unadorora??

Tuwe wakweli.. huu ni uonevu wa dhahiri.. Yaan Serikalini kila mtu anatafuta deal la kufanya ili apate fedha..

This is shame!!!

Baba akiwa dhaifu nyumbani watoto hufanya watakalo na hivi ndio serekali yetu ilivyo.
 
Yaani huu ndiyo udhaifu dhahiri wa serikali yetu.. Hivi inatokeaje mtu mmoja akajitangazia mambo ambayo kiuhalisia hayatekelezeki..

Hapa kuna uonevu mkubwa sana juu ya madereva.. Udereva ni fani kama fani zingine.. Mbona hawajatangaza madaktari nao warudi vyuoni kwa sababu vifo vya wagonjwa vimeongezeka??

Mbona haiwambii walimu warudi vyuoni kwa sababu ufaulu kila siku unashuka..

Mbona haiwaambii wachumi warudi vyuoni kwa sababu uchumi kila siku unadorora??

Tuwe wakweli.. huu ni uonevu wa dhahiri.. Yaan Serikalini kila mtu anatafuta deal la kufanya ili apate fedha..

This is shame!!!

Tatizo kubwa zaidi liko kwa wale ealioanzisha mgomo kwa tamko la Mkuu wa Chuo Kama ni kweli yeye ndiye chanzo cha madereva kugoma.
Kwa tz no wonder , kama konda wa daladala anaweza panga abiria wake Kama magunia ya mkaa kwa kauli tu ! Tena akiwa nje ya daladala itakuwa ni hulka ya Watz kutitafakari na kusimamia ukweli...
 
huyo mkuu wa chuo katumwa na hiyo hiyo serikali ajashauriwa na mkewe ndio maana serikali haikukana hilo tamko na hata madereva walipotangaza mgomo siku 7 nyuma serikali haikuweka mambo sawa kwa kusema sio tamko lao

#Zitto

Asante kaka kumbe upoo, chukua nchi mbona unaweza kaka uozo kama huu hatuutaki hata kidogo
 
huyo mkuu wa chuo katumwa na hiyo hiyo serikali ajashauriwa na mkewe ndio maana serikali haikukana hilo tamko na hata madereva walipotangaza mgomo siku 7 nyuma serikali haikuweka mambo sawa kwa kusema sio tamko lao

#Zitto

Naamini mkuu wa chuo yuko sahihi, na naamini hakukaa tu akajitungia, ila ni busara tu imetumika, lakini kamwe haiwez kuwa ni Mkuu wa NIT kajiamulia.Ila ku neutralize ilipaswa iwe vile alivyosema mh Waziri. By the way, Serikali ni nani¿ Mkuu wa chuo nae ni Serikali, mtekelezaji wa maagizo, au ni mtendaji!
 
Yaani huu ndiyo udhaifu dhahiri wa serikali yetu.. Hivi inatokeaje mtu mmoja akajitangazia mambo ambayo kiuhalisia hayatekelezeki..

Hapa kuna uonevu mkubwa sana juu ya madereva.. Udereva ni fani kama fani zingine.. Mbona hawajatangaza madaktari nao warudi vyuoni kwa sababu vifo vya wagonjwa vimeongezeka??

Mbona haiwambii walimu warudi vyuoni kwa sababu ufaulu kila siku unashuka..

Mbona haiwaambii wachumi warudi vyuoni kwa sababu uchumi kila siku unadorora??

Tuwe wakweli.. huu ni uonevu wa dhahiri.. Yaan Serikalini kila mtu anatafuta deal la kufanya ili apate fedha..

This is shame!!!
Serikali dhaifu kila kitu ni dhaifu wanawaza deal tu
 
Wana JF hii story sio kweli ni changa la macho tu huyo mkuu wa chuo anaujasiri gani mpaka atangaze hayo?
 
Ulikuwapo ubungo wakati kova na kabaka wanawatangazia madereva, ok sawa ukuwepo umetazama taharifa ya habari star tv, itv saa 2 usiku au unapenda kubisha vitu ambavyo viko wazi mkuu
 
Yaani huu ndiyo udhaifu dhahiri wa serikali yetu.. Hivi inatokeaje mtu mmoja akajitangazia mambo ambayo kiuhalisia hayatekelezeki..

Hapa kuna uonevu mkubwa sana juu ya madereva.. Udereva ni fani kama fani zingine.. Mbona hawajatangaza madaktari nao warudi vyuoni kwa sababu vifo vya wagonjwa vimeongezeka??

Mbona haiwambii walimu warudi vyuoni kwa sababu ufaulu kila siku unashuka..

Mbona haiwaambii wachumi warudi vyuoni kwa sababu uchumi kila siku unadorora??

Tuwe wakweli.. huu ni uonevu wa dhahiri.. Yaan Serikalini kila mtu anatafuta deal la kufanya ili apate fedha..

This is shame!!!
Wizara ni lszima ina mkurugenxi wa mafunxo ambapo idara vyuo vyote vina ripoti kwake.
Naye kimyaaa!
Utafikiri hayupo kuongoza walio chini yake
AJIUZULU
 
Mbona hawaambii Polisi warudi CCP Kwa ajili wanaporwa silaha kila kukicha.
Mkuu hiyo ni dili Polisi, NIT na Sumatra. Dereva mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 10 anajifunza nini cha ziada? Kikubwa ni kuchange attitude ambayo kamwe haiwezi kubadilishiwa shule na pia kupanua na kukarabati barabara
 
Tanzani tumejitahidi sana kujiongoza yaani ten years without goverment kweli tunajiweza.
 
Habari wana jamvi,

Jana wakati Mheshimiwa Waziri akihutubia Madereva katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo, alisikika akisema kwamba taarifa iliyotolewa na kiongozi wa NIT kuhusu gharama ya masomo ya baada ya muda wa Leseni ya Udereva kumalizika haikuwepo Serikalini na yalikuwa ni ya kwake huyo kiongozi.

Sasa inakuwaje katika nchi injyoongozwa na sheria na taratibu, inatokea mtu tu anaamua tu kufanya jambo kubwa kama hilo yeye mwenyewe? Kama ni kweli kwa kile kilichotokea jana kwa kiasi kikubwa kilichcheowa na kauli za huyo kiongozi, kwa maana hiyo anastahili kuwajibishwa.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom