Inaniuma sana lakini nitafanyaje, inabidi niwe mnafiki tu

kiroka

JF-Expert Member
Feb 28, 2018
355
1,856
Nina mdogo wangu mtoto wa mjomba yangu tumbo moja na Mama angu, huyu dogo nimekua nae kama mdogo wangu tumbo moja na jamii inajua tumezaliwa pamoja, kwa uku mjini tunaish mtaa mmoja

Shida inakuja dogo alipata demu mmoja ivi lakini cjui walikutana wapi demu mwenyewe wa singida nilijaribu kumuuliza alimpata wapi hajanijib mpk leo

Wakati wanaanza mahusiano dogo alinambia demu wake kwao maisha safi na stori kibao wakati huo dogo yupo kwao, mara gafla demu akaja dar dogo akanambia demu amefunguliwa duka na wazazi wake apa mjini mara dogo akachange stor akasema demu ana taaluma ya computer kaajiriwa kwenye shule flani km secretary lkn katika mizunguuko yote hyo dogo akanunua vitu vya ndani akalipa Kodi akamuweka demu akae umo ili iwe rahis kula mzigo

Mara demu akapata ujauzito akajifungua mtoto ikawa bahati mbaya, cku ya mazishi ya kichanga ndo mambo yakaanza kua wazi hakuna hata ndugu mmoja wa demu aliekuepo isipokua sisi upande wa kiumeni tu nikamuuliza dogo mbona wakwe wako hmn hata mmoja wala simu ya kuwapeni pole wala mtu wa kumfutilia huyu mwanamke vipi

Baadae demu akaja kukiri kwa dogo kua kwao hamna kitu maisha magumu inshot stor zoote alizompa dogo kwa mara ya kwanza ilikua uongo na visa vingi vingi saana, nikamshauri dogo ampige chini dogo akaelewa mkakakati ukawa dogo amwachie chumba aendelee na maisha yake likapita Hilo kumbe dogo akawa anaenda kwa Siri penzi likarud upyaaa.wakarudiana mwisho teena wakazinguana wakapigana saana nikaitwa kwnda kuwaamulia nikampka saana dogo nikamwambia c tulikubaliana uachane na huyu demu dogo akakir nisamehe brother yakaisha dogo akahamia tena kwa demu hapo demu tangu ajifungue hana kazi dogo ndo akawa analipa Kodi na kutoa pesa ya kula

Dogo akarudi tena kwa demu Safari hii hajaniambia chochote tukionana anakimbia kimbia kunikwepa hatimae demu akabeba mimba nyingine nikajua dogo kayakanyaga demu msumbufu ivi azae nae c majanga haya baas bhana demu akawa mimba imekua kama ugonjwa kila siku hospital akipimwa hakuna ugonjwa dogo akawa anateketeza pesa tu.

Siku ya siku tukaenda kijijini kwetu tukamkuta mama angu ambae kwake ni shangazi lkn km mama yake akamwambia mama kuhusu habari za ujauzito wa demu wake Mimi nikaanza kumchana dogo mbele ya bi mkubwa kuhusu mapungufu ya demu na jinsi anavomkost dogo nae akawaka bi mkubwa akaniwakia saana kwann nimchagulie mwenzangu mke wakat mimi cjachaguliwa na mtu,nikakaa kimya

Kimbembe kinakuja demu kajifungua mtoto hafanani na dogo hata kidogo kafanana na jamaa mmoja mtaani kwetu inasemekana huyo jamaa alikua anamla demu watu mtaani wananambia mdogo wako kaibiwa dogo ndo hasikii na kwa hili la demu kuliwa cjamwambia na kuhusu mtoto kufanan na mtu mtaani cjamwambia dogo haoni wala hasikii

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Umeamua kua mnafiki. Sasa umeshindwa vipi mwambia kua mtoto hafanani naye anafanana na mtu mwingine.

Kikubwa muache dogo apambane nawakati na yeye aje pata cha kusimulia kuhusu mapenzi
 
Mwanaume mzima unakuwaje mbeya?!! Kwani wewe ndio unamlisha? Mwache na maisha yake, au unamtaka wewe huyo mwanamke? Ptuuuuuuu!!
 
Nina mdogo wangu mtoto wa mjomba yangu tumbo moja na Mama angu, huyu dogo nimekua nae kama mdogo wangu tumbo moja na jamii inajua tumezaliwa pamoja, kwa uku mjini tunaish mtaa mmoja

Shida inakuja dogo alipata demu mmoja ivi lakini cjui walikutana wapi demu mwenyewe wa singida nilijaribu kumuuliza alimpata wapi hajanijib mpk leo
Mkuu hauna yako ya kufuatilia
 
Back
Top Bottom